REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

LOVE KITAA: ETI KANGAYE YA NYAKATO-MWANZA..INA WEZI WENGI?

8:27:00 AM Add Comment
PICHA : Kwa Hisani ya G-SENGO BLOG

Na Baba Juti

LOVE KITAA kutoka Kunako Kipindi Cha Hiot Zone ya 93.7 JEMBE FM, Iliweza kufika mpaka Eneo la KANGAYE lililoko Nyakato Mwanza , na kufurahia Story kadhaa kutoka kwa Wakazi wa eneo hilo.

Hivi Ndivyo ambavyo nilipiga Story na Ndugu zangu hawa wa Kangaye


MILEY CYRUS: NINASIKILIZA SANA WIMBO WA HUMBLE SABABU HAUZUNGUMZII NGONO.

7:10:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
HATIMAYE Mkali Wa Pop kwa Upande wa akina Dada, Miley Cyrus ameweka wazi kile ambacho huwa kinamfanya asifurahie sana kuwa karibu na Muziki wa Hip Hop, ingawa kuna mmoja ambao anaufuatilia na anaupenda

Miley Cyrus amesema kuwa amekuwa akimsikiliza Sana Kendrick Lamar hasa kupitia Mkwaju wa HUMBLE ambao anadai kuwa ni kwa sababu ujumbe wake hauzungumzii masuala ya Bangi, madawa ya Kulevya, na maneno ya Ngono ngono.
Wimbo wa Humble wa kwake Kendrick Lamar, ndio unaomkosha Zaidi Miley Cyrus sababu hauna maneno makorofi

Bibie huyu ambaye alifanya Po asana na mkwaju wa “WRECKING BALL” amedai kuwa, kuna muda huwa hataki kabisa kujihusiosha na Masuala ya Hip Hop na hata kutokupenda kusikiliza, na hii ni kwa sababu asilimia kubwa maneno yanayopatikana katika Mashairi yao, ni Pombe, Bangi, Madawa ya Kulevya, na wanawake  kudhalilishwa na maneno ya ngono ngono kuhusishwa Mara kwa mara
Miley Cyrus amewahi kufanya Kazi na Rapper/Producer Mike Will Made It (Kulia) katika Wimbo unaitwa "23" wakiwa wamemshirikisha Wiz Khalifa


“ Ninaupenda Wimbo wa Humble kwa sababu hauna maneno kama Vile, Njoo nifanye ngono na wewe na mengineyo, vitu ambavyo siwezi kuusikiliza hata Kidogo. N hicho ndicho kilinitenganisha na Hip Hop. Kumejaa Lamborghin, nina Rolex, nina mwanamke juu ya uume wangu, navuta Bangi, na kadhalika”

MARIAH CAREY: ANAKULA POMBE NI BALAA

7:02:00 AM Add Comment
Mariah Carey anadaiwa Kunywa Pombe sana katika Kipindi Hiki

Na Baba Juti
WATU WA MUNGU  Inasemekana kuwa Mariah carey Hivi sasa anakunja Pombe balaa tangu ameachana na Boyfriend wake a.k.a Kiserengeti Boy Chake a.k.a Mkata Viuno wake, BRYAN TANAKA

Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka Kwa watu wa karibu hasa kunako management yake, wamedai kuwa wanaanza kuhofia Hali ya Mariah Carey kwa Hivi sasa sababu amekuwa ni Mtu wa Kutungua Chupa Nyingi za Mtungi kuliko ambavyo inadhaniwa, nah ii ni baada ya kuachana na Tanaka
BRYAN TANAKA anadaiwa kuachana na Mariah Carey kwa sababu kitendo cha Mariah Kutoka na Nick Canon (aliyekuwa Mume wake na wamezaa watoto wawili) katika Tuzo za Watoto, kilitafsirika kama ni dharau kwake

Mmoja kati ya Member wa Management ya Mariah Carey ambaye hakutaka aanikwe hadharani ili kulinda Msosi wake, anadai kuwa haikuwa kawaida kwa Mariah Carey kupiga Tungi kiasi cha kukwaza hata watu wengine huku dalili za stress za kuachwa na Boy wake zikiwa hadharani kabisa
Tofauti na Hilo, Chanzo hicho kimedai kuwa, hufikia Muda Mariah Carey hataki hata kujihusisha na Kazi ya aina yoyote huku akiwapa wakati Mgumu


“Kama mtakuwa mlimuona Hivi majuzi alipoingia kwenye Mgahawa wa CATCH ulioko Hollywood, alikaa kama masaa matano, lakini alipotoka Nje Tu, alikuwa amelewa sana kiasi cha kushindwa kupanda Gari yeye Peke yake. Na hata kuwa hurru sana kwa Mashabiki wake pasipo kubaini kuwa baya lolote linaweza kumtokea”

TIZAMA PICHA ZA MARIAH CAREY NA TANAKA ENZI ZA MAHABA YAO






DJ SNAKE NA LIL JON: WAMEIBA WIMBO WA TURN DOWN FOR WHAT !!!

6:52:00 AM Add Comment
DJ SNAKE
Na Baba Juti
Sasa, hii System inaelekea kuwa Ya Moto zaidi kiasi kwamba watu inabidi muwe makini zaidi aisee.

Mwaka 2014, DJ SNAKE na LIL JOHN walishtua Ulimwengu wa Burudani na kuwafanya Baadhi kuwa Wehu hasa unapopigwa Mkwaju wa TURN DOWN FOR WHAT, lakini kumbe Mzigo huo ulikuwa ni Wa Kuiba mazee
LIL JON

Kampuni ya GOLDEN CROWN PUBLISHING ndio ambao wamefungua Mashtaka hayo siku ya jana, dhidi ya Wasanii hao wawili, wakidai kuwa Rapper FREDDIE GZ ndiye mmiliki halali wa Idea na Mkwaju huo wa Turn Down For What, na yeye ndiye alikuwa Msanii wa Kwanza kuuachia.

Kampuni hiyo ambayo inawakilishwa na RICHARD BUSCH ambaye pia laikuwa katika Upande wa Utetezi katika Wimbo wa “Blurred Lines” na hatimaye familia ya Marvin Gaye kushinda, anadai kuwa Watu watatu ambao ni FREDLEY SAURE (Freddy GZ) MALIKI SANKOH na ROBERSON BONJEAN, ndio waliopika Idea ya TURN DOWN FOR WHAT  mwaka 2012.
FREDDIE GZ

Pia maelezo yanaendelea kumiminika kuwa, Mwaka 2013 walifanikiwa kurekodi  mwaka 2013 na kisha kuachiwa Rasmi March Mwaka 2013. Kitu ambacho Freddie GZ anakiongeza ni kuwa, baada ya kuachiwa tu, basi mitandao mingi ya Kijamii na hata watangazaji mbali mbali wa Radio za Hip Hop Nchini Marekani waliukubali na kuutabiria Mengi Mazuri

Lakini mnamo July 2013 walioshangaa kumuona Lil Jon na Dj Snake wakitweet kuhusu neon TURN DOWN FOR WHAT, mara LETS GO, na kisha Mkwaju kuachiwa Rasmi


“Baada ya Freddie GZ kuachia Wimbo wake March 2013, Dj Snake na Lil Jon waliachia tena wimbo wenye Jina Hilo hilo, na Kutumia vionjo vile vile vya Kazi ambayo ni Original” walidai walalamikaji

MNADA BANNER