REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WIKI HII !! : ABIRIA ASABABISHA NDEGE KUTUA KWA DHARURA , KISA...ANAJAMBA SANA

1:32:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi   
WENGI tunafahamu kuwa kujamba Ni Afya....kwani kuna mtu anapingana na hilo?, maana hata Hospitali, kuna muda Ushuzi wako unahitajika sana ili kujua masuala ya kiafya kwa upande wako

Ndani ya Wiki Hii, kimetokea kituko cha ajabu ambacho kilimfanya kila mmoja aliyekiskia kustaajabu na kujiuliza maswali mengi juu ya tukio hilo.

Abiria mmoja Raia wa Ujerumani ambaye hajafahamika jina mpaka hivi sasa, alisababisha Ndege ya Shirika la TRANSAVIA kutua kwa dharura katikauwanja wa ndege wa VIENNA kutokana na kitendo chake cha kujamba sana akiwa ndani ya ndege

Kwa Mujibu wa taarifa kamili kutoka jeshi la Polisi kutoka Vienna, inasemekana kuwa Binti huyo aliyekuwa na dada yake, alikuwa akijamba ndani ya ndege hiyo inayopiga safari kutoka DUBAI kwenda AMSTERDAM hali iliyosababisha mzozo mkubwa ulioambatana na ugomvi kwa vijana wengine wawili waliokuwa wamekaa pembeni yao wakidai kukereka na tukio hilo

Inasemekana kuwa, Vijana hao walianza kulalamika kuhusu kitendo cha Binti huyo kuachia ushuzi mara kwa mara bila kutulia na kusababisha harufu nzito iliyowasumbua, lakini bado hakukuwa na heshima wala nidhamu ya kuwasikiliza

Pia Rubani wa Ndege hiyo alitoa Onyo kuhusu Tukio hilo na ugomvi huo lakini bado hali haikuwa shwari , na ndipo alipoamua kutua kwa dharura huku polisi wakiwa wameshafika eneo la tukio.

Hata hivyo, Shirika hilo linadai kuwa, liliwaandalia njia nyingine ya usafiri katika ndege yao ambayo ingeondoka kesho yake

Kwa upande mwingine, Ndugu hao wawili wamepanga kufungua mashtaka dhidi ya shirika hilo la ndege.

KARUDI KUNDINI !!: HATIMAYE HITMAKER WA "CHOKOZA", MARYA, NAYE AMEAMUA KUOKOKA

1:12:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
#WatuWaMungu Halelluyaaaaa !
Hii ni kutokana na namna ambavyo idadi ya kondoo wanaoamua kurudi katika Kundi inavyozidi kuongezeka kila kukicha na hii inaashiria kuwa upako umeanza kutawala mioyo ya Watu mbali mbali maarufu.

Nchini Kenya, kama utakuwa unaufahamu vema mkwaju wa CHOKOZA uliomuhusisha Bibie Avril pamoja na Marya, basi itabidi uendelee kuuenjoy maana nadhani itakuwa ndiyo last HITSONG ya Muziki wa kidunia kutoka kwa MARYA.

Bibie huyo ambaye pia ni Ex wa Colonel Mustafa, ameamua kubwaga manyanga ya masuala ya kidunia na kuamua kumrudia mungu ...yaani kuokoka.

Kama utakuwa unatembea sana katika masuala ya mitandao ya kijamii, utakuwa umeshakutana na video Clip ambayo inamuonesha Marya akiwa katika kanisa la Mchungaji maarufu Nchini Kenya, Pastor Burale, na kukiri kuwa ameamua kumrudia mwenyezi mungu na huo ni uamuzi wake

Hii imetokea ikiwa ni baada ya Juma moja tangu amani atangaze rasmi kuwa yeye ameokoka bila kificho na hivi sasa anamtumikia mungu moja kwa moja na wala hayuko kibiashara

Kama utakuwa unakumbuka vizuri, awali Marya aliwahi kukumbana na kashfa ya Usagaji, kisha akatiwa Dosari na kuvunjika kwa mapenzi yake na Colonel Mustafa huku akirushiwa tuhuma nyingi na Ex wake huyo, na hivi sasa tayari yupo katika Maisha yake ya kifamilia na boyfriend wake mpya

MNADA BANNER