REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

BAADA YA KUJARIBU KETE YAKE KATIKA TUZO ZA KTMA 2014, HIKI NDICHO ALICHOKIANDIKA MSANII MIKE

10:01:00 AM Add Comment

Okay, nimefurahi kuona wale wasanii wapya waliokaza mwaka huu wametajwa kwenye nominations za Kilimanjaro Premium Lager

Mimi sina muda ofcoz ila nafurahi kwamba nimeanza vizuri na kutotajwa mwaka huu sio mbaya maana bado nahitaji kuskika zaidi kuthibitisha uwezo nilio nao.

Mwaka huu nimejiwekea kuwa nitajiweka pazuri kwenye soko la muziki, nifahamike kwa kazi nzuri zaidi.

Naamini kwa malengo niliyojiwekea mwaka huu kwenye mziki, mwaka ujao huenda nikakumbukwa kwenye orodha ya wateule wa KTMA hata kwa kutajwa tu.

Hongera sana NAVY KENZO, Makomandoo, Youngkiller Msodoki, Richard mavoco, Vanessa Mdee, Meninah na Walter Chilambo, pamoja na Maua Sama.

Niliona wote wakati mnaanza na nimeona bidii yenu na sasa mpo kwenye orodha. Mwaka ujao nitakua miongoni mwenu bila shaka naamini hivyo. Hongereni sana...

Pia naamini kwamba rafiki zangu mlinipigiakura nyingi tu kupendekeza niwepo, wala msivunjike moyo. Nyote mnafahamu tumejaribu kuwa wamoja kuweka kazi yangu kwenye nafasi nzuri.

Mungu akijaalia mwezi April single yangu mpya itatoka rasmi. Bado nasisitiza kuwa msiniache nikaanguka maana ninyi ni nguzo yangu, nitazameni vizuri na kunifauatilia katika kazi zangu za muziki ili siku nikifaulu muwe mashahidi kwamba nilikuwa nyota njema toka awali.

Asante sana kwa Ben Pol, Joh makini, Damian soul, G Nako pamoja na Dir Nisher Bybee kwa kunipa moyo na ushauri pia. I promis you next year i'll make it.

Written by Mike..

BEST IN MWANZA: USIMALIZE WIKI YAKO..CLARA SALOON-MWANZA, WANAKUPA TIBA YA UREMBO

9:43:00 AM Add Comment
MAJEMBE KAZINI: (KUTOKA KUSHOTO) ROBERT TAWILE, MASOUDI "MING'ARISHO NA RAMA DEE

HATA MAHARUSI PIA: MOJA KATI YA MAHARUSI WALIOHUDHURI NA KUFURAHIA HUDUMA YA CLARA SALON, AKISHUKA KUTOKA SALON KWA MBWEMBWE ZOTE

LETE MIGUU YAKO NA MIKONO YAKO: OFISI YA MASOUD "MING'ARISHO", KWA AJILI YA KUSHA, MIKONO PIA

NAKULA KICHWA : RAMA DEE AKIWA KAZINI KAMA KAWAIDA

NIPO KAZINI: MASOUDY "MING'ARISHO AKISHUGHULIKA NA UREMBO WA MIGUUNI


BAADA YA KUNYOLEWA, NA HATA KUFANYIWA UREMBO WA KICHWA, KICHWA KINASAFISHWA NAMNA HII

ROBERT TAWILE AKIWA MZIGONI KAMA KAWAIDA

SCRUB TIME: MWANADADA LINAH AKIPIGA SCRUB USO WA MTEJA




AKINA DADA WA UPANDE WA SALON YA KIKE WAKILA MZIGO KAMA KAWAIDA


HII NDIYO ORODHA YA WASHIRIKI WA TUZO ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS (KTMA)- 2014

9:18:00 AM Add Comment

Orodha Kamili ya waliongia katika kinyang'anyiro cha Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014:

Wimbo bora wa mwaka 
1 Number one-Diamond
2 Joto hasira-Lady Jaydee Ft Prof Jay
3 I love u-Cassim Mganga
4 Yahaya-Lady JayDee
5 Kidela -Abdu Kiba Feat Ali Kiba
6 Muziki gani-Ney ft Diamond

Wimbo bora wenye vionjo vya asili ya Kitanzania
1 Kwejaga nyangisha-Batarokota
2 Nalonji-Kumpeneka
3 Bora Mchawi-Dar Bongo massive
4 Tumbo lamsokota-Ashimba
5 Aliponji -Wanakijiji
6 Agwemwana-Cocodo African music band

Wimbo bora wa kiswahili -Bendi
1 Ushamba mzigo-Mashujaa Band
2 Shamba la Bibi -Victoria Sound
3 Chuki ya nini -FM Academia
4 Yarabi nafsi -Mapacha Watatu
5 Kiapo mara 3 -Talent Band

Wimbo bora wa Reggae 
1 Niwe na wewe-Dabo
2 Hakuna Matata-Lonka
3 Tell Me-Dj Aron ft Fidempha
4 Bado nahitaji-Chikaka ft Bless p & Lazzy B
5 Bongo Reggae-Warriors from the east

Wimbo bora wa Afrika Mashashariki
1 Tubonge-Jose Chamelleone
2 Nakupenda Pia-Waire Ft Allain
3 Badilisha-Jose Chamelleone
4 Kipepeo-Jaguar
5 Kiboko Changu-Aman FT Weizal and Radio

Wimbo bora wa Afro pop 

1 Number one-Diamond
2 Joto hasira-Jay Dee
3 Kidela-abdul kiba ft Ali Kiba
4 I love you-Kassimu
5 Tupogo-Ommy Dimpoz Ft J Martins
6 Roho yangu-Rich Mavoko

Wimbo bora wa Taarab 
1 Wasi wasi wako-Mzee Yusuf
2 Asiyekujua Hakuthamini-Isha Ramadhani & Saida Ramadhani
3 Nipe stara -Rahma Machupa
4 Sitaki shari-Leyla Rashid
5 Fahari ya Mwanamke-Khadija Kopa
6 Mambo bado-Khadija Yusuf
7 Kila muomba Mungu -Mwanahawa Ali

Wimbo bora wa Hip hop 
1 Bei ya mkaa-Weusi
2 Nje ya box-Nick wa pili ft Joh Makini and , Gnako
3 Siri ya mchezo-Fid q ft Nature
4 2030-Roma
5 Pesa-Mr Blue Ft Becka Title

Wimbo bora wa R&B 
1 Listen-Belle 9
2 Closer -Vanessa Mdee
3 So crazy-Maua ft Fa
4 kama huwezi-rama dee ft jay dee
5 Wa ubani-Ben Pol ft. Alice

Wimbo bora wa kushirikisha/kushirikiana
1 Music Gani-Ney Mitego ft Diamond
2 Joto Hasira-Lady JayDee ft. Prof Jay
3 Kidela -Abdul Kiba ft. Ali Kiba
4 Bila Kukunja Goti-Mwana FA na AY ft. Jay Martins
5 Tupogo-Ommy Dimpoz ft. Jay Martins

Wimbo bora wa Ragga/Dancehall 
1 Nishai-Chibwa Ft Juru
2 Sex girl-Dr Jahson
3 My sweet-Jettyman Dizano
4 Feel Alright-Lucky Stone
5 Wine-Princess Delyla

Wimbo bora wa Zouk /Rhumba
1 Yahaya-Lady Jaydee
2 Yamoto-Mkubwa na wanawe
3 Msaliti-Christian Bella
4 Nakuhitaji-Malaika Band
5 Narudi kazini-Beka

Mwimbaji bora wa kike -kizazi kipya
1 Vanessa Mdee
2 Lady Jaydee
3 Linah
4 Maua

Mwimbaji bora wa kiume -kizazi kipya
1 Ben Pol
2 Rich Mavoko
3 Diamond
4 Ommy Dimpoz
5 Cassim Mganga

Mwimbaji bora wa kike -Taarab
1 Khadija Kopa
2 Isha Ramadhani
3 Khadija Yusuf
4 Mwanahawa Ali
5 Leyla Rashid

Mwimbaji bora wa kiume -Taarab
1 Mzee Yusuf
2 Hashimu Saidi
3 Mohamedi Ali aka Mtoto Pori

Mwimbaji bora wa kiume -Bendi
1 Jose Mara
2 Kalala Junior
3 Charz Baba
4 Khalid Chokoraa
5 Christian Bella

Mwimbaji bora wa kike -Bendi 
1 Luiza Mbutu
2 Catherine (Cindy)
3 Ciana

Msanii bora wa -Hip hop 
1 FID Q
2 Stamina
3 Young killer (Msodoki)
4 Nick wa pili
5 Gnako

Msanii bora chipukizi anayeibukia
1 Young Killer(Msodoki)
2 Walter Chilambo
3 Y Tony
4 Snura
5 Meninah

Rapa bora wa mwaka -Bendi
1 Kitokololo
2 Chokoraa
3 Furguson
4 Canal Top
5 Totoo ze Bingwa

Mtumbuizaji bora wa kike wa Muziki 
1 Khadija Kopa
2 Vanessa Mdee
3 Isha Ramadanni
4 Luiza Mbutu
5 Catherine (Cindy)

Mtumbuizaji bora wa kiume wa Muziki
1 Diamond
2 Christian Bella
3 Rich Mavoko
4 Ommy Dimpoz
5 Abdu Kiba

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka -Taarab
1 Enrico
2 Ababuu Mwana ZNZ
3 Bakunde

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka -Kizazi kipya
1 Marco chali-Mj Records
2 Man Water-Combination Sound
3 Mazoo-Mazoo Records
4 Sheddy Clever-Burnz Records
5 Nahreel -Home Town Record

Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka -Bendi
1 Allan Mapigo
2 C9
3 Enrico
4 Amoroso
5 Ababuu Mwana ZNZ

Mtunzi bora wa mwaka -Taarabu
1 Mzee Yusuf
2 El-Ahad Omary
3 El-khatib Rajab
4 Kapten Temba
5 Sadiki Abdul
6 Nassoro Seif


Mtunzi bora wa mwaka -kizazi kipya
1 Belle 9
2 Ben Pol
3 Diamond
4 Rama dee
5 Rich mavoko

Mtunzi bora wa mwaka -Bendi
1 Christia Bella
2 Jose Mara
3 Chaz Baba
4 Nyoshi Saadat
5 Kalala Junior

Mtunzi bora wa mwaka -Hip hop
1 Nikki wa Pili
2 Young Killer(Msodoki)
3 Roma
4 FID Q
5 G- Nako

Video bora ya muziki ya mwaka
1 Number one-Diamond
2 Yahaya-lady Jaydee
3 Joto hasira-Lady Jaydee Ft Prof Jay
4 Uswazi takeaway-Chege Ft Malaika
5 Mama Yeyo-Gnako Ft Ben Pol

Bendi ya mwaka 
1 FM Academia
2 Mapacha Watatu
3 African Stars(Twanga Pepeta)
4 Akudo Impact
5 Malaika Band
6 Mashujaa Band

Kikundi cha mwaka cha Taarab
1 Jahaz Modern Taarab
2 Mashauzi Classic
3 Five Stars

Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya
1 Makomandoo
2 Navy kenzo
3 Weusi

4 Mkubwa na wanawe

JAMAA TU FLANI AWAVUSHA MIPAKA NATTY E, HONEYA NA DEEY CLASSIC, KUTOKA MWANZA, KENYA MPAKA CANADA

9:09:00 AM Add Comment

WIKI Iliyopita TTM kupitia BLACK TOUCHEZ tulikushushia Kwaju jipya la The Hot Female Hip Ho Emcee, NATTY E Ambayo inafahamika kwa Jina la HAINAGA NOMA, na Hivi Leo imetambulishwa rasmi kupitia Kipindi Cha Jam Session cha 99.4 MHz, ikiwa ni baada ya Kufanyiwa Utambulisho wa Awali kupitia Kituo Cha RADIO FREE AFRICA Mwanza.

Tofauti na Hilo, Honeya ni Moja kati ya wasanii ambao tulipata nafasi ya kuzungumzia Uwezo wao mzuri wa kuimba, huku tukikukabidhi Track yakle ya UWE WANGU.
Producer Deey Classic

In That Case, Kipaji cha wawili hawa wawili NATTY E & HONEYA, finaly kimeweza kuvuka mipaka na kutua nchini KENYA, ambapo The Hip Hop Artist Nchini humo, anayefahamika Kwa Jina la JAMAA TU FULANI ameweza kuwakutanisha katika Track Moja.

JAMAA TU FLANI ambaye hivi sasa anaishi CANADA, amewapa SHAVU Honeya katika Chourus, Huku Natty e akikamua Verse ya Kwanza katika Ngoma hiyo inayofahamika kwa jina la FREEDOM..
Mzigo infact Umesimamiwa na Mbabe Mwenyewe, DEEY CLASSIC kutoka Revolution Sound Jijini Mwanza, ambaye amefanya kile ambacho ukubali ukatae, anastahili Credit Yake.

SIKILIZA KIDUUUCH:..

HATIMAYE ALIYEKUWA MUME WA NAZIZI AZUNGUMZIA KUHUSU TALAKA YAO

1:48:00 AM Add Comment

KAMA Utakuwa ni SUPPA FAN wa TTM, basi utakuwa unakumbuka Vizuri kabisa kuwa tulikupa mtonyo kuhusiana na Ishu ya Naziz kuomba Talaka kutoka kwa Mumewe.

Baada ya NAZIZI kuzungumza Mengi kuhusu Mchakato huo, huku akithibitisha kuwa hivi sasa amebaki Singo na hakuna Tena Ndoa baina ya wawili hao.

Kwa upande wake VINI LEOPOLD ambaye ndiye alikuwa Mume wa nazizi, na wakafanikiwa kupata Mtoto mmoja wa kiume, amesema kuwa kitendo cha kupeana talaka na Msanii huyo ambaye anaunda kundi la NECESSARY NOISE na EAST AFRICAN BASHMENT CREW, hakijawafanya wao kuwa Maadui, na bado wanawasiliana na Kuzungumza Vizuri.

Akizidi kufafanua kuhusu Hilo, Vini ameongeza kuwa, Yeye na Nazizi ingawa kila mtu ana maisha yake hivi sasa, lakini bado ni marafiki wazuri, sababu ukizingatia hata talaka waliyopeana, ilikuwa ni makubaliano yao wawili na hakukuwa na Ugomvi

Aidha Vini ambaye alifunga Ndoa ya Siri na Nazizi Mnamo Mwaka 2008, amesisitiza kuwa, Vyombo vya habari viache Kuandika habari zisizo na ukweli kuhusu kuvunjika kwa Ndoa yao, kwani wana motto wao Mmoja, na hatakiwi kukutana na Info hizo.


Katika Kumalizia, VINNY amewashauri mashabiki na watu Mbali mbali, Kuupa Support Muziki wa Nazizi, huku wakiacha maisha yao Binafsi yaende Sawa.

LIL WAYNE AWA MKWELI KWA NICKI MINAJI

1:27:00 AM Add Comment

Thanx kwa YMCMB kwa kushusha rasmi Albam yao ya RISE OF AN EMPIRE, ingawa Baadhi ya Mikwaju haijapokelewa na mashabiki wa FAMILIA hiyo baada ya kuisubiri kwa Muda Mrefu.

Lakini jambo ambalo wengi hawakulitarajia kutoka kwa the Big boss wa YMCMB, LIL WAYNE, ni kuizungumzia Tofauti Track ya Nicki Minaji, inayofahamika kwa jina la LOOKING BACK NECCAH, ambayo kwa asilimia kubwa wengi wameikubali, na baadhi wameipinga huku ikishindwa kupata airtime ya kutosha hasa kimataifa.

Akizungumzia Track hiyo katika moja ya Interview kunako kituo cha MTV, Weezy alisema kuwa binafsi , anadhani Nicki Minaj angefanya vizuri zaidi katika Track hiyo, jambo ambalo linaashiria bado hajakubali kiwango ambacho kimetoka kunako kwaju hilo.


Pia Weezy ambaye pia Track yake ya WE ALL RIGHT imehusika kunako ALBAM hiyo ya The Rise Of An Empire, ameongeza kuwa Hivi sasa Nicki anashughulikia Project yake Mpya, huku akimsifia na kuthibitisha kuwa hajawahi kumuangusha katika Kila kazi anayoifanya, hivyo anaamini kila kitu kitakuwa Byee

WIZKID YUKO SINGLE MAZEE..AMETEMANA NA HOT GIRLFRIEND WAKE..

1:06:00 AM Add Comment

THE JUSTIN BIEBER wa Nigeria ambaye anakubalika kwa Namna kubwa, WIZ KID, amethibitisha rasmi kuwa Hivi sasa Yuko Single and Free.

Kauli hiyo ya ya Wiz Kidi imetufikia TTM na kuanza kufuatilia Source ya Yeye kusema Hivyo, na hatimaye tukabaini kuwa WIZ KID amemwagana na aliyekuwa Girlfriend Wake TANIA OMOTAYO.

Kwa Mujibu wa Chanzo ambachi kipo karibu sana na WIZ, kimebainisha kuwa Msanii huyo aliyetisha Na Vibao kama Vile AZONTO na Collabo Kibao, amemwagana na Mpenzi wake, huku akithibitisha Hilo kupitia Moja ya Interview ya radio iliyofanyika huko Nchini Nigeria.


Katika kujibu Swali ambalo aliulizwa na Mtangazaji wa kituo Hicho, WIZ alibainisha Kuwa TANIA (ambaye ni X-Girlfriend) yuko sawa, anaendelea Vizuri ingawa hivi sasa Yuko Single na wanaendelea Vizuri tu katika Mhusiano ya Kirafiki ya kawaida

HEART BREAKING..OR TRUE LOVE?: MCHEKI SWIZZY BEATZ AKIMBUSU MKE WAKE MPYA ALICIA KEYS MBELE YA MASHONDA , MKE WAKE WA ZAMANI, MASHONDA

12:22:00 AM Add Comment


WAY BACK: MCHECKI RAPCELENCY PREZZO..AKIWA NA WAZAZI WAKE ENZI HIZOOOOOOOOO

12:12:00 AM Add Comment

 NYOTA NDOGO AITISHA MAANDAMANO YA KUMKOSOA MUSTAPHA COLONEL KUHUSU PICHA ZAKE NA HUDDAH MONROE….

12:07:00 AM Add Comment

NYOTA NDOGO ameshindwa kuvumilia kile ambacho COLONEL MOUSTAPHA amekifanya kwa kupiga Picha za utupu na aliyekuwa mshiriki wa BBA akiiwakilisha Nchi ya Kenya, HUDDAH MONROE.

Ili kudhihirisha kuwa amechukizwa na hilo suala, Hatimaye Nyota Ndogo aliamua kuitisha Maandamano ya Wanawake ambao wamekwazwa na Kitendo hicho, kushinikiza Jamaa huyo ambaye alikimbiza sana na Track yake ya MTAANI.COM, ajirekebishe na hata Kuachana kabisa na Biashara Hiyo.

Katika Moja ya mabango ambayo yalionekana kubebwa na Wanawake hao, ni pamoja na moja ambalo lilikuwa limeandikwa “COLONEL MUSTAPHA HESHIMU WANAWAKE”

Aidha kwa upande wake Mustpha, alichukua uamuzi sahihi wa Kuomba Msamaha kwa Huddah Monroe pamoja na wanawake ambao wamekerwa na Kitendo hicho. Hapa namnukuu Mustapha akisema..


“Ninawaomba msamaha kwa sababu ni lazima tu-respect wamama.”

MNADA BANNER