REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HIVI ICE PRINCE WA NIGERIA ANAJICHUBUA?..AMA?

5:46:00 AM Add Comment

Wengi Tunajua Mtakuwa Mnafahamu Kwaju la Oleku la Kwake Ice Prince..Kweli Si Kweli?

Sasa, TEAMTUKOMBELE tumepaa hili Jingine kutoka Obina land.
Iko Hivi, Hivi majuzi kati ya mafanz wa ICE PRINCE alishare Picha ya Msanii huyo katika Account ya facebook na Kupost kuwa Eti Mshikaji anajichubua a.k.a anajikwatua.


Baada ya Mnato huo kuwekwa, Membaz Kibao ambao wanaupenda sana Mziki wa ICE PRINCE walianza kukoment kua Jombaa anajikwatua kutokana na baadhi ya Weusi katika baadhi ya Sehemu kama vile kwenye Vidole na kadharika.



Baada ya kuwa Topic Sana kuhusu hilo, ICE PRINCE alijitoa Mbele kama Sie na kuzungumzia Tuhuma Hizo, huku akizikanusha Vikali Kupita maelezo na kusema Kuwa, Suala la Kujichubua Kwa Upande wake, Hebu sahauni kabisaaaaaa.

MAMA MTOTO WA RICK ROSS KUMSHITAKI 50 CENT KWA KUVUJISHA VIDEO CLIP YAKE YA NGONO

5:38:00 AM Add Comment

Oshalalalaaaaaa..Kila kitu kiko Mbele maze kama Hivi.

Mchakato ambao Umefika Kunako Meza ya TEAM TUKO MBELE, ni Kumuhusu rapper JACKSON CURTIS “50 CENTS” kuvujisha Video ya Ngono a.k.a Weka Mbali na watoto ya Mzazi Mwenzake na Rick Ross “Rozay” anayefahamika kwa Jina la LASTONIA LEVISTONE

Kwa Mujibu wa data halisi ni kwamba 50 CENTS alivujisha Video Hiyo wakati bado yuko ndani ya BEEF KALI na hasimu wake Rozay, huku ikimuonesha Mama huyo akikunjuka Vema na Jamaa aliyetambulika kwa Jina  MOURICE MURRAY ambaye anadaiwa kuwa ndiye alimpenyezea FIF Clip Hiyo.

Katika Video Hiyo, Jombaa huyo Murray anaonekana upande wa Uso, huku Mzazi Mwenzake na Rick Ross ambaye hivi sasa ni Ex- Lover wake, akionekana Mzima mzima Kudaadeki.


Video Clip Hiyo iliweza Kutazamwa na Jumala ya watu Milioni 3.2 Ulimwenguni Muda Mchache baada ya Mwanababy LEVISTON kufungua Mashtaka Dhidi ya 50 Cents. Juma lililopita, Jaji wa mahakama ya MANHATTAN Nchini Marekani aliahirisha kesi hiyo mpaka Muafaka Utakapojulikana

FREEWAY RICK ROSS HAJAKATA TAMAA

5:34:00 AM Add Comment

FREEWAY RICK ROSS ambaye Ndiye anayedaiwa kuwa mmiliki wa Jina la RICK ROSS, ametoa Tamko kuhusu Rick Ross “Rozay” kuchukua Jina lake na hata Kupata Ushindi mahakamani.
Akizungumza Kwa Uchungu kuhusu Hilo akiwa na Hisia kali,  Freeway Rick Ross amesema kuwa binafsi yeye kama yeye anauheshimu Muziki wa HIP HOP, na hata baadhi ya wasanii ni Marafiki zake.

Pia Freeway ameongeza Kuwa, Kwa kuwa Muziki wa Hip Hop Unazungumzia Ukweli, Huwezi kutoka hapa na Kwenda Kule ukajitapa Kuwa Unafanya Muziki wa Hip Hop, na hip Hop Ipo katika damu yako wakati Bado unasema Uwongo kwa jamii hasa Vijana
Free way amezidi kudai Kuwa, anastaajabishwa na Mmoja wa maofisa wa Zamani (Rick Ross) kuamua Kutumia Jina lake na Kila Kitu chake ili aweze kupata Umaarufu na hata eti kukubalika Kwa jamii kuwa Ni Mtu wa watu, na hatimaye kupata mafanikio makubwa.

Kitu Hicho kimeonekana kumuudhi sana  Free way Rick Ross huku akizidi kusisitiza Kuwa, bado atazunguka kila eneo husika ikiwemo katika Shule mbali mbali, ili aweze kutoa Elimu na Kuzungumza Ukweli kuhusu yeye, maisha yake na madawa ya kulevya, pamoja na mambo ya Msingi ambayo kijana anatakiwa kuyafanya.

Pia Free way amemalizia kwa kusema kuwa, yuko Mbioni kuachia kitabu chakekinachomuhusu yeye na maisha yake, pamoja na Filamu ambayo itakuwa na mafunzo kwa vijana.

MNADA BANNER