REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MAJANGA: MWANAFUNZI ALIYEHITIMU KIDATO CHA NNE AKAMATWA KWA TUHUMA ZA WIZI WA NJIA YA ATM

2:13:00 AM Add Comment


POLISI wilayani Rungwe, mkoani Mbeya, limewanasa watu wanne akiwamo mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana, wilayani Bunda, mkoani Mara, baada ya kukutwa wakiiba fedha Benki ya NMB tawi la Tukuyu kupitia mashine za kutolea fedha (ATM).

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chrispin Meela alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 2:30 usiku.
Meela aliwataja watuhumiwa  hao kuwa ni mkazi wa mjini Tukuyu,  Mfanyabishara wa Mbozi, mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana wilayani Bunda na mkazi wa Msasani Tukuyu.

Alisema akiwa nyumbani kwake usiku, alipigiwa simu na msamaria mwema na kuambiwa taarifa za kuwapo watu  wakiwa kwenye mashine hizo za kutolea fedha, huku wakiwa wanatoa fedha mfululizo na aliwatilia shaka.

“Jana  usiku saa 2:30 nilipigiwa simu na msamaria mwema na kuniambia kuwa,  kuna watu wapo Benki ya NMB wanatoa fedha ATM tena mfululilo huko wakiwa na kadi nyingi za ATM,” alisema Meela na kuongeza:“Baada ya kuambiwa hivyo nilimpigia simu OCD (Mkuu wa polisi wilaya), akatuma timu ya makachero eneo ta tukio na wakabahatika kuwakuta na kuwatia nguvuni.”

Meela alisema watuhumiwa  walikutwa wakiwa na kadi bandia za ATM 150 za watu tofautitofauti  na kwamba, hadi wanatiwa mbaroni tayari walikuwa na Sh20.5 milioni mkononi. Alisema kadi zote ni za NMB na kwamba, zilikuwa zinaonyesha  wateja wote ni walimu kutoka wilayani Mbozi.

Alisema baada ya watuhumiwa kuhojiwa  walidai ni wafanyabiashara wanajihusisha na kukopesha fedha walimu, hivyo  katika kuzirejea fedha hizo walimu waliwapatia kadi zao ili waende kutoa  benki.

“Kinachotupa hofu  hapa ni kwamba, kadi zote hizi zinaonyesha wateja kutoka wilayani Mbozi, sasa swali kwa nini waje kutolea fedha hizo wilayani kwetu?” alihoji Meela.

Alisema watuhumiwa wote wapo Kituo cha Polisi Tukuyu kwa mahojiano zaidi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani alikiri kupata taarifa hizo, lakini alikataa  kulitolea ufafanuzi kwa sababu  wanaendelea na uchunguzi.

KASHFA: MSANII BONGO, ATELEKEZA MTOTO WAKE UBUNGO

1:59:00 AM Add Comment


MPEKUZI

MREMBO aliyewahi kupamba video kadhaa za wasanii wa Bongo Fleva ukiwemo wimbo wa Kidato Kimoja ulioimbwa na J.I, anayekwenda kwa jina la Maya Silemwe, amedaiwa kumtelekeza mwanaye wa kumzaa aitwaye Junior Justine (3).

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo mtoto huyo aliokolewa na msamaria mwema.


Akisimulia mkasa mzima ulivyokuwa, shangazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Monalisa, alisema wao kama familia wameumizwa sana na kitendo kilichofanywa na Maya.

“Maya amezaa na kaka yangu Justine anayeishi Marekani na amekuwa akimjali sana kwa kumtumia fedha za matumizi mara kwa mara. Kisa ni kwamba kaka alimwambia Maya ampeleke mtoto Bukoba (nyumbani kwa baba wa mtoto) akasalimie, Maya akakubali lakini akamwambia atapitia kwanza Arusha (nyumbani kwao) ndipo waende Bukoba.

“Justine akamuelewa lakini kumbe alidanganya, hakwenda Arusha na kuna watu walimuona akiingia kwenye klabu moja hapahapa Dar es Salaam, wakamjulisha kaka. Sasa alipompigia kumuuliza, akawa anajing’atang’ata, siku iliyofuata akadamkia Ubungo ili kumsafirisha mtoto kwenda Bukoba kwa mama yetu (bibi wa mtoto) lakini alitaka kumsafirisha kwa kumtumia kondakta,” alisema Monalisa na kuongeza:

“Alikubaliana na kondakta huyo kisha akamwachia namba ya simu ya mama na yake ili waweze kuwasiliana na kumpokea mtoto huko Bukoba.

Kwa bahati mbaya siku ile yule konda alikuwa hasafiri mpaka siku inayofuatia. Mtoto akaanza kuhangaika stendi siku nzima bila uangalizi mzuri.

“Bahati nzuri mama mmoja msamaria mwema akafuatilia na kuonana na huyo konda, akamuomba namba za mama wa Bukoba kisha akawasiliana naye, kwa kuwa alikuwa na safari ya kwenda huko siku iliyofuata, akaamua kuchukua jukumu la kusafiri naye.”

Monalisa alikubali kutoa namba za simu za msamaria aliyejitolea kusafiri na mtoto huyo, alipopigiwa alikiri lakini aliomba sana asitajwe .

“Mimi kama mzazi iliniuma sana kumuona mtoto mdogo anahangaika stendi bila uangalizi. Nilishangaa sana kuona mzazi aliyeingia ‘leba’ anawezaje kumwacha mwanaye mdogo namna ile asafiri mwenyewe?” alisema.


Naye baba mzazi wa mtoto huyo, Justine aishiye Marekani ambapo alisema kuwa: 
“Jambo hilo limeniumiza sana. Kwa kweli kama ningekuwa huko nyumbani (Bongo) ningehakikisha namfundisha adabu huyo mwanamke kupitia sheria.

“Nashukuru kusikia kwamba mwanangu alifikishwa salama Bukoba.”

Mama wa mtoto huyo alipopigiwa simu alizua kioja baada ya kukataa kwamba hajawahi kumuacha mtoto kwa konda Ubungo na pia akadai eti hana mtoto na wala hajawahi kuzaa katika maisha yake yote.

Wakati tukijiandaa kwenda mitamboni juzi Jumatatu, habari zilizopenyeza katika chumba chetu cha habari zilisema kwamba mrembo huyo alimpigia simu mama mkwe wake na kumchimba mkwara mzito.

FULL SECURITY: JACKLINE PATRICK AONESHA BASTOLA YAKE INSTAGRAM

1:49:00 AM Add Comment

OH MY GOOOOOOOOD...akiwa bado katika Msala wa Kumchapa na Chupa Mrembo mwenzake, Kama hakijatokea kitu vile, Jackline wa Patrick amesanua Mguu wake wa Kuku...namaanisha Bastola kupitia Mtandao wa INSTAGRAM, kama uonavyo hapo, Huku akipost Kauli hii

"This is For Security Purpose, nat harmful to anyone. Loool"

SWALI:, Kama umemtandika yule dada na BOTTLE, je hii ukiwa nayo karibu si utamfyatulia Mtu akikuudhi?

ONYO: WALIMU WAPEWA KALI

1:26:00 AM Add Comment


MKUU wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele, ametoa onyo kwa baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari wanaotumia vibaya madaraka na kuwachangisha michango mipya wananchi bila maelezo ya msingi.

Henjewele ametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilayani hapa juzi.

Alisema kuanzia sasa atawaagiza wakaguzi wa ndani kukagua hesabu zote katika shule za sekondari wilayani hapa.

Alisema katika siku za hivi karibuni wazazi wamekuwa wakielezwa kuchangia fedha nyingi kila mwanzo wa muhula wa kwanza wakati hakuna hesabu maalumu katika shule hizo zinazoonyesha matumizi ya michango ya mwisho wa kila mwaka.

“Baadhi ya wazazi wamelalamika juu ya utitiri wa michango hususan katika shule za serikali za kata kila wanapoanza muhula wa kwanza kila mwaka kiasi cha baadhi yao kushindwa kuwapeleka watoto wao kuanza kidato cha kwanza kwa wakati.

“Kuanzia sasa nimewaagiza wakaguzi wa hesabu wa ndani wa halmashauri kufanya ukaguzi katika shule zote za sekondari…na iwapo itathibitika kuwa ubadhirifu umetokea na kusababisha upotevu wa fedha hatua stahiki zitachukuliwa,” alisema Henjewele.

Alisema michango hiyo imegeuka neema kwa baadhi ya wakuu wa shule hizo ambapo sasa baadhi wamekuwa wafanyabiashara huku wakiacha watoto bila kufundishwa sawasawa na kusababisha kupatikana matokeo yasiyoridhisha wakati wa mtihani wa kidato cha nne.

FEDHEHA : MOSHI WAMKERA MHE. CHARLES TIZEBA

1:15:00 AM Add Comment

Na Rodrick Mushi, Moshi


NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Charles Tizeba, amesema amefedheheshwa na kitendo cha uongozi wa manispaa ya Moshi kutaka kuua uwanja wa ndege wa Moshi kwa kugawa ardhi ya uwanja kwa baadhi ya watu.

Mbali na hilo alisema pia kuna mkanganyiko wa mchoro wa uwanja huo wa awali baada ya kubadilishwa.

Tizeba alisema hayo mjini hapa jana baada ya kufanya ziara yake kwenye uwanja huo akiwa ameambatana na Mbunge wa Jimbo la Moshi, Philemon Ndesamburo.

Katika ziara hiyo walizunguka maeneo mbalimbali ya uwanja huo na kujionea ujenzi uliofanyika ndani ya uwanja huo.

Akizungumza kwenye kikao kilichofanyika ndani ya uwanja huo, Tizeba alisema kufa kwa uwanja huo kunachangiwa na watu wa Moshi wakiwemo baadhi ya viongozi wa manispaa.

Kutokana na hali hiyo alimtaka kufika Ofisa Mipango Miji, Alex Poteka, ambaye alifika muda mfupi huku majibu yake yakionyesha kutomridhisha naibu waziri huyo.

Awali akitoa malalamiko kwa Waziri Tizeba, meneja wa uwanja huo wa ndege, Francis Massao, alilalamika kuomba michoro ya awali ya uwanja huo toka kwa uongozi wa manispaa akiwamo ofisa mipango miji, Poteka, kwa kuandika barua bila mafanikio.

“Hivi ni wapi au ni uwanja gani wa ndege unaoweza kuongoza ndege huku kukiwa kuna nyumba imejengwa katikati ya uwanja!?” alisema Massao.

Tizeba alisema kuwa uwanja wa Moshi ni uwanja mkongwe kuliko yote ila umechoka kutokana na kutofanyiwa ukarabati muda mrefu.

Kwa upande wake, Poteka alijitetea kuwa hana taarifa kamili juu ya watu waliojenga kwenye eneo hilo la uwanja.

WIZI KWA NJIA YA ATM WAZIDI KURINDIMA

1:02:00 AM Add Comment


NA Christopher Nyenyembe

WIMBI la wizi wa fedha kwenye mitandao ya benki kupitia njia ya mashine za kuchukulia fedha (ATM), umewatia hasara wateja wengi wa benki ambao zaidi ya sh milioni 20 zinadaiwa kuchotwa kwa nyakati tofauti na watu wanne wanaomiliki kadi zipatazo 150.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumatano umegundua kuwepo kwa mtandao wa wizi kwa njia ya ATM unaotumiwa na watu wanaojifanya kuwa ni madalali wa fedha wanaowalaghai watumishi wa serikali.

Madalali hao wanadaiwa kuwakopesha watumishi hao wa serikali kwa sharti kwamba wawapatie kadi zao za kuchukulia fedha benki kama dhamana.

Uchunguzi umebaini kuwa, mtindo huo umeenea katika maeneo kadhaa mkoani Mbeya na hasa ukiwalenga watumishi wa serikali ambao kutokana na hali ngumu ya kifedha, wamejikuta wakiingia kwenye mtego huo na kuamua kutoa kadi zao za ATM ili waweze kupata mikopo.

Habari ambazo gazeti hili imezipata kutoka kwa waathiriwa wa wizi huo wa mtandao, unasema kuwa wapo madalali ambao wanawafuata watumishi wa serikali kwa lengo la kuwakopesha fedha kwa masharti kwamba watoe kadi zao za ATM na namba za siri kama dhamana.

“Mtandao wa kuchukua fedha kutoka kwa watumishi wa umma umeenea sana, haukuanza leo, wapo watu wanakopesha fedha kwa sharti la kutoa kadi ya ATM na namba yako ya siri ili mshahara wako unapoingia, wao wanakwenda kuchukua fedha zao walizokopesha na riba,” alisema mtumishi mmoja wa serikali jijini Mbeya.

Wakati hali ikiwa hivyo, habari kutoka Wilaya ya Rungwe zinadai kuwa kiasi kikubwa cha fedha kimechukuliwa benki na watu wanaomiliki kadi za ATM zaidi ya 120, na kwamba tayari Jeshi la Polisi linawashikilia watu hao ambao wamekutwa na idadi hiyo ya kadi zisizokuwa zao.

Habari zaidi zinasema kuwa, mtandao wa madalali hao wa fedha umekuwa mkubwa, na kwamba watu hawaibiwi kwani wametoa kadi zao wenyewe baada ya kukubali kukopeshwa.

“Ndugu mwandishi tumefikia uamuzi huu kutokana na hali ngumu ya maisha, watoto wanatakiwa walipiwe ada, tunahitaji mbolea kwa ajili ya kilimo na gharama za maisha zipo juu, tutafanyaje? Ndiyo maana tumejikuta tukitoa kadi zetu za ATM ili tutatue matatizo yetu, kama wapo matapeli hilo sijui, ila wengi tumeingia kwenye mtego huo,” alisema mama mmoja aliyejitaja kuwa ni muuguzi.

Meneja mmoja wa benki ambaye hakutaka jina lake liandikwe wala benki anayofanyia kazi, alisema wizi kwa njia ya ATM ni tatizo sugu kwa wateja wao, kwani wamekuwa wakipokea malalamiko kila siku kuwa fedha zao zinaibwa bila wao kujua.

Alisema hana taarifa kama kuna wateja wanaotoa namba zao za siri na kadi zao kwa madalali wa fedha.

“Kinachonishangaza benki yetu inakopesha, sasa huu mtindo uliozuka kati ya wateja na madalali wa nje unatia shaka usalama wa fedha kwenye benki zetu, inabidi hatua kali zichukuliwe kwa wateja wanaoruhusu watu wengine wawachukulie fedha, hilo ni kosa la jinai kufanywa na wateja wasiokuwa waaminifu,” alisema meneja huyo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman alipohojiwa alisema kuwa amepokea taarifa za kuwepo kwa tukio hilo, hasa Wilaya ya Rungwe na kwamba tayari anasubiri taarifa kamili kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Mbeya (RCO) ili atoe taarifa kamili leo.

NANI KAMA MAMA?.. YOUNG AND BEAUTIFUL

12:40:00 AM Add Comment
KAMA huna kawaida ya kumpenda Mama Yako Mzazi, basi hakika una baraka Chache sana Maishani mwako. 

Binafsi Tunampenda sana Mama Yetu Mzazi, MAGRETH KAGARUKI (Kushoto) ambaye amekuwa chachu kubwa sana ya Maendeleo katika Familia Yetu. Upendo wake wa Dhati kwa Baba Yetu Mzazi MAGNUS JOACHIM na Sisi watoto wao, umekuwa ni Sukari ya Furaha, Mapendo na hata Amani ndani ya Familia Yetu.

Tunakupenda sana Mama Yetu, na Hata Baba Pia. Ila amini usiamini, nimekumiss sana, maana ni Miaka Mitatu sasa Sijaonana na Wewe, ila nakuahidi Mwezi March mwaka huu, lazima nije kuitembelea Familia Yangu.

WE LOVE YOU ALOT, AND WE ARE VERY PROUD OF YOU MAMA and DADY TOO

HANKER CHIEF YANGU: BINAFSI NIMEMUELEWA TIMBULO

12:30:00 AM Add Comment

HANKER CHIEF YANGU LEO inamfguta Jasho Timbulo kutokana na Msala ambao ulikuwa unamkabili, kuhusu MADAWA YA KULEVYA;

Timbulo amesema ni kweli alihisiwa kuwa amebeba madawa ya kulevya kitu kilichowafanya wanausalama kuomba kumkagua na kweli kumkuta na Pipi ambazo mara nyingi zimekua ni mfumo wa kubebea madawa ya kulevya katika begi lake, lakini katika maelezo ya timbulo anasema hazikuwa dawa za kulevya kweli bali ni mfano wa dawa ambazo alifanyia shooting katika movie yake ya hivi karibuni na kusahau kuzitoa.

BALAA: BOBBY BROWN ATUPWA JELA

12:14:00 AM Add Comment


WAKATI Binti ake akiwa katika Skendo la Kufuata Tabia za Mama Yake Marehemu Whitney Huston kwa kuchoma Shisha, Boby Brown ambaye ni Mume wa Marehemu Whitey ametupwa Jela kwa Siku 55.

Kwa Mujibu wa WADAKU wa Mbele, Mkali huyo wa RnB amekutana na Nyundo hiyo baada ya kukamatwa na Askari akiendesha Gari kwa Kasi huku harufu ya Pombe ikiwa imetawala ndani ya Gari L:ake.

PICHA : NAUANGALIA

12:07:00 AM Add Comment
 MAHALI PA KUKAA: RaisJakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi  mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali(picha na Freddy Maro)



UNAONEKANA VIZURI AISEE: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi  mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam.Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi.Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali(picha na Freddy Maro)

MNADA BANNER