REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

NICKI MINAJI AFUNGUKA KUHUSU OMBI LA DJ KHALEED

11:36:00 AM Add Comment

ZIMA NIKUPE MTONYO;

HATIMAYE Badaa ya kusubiriwa kwa Muda Mrefu sana kuhusiana na Ombi la Ndoa kutoka kwa Dj Khaleed, NICKI MINAJ amefunguka rasmi..Heheheiyaaaa...Kudaaaadeki !

Baada ya DJ KHALEED kuelezea Hisia zake juu ya Mtoto Mrembo Minaji kupitia Kituo cha MTV, kila mtu amekuwa yuko kimya sana kusikia ni kipi ambacho atakijibu Sweetie huyu, kama ni NDIYO, ama Kibuti

KAULI YA NICKI MINAJ
Lakini licha ya Nicki Minaji kutokuichukulia ishu hiyo Serious kihivyo, bado aliwaacha Mashabiki wa KHALEED na Yeye Mwenyewe Kinywa Wazi baada ya Kusema haya:

"Nilishtuka sana kama ambavyo Ulimwengu Mzima ulishtuka. Nilicheka pia kama ambavyo ulimwengu Mzima ulifanya hivyo, kwa sbabu Khaleed ni Mtu anayesimamia kila anachokifanya."

Bora hata ya Kauli hiyo, lakini ya kushangaza zaidi ni Hii aliyoisema mwanamama NICKY
" Ilikuwa ni Njia nyingine ya kipekee, kwa yeye kutoa sehemu ya Ujumbe ama maneno ambayo yatapatikana katika Wimbo wake Mpya"

TRACK HIYO PAMOJA NA ALBAM MPYA:
Hilo lilikuwa ni neno la kuitengenezea Njia Track yake pamoja na Albamu yake Mpya. Ngoma yake hiyo inaitwa "I WANNA BE WITH YOU" ambayo amemshirikisha Nicki Minaj, Future na Rick Ross. Albam yake itatambulika kwa Jina la SUFERRING FROM SUCCES

NICKI ALICHUKULIAJE TAMKO LA DJ KHALEED.

"Khaleed Ni Kaka angu, na hakuwa Serious wakati anatamka ombi hilo la Ndoa kwangu. Ifahamike hivyo Tafadhali. Alikwa anatania. Khaleed hajavutiwa na Mimi na wala hanihitaji Kimapenzi. Ni Mtu na Dada Yake" Alisema Nicki




LHRC - "TUTAMBURUZA PINDA MAHAKAMANI"

9:07:00 AM Add Comment

Kituo cha  Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), wiki hii kinatarajia kumburuza mahakamani, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumtaka afute kauli yake aliyoitoa bungeni mwezi uliopita kwamba Polisi wawapige raia wanaoleta uchokozi na kuashiria uvunjifu wa amani hapa nchini.

Mwezi uliopita Pinda katika mkutano wa Bunge la bajeti mjini Dodoma alitoa kauli ya kulitaka jeshi la Polisi nchini kuwapiga raia wanaokaidi amri halali ya jeshi hilo wakati aikijibu maswali ya Papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia, alisema taratibu zote za kisheria za kumfikisha Pinda mahakamani zimekamilika na siku yoyote wiki hii watafungua kesi.

Sungusia alisema kauli ya Pinda, imevunja katiba ibara ya 13 na kwamba lazima sheria ichukue mkondo wake kwa mkumfikisha mbele ya mahakama.

Alifafanua kuwa ibara ya 100 inayompa kinga mbunge anapotoa jambo lolote bungeni inamweka kando Pinda, kwa kuwa yeye hakuzungumza bungeni kama mbunge bali alikuwa anatoa msimamo wa serikali yake.
 Alisema kauli ya Pinda ilikuwa kali na mbaya na kwamba, walimtaka Pinda aifute siku chache baada ya kuitoa, lakini mpaka sasa amekaidi na hivyo wameamua kuchukua hatua ya kumfikisha mahakamani ili haki iweze kutendeka.

Pinda alitoa kauli hiyo nzito alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyetaka kujua kauli ya serikali juu ya vyombo vya dola kudaiwa kuwapiga raia hususani katika mikoa ya Mtwara na Arusha.

Akijibu swali hilo Pinda alisema “Mheshimiwa Mangungu hapa ameanza vizuri, lakini mwisho hapa naona anasema vyombo vya dola vinapiga watu, ukifanya fujo au umeambiwa usifanye hiki ukaamua kukaidi utapigwa tu.”

 Akaendelea kusema kuwa, “Lazima wote tukubaliane kuwa nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya sheria na kama wewe umekaidi, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndio jeuri zaidi, watakupiga tu,"
“Na mimi nasema wanaokaidi amri halali ya Jeshi la Polisi muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine ya kupambana na wakaidi zaidi ya kuwapiga,” alisema Pinda.


T.A.T NIPASHE

ZIMA MOTO : OLE WENU MNAOTUCHEZEA.....

8:59:00 AM Add Comment


Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, limesema liko mbioni kupata ‘mwarobaini’ kwa wananchi wanaotoa taarifa za udanganyifu na lugha za matusi kwa kupiga simu za uongo kwa jeshi hilo.

Jeshi hilo limesema katika kukabiliana na hali hiyo, litafunga mtambo wa kuwabaini wahusika hao.
Naibu Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini, Jenerali Saimon Mgomba, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akiwatunuku vyeo maofisa tisa wa jeshi hilo.

Alisema changamoto kubwa inayolikabili Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini ni kupokea taarifa za uongo kutoka kwa baadhi ya wananchi kuwa kuna tukio la moto.

Mgomba alisema jeshi hilo hupokea wastani wa taarifa za simu za uongo 20 kwa siku kwamba kuna matukio ya moto yametokea katika maeneo fulani.

Aliongeza kuwa mbali na kuwapo kwa miito ya uongo, pia hupokea lugha za matusi kutoka kwa baadhi ya wananchi. “Haya ni mateso makubwa tunayoyapata, nasema siku zao zinahesabika ndani ya wiki mbili hadi tatu tutafunga mtambo wa kuzijua namba hizo pamoja na majina yao,” alisema Mgomba.

Alisema zoezi hilo litaanzia Dar es Salaam na litakuwa endelevu katika mikoa mingine muda mfupi ujao.

Aidha, alisema malengo ya Jeshi la Zimamoto kwa sasa ni kufika katika eneo la tukio ndani ya dakika 15 lakini wanakwamishwa na tatizo la miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam kutokana na foleni.


Pia alisema tatizo la visima vya kuchotea maji bado ni changamoto na kueleza kuwa hadi sasa wana visima vitano vinavyofanya kazi na zaidi ya 1,000 vibovu.

UCHUMBA KWA NICKI MINAJ : DJ Khaleed Hajakata tamaa, na hatokata Tamaa

2:55:00 AM Add Comment

IKO HIVI....
Kama Unadhani Dj Kahleed alikuwa anatania katika Hatua ya Kumuomba Uchumba mwanamama Nicki Minaji, basi jamaa hakuwa hivyo.

Akiwa katika Interview na POWER 106, CEO huyo wa WE THE BEST alisisitiza kuwa hakuwa anatania kumuomba Uchumba Memba huyo wa YMCMB (Nicki), bali ameelezea uwazi juu ya Hisia Zake

"Nilitakiwa kuwa Muwazi katika Hili. Ninampenda sana na Imenibidi niamue kumuomba Uchumba ili hatimaye Nifunge naye Ndoa. Ni rafiki angu Kweli" Alisema Khaleed , ambapo pia kauli yake iliungwa Mkono na Rafiki ake wa Karibu RICK ROSS  "The Boss"

Pia Khaleed aliongeza kuwa, anaamini Minaj na Yeye wanaendana kabisa kiasi kwamba huenda ikawa Rahisi kwao kufikia hatua Nzuri

"Kama akinitolea Nje, ni sawa coz ndio mapenzi. Minaj ni Rafiki angu na ninaliheshimu hilo. Labda atakuwa hajawa tayari kwa Ndoa. Ninahitaji watoto sasa, na mambo mengine Mengi tu"

Mpaka Hivi sasa Nicki Minaji hajajibu chochote kuhusiana na Ombi la Dj Khaleed.





HAYA : KANYE HATOSHTAKIWA KWA UKABAJI

8:19:00 AM Add Comment

UNACHEZEA Kichwa ya Kanye Wewe????
Kuna uwezekano Mkubwa Rapper wa BLACK SKINED HEAD Kanye West akapona pona kushtakiwa katika Kesi ya kutaka kumuibia kamera PAPARAZI mmoja, Wiki Ilopita.

Kwa mujibu wa Mwanasheria wake, inasemekana Kuwa, Idara ya Upelelezi Nchini Marekani bado inaendelea na Uchunguzi wa Tukio hilo, lakini anaamini kuwa KANYE WEST hawezi kufanya Tukio la Ukabaji

Awali iliaminika kuwa, Jeshi la Polisi Nchini humo, liliazimia kufungua Mashtaka ya UKABAJI kwa Mpiga picha, tukio lililofanywa na KANYE WEST.

hata Hivyo Kanye Mwenyewe na mwanasheria wake wamekanusha Kutenda Kosa hilo

TIZAMA PICHA HIZI ZIKIONESHA KUJERUHIWA KWA PAPARAZI HUYO, BAADA YA TUKIO LA KUZINGULIWA NA KANYE WEST








BATA BOYS & BATA SHOSTEEZ...WHERE ARE YOU AT?...ROCK CITY IS GOING HOT

8:04:00 AM Add Comment

MNATO WA SIKU : A HAPPY KID CARRYING A HAPPY KID

7:57:00 AM Add Comment

HAPO VIPI: Mtoto Caren akiwa amembeba Mdogo wangu Ndundu Jr. Love them alot

BBA THE CHASE : SULU AMTOLEA UVIVU CLEO

7:52:00 AM Add Comment

SULU (zambia) amemtolea Uvivu MzambiaMwenzake, mwanadada CLEO, baada ya kuona kama amejiachia sana.

Washiriki hao wawili wanaoiwakilisha Nchi hiyo, wameonekana Mchana huu katika Bustani ya BB, wakiongea kwa Ukimya zaidi.

Katika mazungumza hayo, Sulu amemkanya Cleo kuepukana na WEMA anaoufanya kwa washiriki mbali mbali, jambo ambalo amehisi linaweza kumfanya aonekane ni mtu wa aina hiyo, na kukaribisha Mengi katika Mchakato wao wa Kutaka kupeleka Heshima ya Ushindi Nchini Kwao




PICHA: MUONEKANO MPYA WA "NDINGA" YA CHRIS BROWN

7:40:00 AM Add Comment
 ILIKUWA HIVI : Muonekano wa Zamani wa Ndinga ya Chris Brown

 SASA IKO HIVI : Muonekano Mpya wa Ndinga Yake

NIMETOA HAPA: Rangi mpya katika gari la CB, umetoka hapa

MR. NICE AKUMBANA NA BONGELA AIBU.

7:42:00 AM Add Comment


Baada ya Kujitapa kuwa sasa Yupo katika Bonge la LEBO na atafanya makubwa akiwa Nchini Kenya, PENGINE sasa MZIMU wa Mikosi unaanza kumuandama LUCAS MKENDA maarufu kama Mr. Nice.
MR.Nice amekumbana na Adha Kali baada ya Kushindwa kufanya Vizuri katika Show iliyofanyika katika Eneo la Kericho, na Hatimaye Kuambulia ma –Booooooooooooooooooooooooo ya kutosha na Kupoteza kabisa Mzuka.
Aidha baada ya Kuharibu katika Stage, Promoter aliyendaa Show hiyo alikataa kumlipa Mr Nice, na Kumuacgha jamaa akiambulia patupu.
Katika Tukio linguine laKushangaza, ni baada ya Mkali huyo wa zamani wa TAKEU pamoja na Promoter huyo kupata Kisanga cha Kuzimikiwa na Gari  walipokuwa wanaelekea katika Eneo la LITEIN – BOMERT na kuwafanya kusimama masaa kadhaa katka safari yao kabla ya Kupata Msaada.

BBA THE CHASE: WATATU WAINGIA KIKAANGONI…………..TANZANIA JE?

7:33:00 AM Add Comment

Na Ntty E

Kama Kawaida, Kila Wiki lazima Watu qwaingizwe Kikaangoni ili Mtu aweze kusepa,na wengnewaeze kusurvive kwa ajili ya kusaka Ushingi.
Wiki hii Mchakato ulikuwa Mgumu Kidogo kiasi kwamba ilileta Kimuhe muhe cha Washirikia kuchaguana mara kadhaa ili apatikane Mtu wa kwenda kikaangoni juma hili.
Lakini Mwisho wa Siku Washiriki watatu wakapatikana, hali iliyoleta utofauti na Utaratibu wa kawaida,ambapo huingia 7 kikaangoni, na Wawili kutoka.
Walioingia Kikaaangoni Juma hili ni Hawa
Annabel (KENYA), Elikem (GHANA), na  Sulu (ZAMBIA)
  
WAKATI Watatu hao Wakiingia Kikaangoni huku Watanzania tukizidi kupeta ndani ya Jengo Hilo la KAKA MKUBWA, Mtanzania Nando pamoja na Mnamibia DILISHI wameonekana kumalizaTofauti zao.
Kikubwa ambacho kiliwafanya wawili hawa Kugombana, ni Kitendo cha NANDO kushindwa kuhifadhi masuala ya Kibinafsi hasa walipokuwawakitaniana Wao wawili, na Badala yake amekuwa akiyafikisha Kwa watu.
Sababu kubwa  ambayo ililetaq Mzozo ilikuwa ni Baada ya NANDO Kutangaza Kwa watu kuwa, Mwanadada DILISH alimshika UUmewake wakati wapo Bafuni,jambo ambalo lilimuudhi sana Mwanadada huyo, huku akilalalamika kuwa, Nando Pia amekuwa akimshika makalio yake mara Kadhaa,likini hakumwambia Mtu,maana alichukulia ni Masuala ya Utani.

ROCK CITY: VIPAJI VIWILI KWA KICHWA HIKI....

7:10:00 AM Add Comment
READY TO ROCK : Msanii wa HipHopna Mtangazaji wa kituocha Redio cha Metro (METRO FM 99.4 MHz) akiwa Katika Mnato,baada ya Kuandaa Package la Show ya JAM SESSION

 NIPO KAZINI: Mwandada Edna "Natty E" akiwa Katika Stage akishusha Mikwaju hatari kunako RapMusic
 ARE YOU READY !!!: Natty E Kazini

TUENDELEE AMA TUSIENDELEE? : Stage kwake huwa Haitoshi....ongezeni Nyingine jamani

BIO:
NAME : Edna Elisha
AGE: Secrety
BIRTH DATE : October 27
TRIBE : Luo
WORK : Radio Presenter at Metro Fm 99.4 Mhz / Hip Hop Artist
RECIDENCE :Mwanza
EDUCATION: Secret
LIKE: Music and other good Stuffs
DISLIKES : Snitches
FACEBOOK : facebook.com/ Natty E


HAVE A GOOD NIGHT

11:35:00 AM Add Comment

I wish You all the Sweet Moments In Your Dreams. Keep Smiling Guys. I real love You all
Frank M. Joachim
C.E.O BLACK TOUCHEZ

MKWAJU MPYA : BIGGER THAN LIFE- Chris Brown Feat. Tyga, Lil Wyne & Birdman

11:29:00 AM Add Comment

MPENZI DEAR BABY : KWANINI NAKUPENDA

8:16:00 AM Add Comment

Na Frank M. Joachim.
Napenda Sana Kukuambia NAKUPENDA SANA ama I LOVE YOU SO MUCH mara Nyingi katika Mazungumzo yetu. Lakini unaju ni kwanini?  :

  • Unajua ni nini maana ya Uwepo wangu katika Maisha yako
  • Unamatarajio na mimi katika kila aina ya Mpango wako na hata wangu.
  • Unajua thamani ya Ahadi ambazo tulidhamiria kuzikamilisha.
  • Hupendi niwe Mpweke, Mnyonge, na hata kutokuruhusu Kutawaliwa na Mawazo katika akili yangu.
  • Unanipenda Mimi na Kila kitu nilichonacho.
  • Wewe ni Kipofu katika Mapungufu yangu Hasa katika Muonekano wangu wa Nje.
  • Unajua namna ya kucheza na sehemu kubwa ya Mahitaji yangu.
  • Unajua kutoa faraja hata nisipoihitaji.
  • Neno lako "Nakupenda" linabeba kila hisia ya Kimapenzi kutoka ndani ya Moyo wako.
  • Unafahamu Utani ninaouhitaji katika Muda Husika, na hata mazingira husika.
  • Hupendi kuchukia mbele yangu.
  • Hujui kunilinganisha na Mtu Fulani mwenye hadhi fulani.
  • Hupendi kunidanganya, maana unakuwa huru katika Kila kitu hasa ukiwa na Mimi.
  • Unatamani sana niwe Sehemu kubwa ya Furaha ya Maisha yako.
  • Unatamani sana Kujenga Familia yenye MAFUA (Mapendo, Furaha na Amani) na mimi. 
Sina Budi kusema "Ninakupenda" kila ninapohitaji kukuambia Hivyo. Ninakupenda

TANGAZO LA FIAT MPYA: TUPO KAZINI

7:16:00 AM Add Comment

HEBU Tizama Piacha Hii kwa Umakini...then Tizama kwa mara ya Pili

Yes, hao ni Wanamitindo (Mamodo) 13 Waliojipinda kadri ya Uwezo wao, katika Kutangaza Ndinga Mpya ya FIAT 500 ABARTH. 
Models hao walikuwa Uchi kama walivyozaliwa, lakini walipakwa rangi na kuonesha Muonekano Halisia wa Gari hiyo Mpya.

UNYANYASAJI: JAMAA AMFANYIA UKATILI MBAYA BINTI HUYU BAADA YA KUMKATAA KIMAPENZI

3:07:00 AM Add Comment
Victoria Akionesha Kovu Lake kubwa katika Mguu

Victoria akionesha Sehemu nyingine

                                    Victoria akionesha Makovu Mengine katika Mkono (PICHA ZOTE NA DJ. ALEX)

Na Frank Joachim & Dj Alex.
Licha Ya Kupigiwa kelele kila Siku, suala la Unyanyasaji bado linazidi kushika kasi katika Maeneo Mbali mbali.

VICTORIA LUMWA, alikutana na Mkasa ambao haukuwa na Maana ya kumpatia makovu yenye Mateso makali kama anayoyapata Hivi Sasa.

ANAISHI WAPI:
Victoria ni Mkazi wa jiji la Mwanza, na anaishi maeneo ya IGOMA. Binti huyu anaishi na Dada yake, ambaye ni Mlezi wake Kwa hivi sasa

KISA CHA KUKUTANA NA MKASA HUO:
Kwa Mujibu wa maellezo yake, kuna Kijana amekuwa akimtaka Kimapenzi kwa Muda Mrefu, jambo ambalo Binti huyu hakuwa tayari kulifanya kwa kuzingatia Hisia zake. Baada ya Victoria Kumkataa Kijana huyo, majibu yaliyotoka ni "Si Unajifanya unanikataa...sasa Ngoja utaona."

Kauli hiyo haikumshtua sana Binti huyu Mrembo wa Kiafrika, na kuamua kuendelea na Maisha yake ya kawaida. lakini siku moja wakati anasafisha Vyombo nyumbani kwa Dada yake, alishangaa Ghafla anatokea Mtu akiwa amebeba Sufuria, huku ndani yake kukiwa na maji ya Moto.

Baada ya Victoria kuhisi hali ya hatari, aliamua kujikinga na Mkono na Kugeukia ubavu mwingine, ili kuepusha maji hayo kumpata Usoni. Dhamira kubwa ya Mtendaji wa tukio hilo, ilikuwa mni Kumuunguza Victoria Usoni, ili kuiharibu Sura yake ambayo inasemekana kuwa ndiyo inayompatia Kiburi cha Kuwakataa wanaume.

IMANI ZA KISHIRIKINA :
Victoria anaamini kuna uwezekano wa Imani za Kishirikina kuhusika kwa namna moja ama nyingine. Sababu za Victoria kusema hayo ni :

  • MTENDAJI wa Tukio hilo alikuja kimazingara, baada ya Kutokea Ukutani akiwa katika Mavazi ya ajabu na kuchukua hatua hiyo, kisha Kupotea Ghafla.
  • Jamaa aliyemtongoza na kumtishia Hilo, ni Mkazi Wa KIGOMA, ambako KWA IMANI zake yeye (Victoria) anadai kuna Imani za Kishirikina


SHAVU: OCTOPPIZO KUSHARE ONE STAGE NA 2 CHAINZ

1:47:00 AM Add Comment
2 Chainz kwa Stage

Baada ya Ya CAMP MULLAH kuchangia Jukwaa Moja na SNOP LION (Zamani Snoop Dog Dogy), sasa ni Time ya Mkali wa Michano OCTOPIZZO kukutana na 2 Chainz kuna Stage Ileile.

Mkali Huyo wa IVO IVO tokea 254- Kenya, anatarajia kuzima na Bonge Moja la Show litakalofanyika Nchini Uingereza, huku akishea Stage Moja na Rapper Nchini Marekani 2 Chainz katika Ukumbi wa UN-CONVENTION CONFERENCE ulioko BIRMINGHARM.

Show hilo ambalo litashushwa Mnamo September, ni Maalum kwa ajili ya Kuhamasisha hasa katika madhara ya Masuala hasa ya Vita ama migogoro mbali mbali ya Kisiasa.

OCTOPIZZO "Mr IVO IVO"

Lakini, hii inaweza kuwa ni sehemu ya RUNGU ambalo atamuumiza Adui yake RABBIT maarufu kama KAKA- SUNGURA ambaye Siku chache zilizopita alionekana kumdiss vilivyo kupitia Mtandao wa Twitter

TETESI: KASHFA YA PEKEE KWA SIZE 8.

1:25:00 AM Add Comment

IKIWA ni Muda Kadhaa tangia Amamua Kuzima katika Michakato ya Mikwaju ya Kidunia na Kuamua kuingia katika Mikwaju ya Injili, Mwanamama Size 8 al the way from 255 Kenya, amekumbana na CLASSIC Skendo. Unataka kujua ni Ipi, Basi Zima nikupe Mtonyo.

Kwa Mujibu wa Mtandao wa Daily Post kupitia Nairobi Exposed, inasemekana Kuwa Mwanadada huyu mweye kila hadhi ya Kuitwa Sexy beibe amewatupa Wazazi wake waili ambao maiosha yao ni Magumu.

Mwanadada huyo anayemiliki Mamilioni ya Fedha huku akitikisa na Kwaju la MATEKE, anadaiwa kuonekana kumwaga Mikwanja katika kunisa ambalo inasemekana Eti, ndilo ambalo hulitumia kufikisha Maombi yake kwa Mwenyezi Mungu.

Tofauti na Kulisupport sana kanisa hilo linaloitwa BARAKA INTERNATIONAL CHURCH liliopo Kairobangi South Mjini Nairobare, Size 8 anadaiwa kusitisha huduma na Kumpotezea kabisa Bi. Mkubwa ake, yaani mama ake.

Wadaku hao wamefafanua Chanzo cha SIZE 8 Kuwakaushia wazazi wake hao, ni kutokana na kutokuwepa kwa Maelewano mazuri baina yao (Wazazi Wake)


Pia inasemekana kuwa, Wazazi wake wamekuwa wakijitahidi kumpigia Simu mara kwa mara, lakini Eti, SIZE 8 huwa anazipotezea kabisaaaa

BBA THE CHASE :KUNACHIMBIKA NDANI YA RUBY…ZIMA KWANZA NIKUTONYE

12:54:00 AM Add Comment

NA FRANK JOACHIM
PENGINE Game limeanza kushika  Fleva katika Mjengo wa BBA. Inaonekana Dhahiri kuwa huenda kukawa na KIJIBIFU cha Kimya Kimya kwa wana RUBY 3, namzungumzia CLE, FEZA (Tanzania) na ONEAL (Botswana).

Katika Muda wa Diary, Mrembo CLEO alionesha msononeko Mkali katika Hisia zake, huku akitoa Machozi wakati akipiga Story na BIG BROTHER. Cleo alifunguyka kuwa, tayari anamini yupo katika Maelewano mabaya na Wanandoa Wapenzi wawili FEZA na ONEAL ambao wanafahamika kama ONEZA.

Akizungumza kwa Masikitiko na Hisia kali, CLEO alionsema kuwa, chanzo ni yeye kukaa katika Moja ya Corner iliyopo katika Nyumba ya RUBBY, inayoaminika kuwa maalum kwa Wawili hao (Feza na Oneal). Ninamnukuu CLEO akisema “Ninahisi kama Wana matatizo na Mie. Na Kama wana tatizo na Mie, Basi wanatakiwa waje kuzungumza na Mie. Ila nimemuomba Mwenyezi Mungu kuhusu hili na aweze kuniepusha nalo.”

Katika Upande wa FEZA, yeye alimfungukia BIG BROTHER kuwa Cleo anaonekana  ni Mbinafsi, ingawa haamini kama ni Mtu Mbaya. Ila tu anatakiwa kubadilika hasa katika Baadhi ya Vitu vichache.

ONEZA walionekana kumlalamikia sana Mzambia huyo hasa katika Muda huo wa DIARY, wakisema kuwa Kuna matukio mbali mbali ambayo ameyafanya na yanawakwaza

MNADA BANNER