REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HUYU NDIYE RAFIKI WA KWELI : THE ROCK HUPENDA KUGAWA MAGARI BURE

2:23:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi  
KAMA itaokea akawepo mtu wa aina hii hapa nchini Tanzania, ambaye ana moyo wa aina hii, na anajitoa kwa njia hii bila kinyongo, basi wabongo tutajiweka naye karibu hasa ukizingatia shobo na udananda ndo mahali petu katika kipindi hiki kigumu kimaisha

DAWYNE JOHNSON a.k.a THE ROCK ambaye ni actor bin Muigizaji wa filamu nchini Marekani, ameweka wazi kuwa tatizo lake kubwa, na ugonjwa wake mkubwa katika maisha yake, ni kugawa magari kwa watu.

Akifafanua kauli yake, The Rock ambaye zamani alikuwa ni mwanamieleka ambaye alijikita katika filamu na kuvutia zaidi katika Filamu kama vile Fast & Furious, Jumanji, na nyinginezo, anadai kuwa chanzo cha hayo yote ni baba Yake, Mzee Rocky Johnson ambaye aliwahi kumtamkia kuwa anahitaji gari la thamani kutoka kwa mwanaye

The Rock alisema kuwa, kuna kipindi baba yake mzazi ambaye pia zamani alikuwa ni mwanamieleka, alipata tatizo katika upande wa Hips moja hivyo ikamlazimu amdanga mtoto wake kuwa daktari ameshauri atumie gari la gharama (jina limehifadhiwa kibiashara) kitu ambacho kilimchekesha sana The Rock lakini akabaini kuwa baba anatamani tu apate gari la hivyo wala sio ushauri wa daktari

Hata hivyo, The Rock hagawi magari kwa watu baki, bali huwa anagawa kwa marafiki, Familia yake, na watu wengine wa karibu zaidi

EXCLUSIVE: DJ KHALED ANAHITAJI KUPUMZIKA

1:37:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
#WATUWAMUNGU wengi tunafahamu kabisa kuwa ili mkono uweze kwenda kinywani, lazima uhakikishe kabisa unapiga kazi kufa na kupona, ikibidi pasipo kulala kabisa ili mambo yako yasogee, na hii imekuwa ikijoptekeza mara kwa mara kwa wasanii mbali mbali kupiga show na kupromote kazi zao pasipo kupumzika.

DJ KHALED ambaye hivi sasa anafanya vizuri na Album yake Mpya "FATHER OF ASAHD" amekuwa katika tours mbali mbali na gigs kadha wa kadha ili kuwashibisha mashabiki wake hasa kupitia Burudani yake ambayo inafurahiwa na watu wengi sana ulimwenguni.

Na tangu ameachia Album yake hiyo, amekuwa akifanya kazi ya kui-promote maeneo mbali mbali pasipo kupumzika vizuri, kitu ambacho kimemfanya achukue uamuzi mwingine sasa hivi

Kupitia instagram account yake, Khaled ameweka wazi kuwa hivi sasa anahitaji kupumzika kwa takriban siku mbili , ili aweze kuilinda afya yake ukizingatia amekuwa akifanya kazi sana bila kupumzika.

Dj Khaled pia ameongeza kuwa, hata Malkia wake (Mama Asahd) ambaye ni mchumba wake, amekuwa akimzuia kupokea simu kwa hivi sasa kwa sababu anahitaji kupumzika ili pia ajijenge kiafya na hata kuwa karibu na familia yake

Tunamnukuu
"Ninahitaji kupumzika. Nimakuwa nikjishughulisha kwa nguvu sana na ninadhani nahitaji siku moja au mbili kupumzika hii , na sababu ambayo inanifanya nipost hili jambo  ni kwamba simu yangu haitoacha kuita kwa sababu malkia wangu ataishia kunizuia nisiongee n mtu kwa sababu nahitaji siku mbili za kupumzika. Sasa, kama mtaona hili jambo, basi niacheni nipumzike, hakuna chochote zaidi ya upendo. Ninahitaji siku mbili kisha nitarejea"


MNADA BANNER