REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PICHA: SKENDO LA NGONO LA PATRICK EVRA..

1:21:00 AM Add Comment
CAPTAIN: Patrick Evra akiwa Uwanjani na Timu yake ya Manchester United

SKENDO MWENYEWE: Mwanadada na Mwanamitindo Clara ambaye alifanya mapenzi na Patrick Evra, jijini Paris

 NDOA: Patrck Evra na Mke wake Sandra

 KITHIBITISHO: Patrick Evra akiwa amevalia Cheni ambayo pia Clara wa Paris alionekana ameivalia siku ya Tukio

 MAMITO : Evra na Clara ndani ya Paris

KITHIBITISHO: Clara akiwa amevalia Cheni aliyokuwa amevaa Patrick Evra

AKILI YANGU ILIVYO FINYU: MHE. DEO FILIKU NJOMBE, TUNASHUKURU KWA MSAADA WAKO, LAKINI HAKUKUWA NA SABABU YA MSINGI KUANDIKA HAYO MAANDISHI YA BLUU HAPO CHINI...HIZO NI SIFA TU...TENA ZA KISIASA

1:08:00 AM Add Comment

MKUU WA MKOA SINGIDA: WALIMU KAJIFUNZENI MAPATO NA MATUMIZI

1:01:00 AM Add Comment

Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya sekondari Mwanzi Manyoni mjini.Dk.Kone hakufurahishwa na hali duni ya ofisi ya mkuu wa shule hiyo wakati shule ikiwa na akiba ya zaidi ya shilingi milioni sita


Na Nathaniel Limu.
Mkuu wa  mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone amemwagiza mkurugenzi mtenadaji wa halmashauri ya wilaya ya Manyoni, achague walimu wakuu wanne wa shule za msingi na wakuu wa shule za sekondari wanne, awapeleke shule ya msingi mchanganyiko Ikungi, ili wakajifunze juu ya matumizi bora ya fedha za umma.

Akizungumza na walimu wa shule ya sekondari ya Mwanzi iliyopo mjini Manyoni pamoja na viongozi wa wilaya ya Manyoni Dkt. Kone amesema shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilaya ya Ikungi,ni shule ya mfano mkoani Singida kwa matumizi mazuri ya fedha za uuma.

Amesema Ofisi ya mkuu wa shule hiyo ni nzuri mno, pengine si rahisi kuifananisha na ofisi nyingi za wakuu wa wilaya. Ina samani za kisasa, tv, kompyuta, internet, jokofu na makochi ya hali ya juu na kuwa Ofisi kama ile inavutia na inachangia mhusika kubaki ofisini kipindi chote cha kazi.

Akifafanua zaidi, amesema majengo ya shule ya msingi mchanganyiko Ikungi pamoja na ujenzi wa uzio wa ukuta, yamekarabatiwa/kujengwa yana ubora unaofanana na thamani ya fedha zilizotumika.

Dkt. Kone amesema walimu wakuu wa shule za msingi na wakuu wa shule za sekondari, hawana budi kufika kwenye shule hiyo ili kujifunza mwenzao Olivary Kamilly (mwalimu mkuu wa shule ya msingi mchanganyiko Ikungi) anavyutumia fedha za umma vizuri.

Mkuu huyo wa mkoa, ametoa agizo hilo, baada ya kutokuridhishwa na hali duni ya ofisi ya mkuu wa shule ya sekondari Mwanzi mjini Manyoni, wakati shule hiyo benki ina zaidi ya shilingi milioni sita ambazo zimekaa kwa muda mrefu bila kutumiwa.

Katika hatua nyingine, Dkt. Kone amewaagiza watendaji wa halmashauri za wilaya na Manispaa, kujenga utamaduni wa kutembelea miradi mara kwa mara, ili miradi yote ya maendeleo iweze kutekelezwa kwa ubora unaofanana na fedha zilizotumika.

Amesema katika ziara yake wilayani Manyoni, amebaini baadhi ya miradi imetekelezwa chini ya kiwango na kitendo hicho kimechangiwa na viongozi kutokwenda vijijini  kutembelea miradi.

“Acheni tabia ya kukaa maofisini, jengeni utamaduni wa kusimamia kikamilifu miradi ya maendeleo, ili iwe na ubora unakusudiwa uweze kufikiwa”alisema Dk.Kone.

Aidha, amewataka kutunza vizuri miradi iliyomalizika na ile inayohitaji ukarabati, ifanyiwe ukarabati unaofanana na thamani ya fedha zitakazotumika.


DODOMA ARE YOU READY?...MASTAA WA EBSS 2012 ATAANZIA KWENU

12:52:00 AM Add Comment

MAISHA CLUB Mjini Dodoma kutakuwa hapatoshi baada ya Mastaa wa Epic Bongo Star Search 2012 kuanzia Mkoani hapo siku ya Ijumaa, ikiwa ni moja kati ya ziara zao za Mikoani kwa Mwaka huu, ikifuatiwa na jiji la maraha, yaani DSM.

TIMU ITAKAYOSHUKA:
Raia watakaoshuka ni Menina Atik, Nsami Nkwambi, Mshindi mwenyewe Walter Chilambo, Wababa Mtuka, Geofrey Levis, Norman Severino, pamoja na Husna Nassoro

WATAKAOSINDIKIZA...
Barnaba Boy, Ali Nipishe, Linah, na Ben Paul himself.

SUPRISE kali itakayokuwepo siku hiyo, ni Mshindi wa ile "Mijihela", namzungumzia Walter Chilambo atakapozindua Mkwaju wake Mpya.

MNADA BANNER