REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WYRE NA JOSEE CHAMELEONE, USO KWA USO NA JAY Z, KANYE WEST NA WENGINEO..

12:51:00 AM Add Comment


Na Oxs Okelleky "Big Dady"
TUNAWEZA Kusema Shukrani sana kwake WYRE THE LOVE CHILD Kutoka Nchini Keny na Josee Chameleone kutoka Uganda, kwa Kuzidi kuipeleka Pazuri Afrika mashariki, Kupitia Sanaa ya Muziki wao.

MIKITO Mikali ya WYRE na CHAMELEONE  imeweza Kuwafikisha katika Tuzo za THE WORLD MUSIC AWARDS kwa Mwaka Huu.

Wyre ambaye hivi sasa anafanya Vizuri na Track yake ya NO MORE pamoja na Chameleone, ameingia katika Kipengere Kigumu sana cha WORLD’S BEST MALE ARTIST, ambako watakutana na Vichwa Nguli na 
balaa katika Muziki ulimwenguni kote.

Wawili hao ambao hawakamatiki katika Muziki wa Dance hall Nchini Kenya, Uganda,  na Afrika Mashariki Kiujumla,w atakutana na Vichwa kama Vile JAY Z, KANYEWEST, P.DIDY, JOHN LEGEND, CHRIS BROWN, JUSTIN BIEBER, RICK ROS, 2 CHAINZ, PITBULL, LIL WAYNE, KENDRICK 

LAMAR, FUSE ODG, FALLY IPUPA na wengineo Kibwena.
Aidha katika CATEGORY hiyo hiyo, Wasnii wengine Kutoka Barani Afrika ni Pamoja na DAVIDO, ICE PRINCE, D BANJ, WIZ KID, TIMAYA, OLAMIDE, FALLY IPUPA,2 FACE IDIBIA, FUSE ODG na Wengineo.


THE WORLD MUSIC AWARDS, ni Tuzo ambazo hutambua kazi na Ubora wa Wasanii Mbali mbali  Duniani

TYGA NA CHRIS BROWN WANAREJEA TENA…..

12:47:00 AM Add Comment

NA EDNA ELISHA "NATTY E"
MOJA kati ya Historia ambayo haitakuja kujitokeza, Ni Baada ya Chris Brown kuungana na Tyga, hatimaye Kutengenza ALBAM ambayo ilikuwa ni “HATOKI MTU HAPA”

Kwa Mujibu wa TYGA katika moja ya Interview Nchini marekani, TTM tumemnyaka akisema kuwa Historia Hiyo inatarajiwa Kuvunjwa baada ya wawili hao kujipanga kwa Ajili ya ALBAM Mpya wakiwa Pamoja.
Mnamo Mwaka 2010, wawili hao walishusha Mixtape ya FAN OF A FAN ambayo ilifanya Vizuri, na Mwaka Huu pia wanakuja na Brand New Albam ambayo itaitwa FAN OF A FAN 2


Katika maelezo yake TYGA ambaye ni Memba wa YMCMB, amesema kuwa wawili hao watajiunga Tena na Kufanya Project ambayo itawaweka karibu sana, huku wakiwapatia Mashabiki wao Kitu ambacho wanakihitaji.


TYGA na Chris Brown waliweza Kuteka masikio ya Mafanz Wao kupitia Mikwaju  Very hot kama Vile DEUCES na HOLLA AT ME 

MB DOG AMEWAHI KUVUTA MILIONI 10 KATIKA SHOW

12:42:00 AM Add Comment

MKALI wa Muziki wa KIzazi kipya Kipindi Hicho, MBWANA MOHAMED Maarufu kama MB DOG, amefichua hili ambalo tulikuwa hatulifahamu Kutoka kwake.

Swahiba Huyo ambaye alifanya vema sana Kupitia Mikwaju kadhaa kama vile LATIFA, INAMAANA, na Nyinginezo Kibao, amedai kuwa aliwahi kulipwa Kiasi cha Shilingi MILIONI 10 alipokuwa akipiga Show Moja katika Nchi ya Burundi

Tofauti na kulipwa Mkwanja Huo, MB DOG aliongeza kuwa, amewahi kulipwa Shows za Milioni Kadhaa, ingawa Wengi walikuwa hawafahamu kwasababu kipindi hicho hakukuwa na tabia ya Kutaja Viwango vya Fedha ambavyo Vinalipwa kutokana na Show, tofauti na Ilivyo hivi sasa, Kila Kitu kiko wazi.

Pia MB DOG ambaye ni Ex Memba wa Kundi la TIP TOP CONNECTION, ameongeza kuwa Show yake ya Kwanza alilipwa Kiasi cha Shilingi Milioni 3, huku Show ya Mwisho Ikiwa ni Milioni 10 za Kitanzania mnamo Mwaka 2006, ambayo ilikuwa ni maajabu kwake.


Lakini Mpaka Hivi sasa, Swali ambalo MB DOG anajiuliza, je Ni kweli anaweza Kupiga Show Yenye Mzuka na Watu Wengi huku akiingiza Mkwanja Mkali kama Kipindicho?

MNADA BANNER