REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HANGOVER MONDAY: HAIKUWA WEEKEND NZURI KWA MTOTO WA LIL WAYNE , REGINAE CARTER NA BOYFRIEND WAKE BAADA YA KUKAMATWA NA POLISI

1:51:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
IKIWA leo ni Jumatatu, Kupitia Weekend kuna matukio mazuri na mabaya ambayo yalitokea, ila kubwa zaidi, ilikuwa ni hili la Mtoto wa Rapper Lil Wayne na Boyfriend wake kulambwa na Pingu walipokuwa katika moja ya kiwanja cha Bata huko Nchini Marekani.

Reginae Carter (Binti wa Lil Wayne na Toya Wright) mwenye miaka 19 akiwa na Boyfriend wake YFN Lucci mwenye miaka 27 ambaye pia ni Rapper, walikutana na noma hilo Usiku wa kuamkia Jumamosi walipokuwa maeneo ya KNOXVILLE, TENNESSE, Marekani ambako YFN alikuwa meenda kwa ajili ya shughuli ya Special Appearance

Ingawa haijawekwa wazi chanzo cha tukio hilo ni nini, lakini Camera ziliwansa wawili hao wakibishana na Polisi waliokuwa katika eneo la tukio, hali iliyosababisha kutiwa pingu na kupelekwa kituo cha Polisi cha Knoxville na kuwekwa ndani kwa masaa kadhaa

Pia baada ya muda kidogo, Binti huyo wa Lil Wayne alipost kupitia instagram account yake akidai kuwa yuko sawa na hayupo jela.

Mpaka hivi sasa taarifa rasmi kuhusu kukamatwa kwao hazijawekwa bayana ingawa wengi wanaamini inawezekana kabisa kulikuwa na kutokuelewana baina ya YFN Lucci na waandaaji wa Show hiyo.

Wawili hao walianza kutajwa kuwa na mahusiano mapema mwaka huu ingawa Reginae Carter alikuwa akikanusha uwepo wa mahusiano yao, lakini hivi sasa mambo yako hadharani

MAMBO YAMEKUWA MABAYA : RAPPER T.I ANAOMBA KESI YAKE NA KAMPUNI YA INAYOMDAI...ITUPILIWE MBALI !!!!

1:31:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
#WatuWaMungu Rapper T.I ameamua kupinga mashtaka ya kukatisha mkataba na kutokulipia "vito" vya thamani a.k.a "Bling Bling" za moja kati ya kampuni ambayo ilifungua mashitaka dhidi ya Rapper huyo.
 
KAMA ULIKUWA HUFAHAMU..... 
Wafanya Biashara wakubwa wa Vito hivyo vya thamani AYDIN & CO ambao huuza vitu kama vile cheni, saa Heleni kwa Watu maarufu wenye majina nchini Marekani, mwaka 2015 walifungua Kesi dhidi ya Rapper T.I kwa madai kuwa Hit Maker huyo wa WHATEVER YOU LIKE alikiuka makubaliano yao ambayo yalikwekwa kwa njia ya mazungumzo (Oral Agreenment) kuhusu yeye kuchukua na kutumia vito hivyo vya thamani, na tayari alikuwa hajalipia takriban USD 775,000 ya vitu ambavyo alichukua kwa wafanya biashara hao

Katika Madai yao, Kampuni hiyo inadai kuwa kati ya mwaka 2004 na 2012, walimuuzia T.I Bling za kiasi cha Maelfu ya Dolari za kimarekani ikiwema Heleni za madini ya Diamonds zinzogharimu USD 9500, Cheni yenye madini ya Diamonds inayogharimu USD zaidi ya 9000, Cheni aina ya DOG TAGS zinzogharimu USD 10,000, Cheni ya Mkononi ya kike yenye madini ya Diamonds inayogharimu USD 24,500, Saa ya Madini ya Diamonds yenye rangi ya Blue inayogharimu USD 30,000 pamoja na pete ya ndoa ya kiume inayogharimu USD 13,000

KINACHOENDELEA     
Sasa, baada ya kukutana na mashtka hayo na kesi kusikilizwa May 18, T.I ameiomba mahakama kupuuza na kutupilia mbali mashtaka hayo dhidi yake maana hakuna ukweli wowowte ndani yake, bali wanataka tu kufaidi kupitia yeye

Hata hivyo, mmiliki wa Kampuni hiyo, FEVZI AYDIN alidai kuwa, Kampuni yake pamoja na T.I walifungua akaunti maalum kwa ajili ya malipo, na T.I alikuwa akilipa mpaka Mwaka 2013 ambapo aliacha ghafla kulipa mkwanja huo.

Kesi hiyo imeahirishwa na kusikilizwa tena mpaka mwisho wa kipindi cha Joto

JUNE 04TH : TAILOR'S DAY

12:59:00 AM Add Comment

DAYS OF THE YEAR   
Tailors Day is a day where people are encouraged to dress their best and to reach out and thank the person that helps them achieve their high level of sartorial elegance. 

While off-the-peg clothes may have become commonplace, even among some of the best dressed, the tailor still plays an integral part in ensuring some people look their best, and Tailors Day is the day to thank them.

There is no doubting the skill of a good tailor. They can create the perfect outfit, for any event, and can make even the most casual dresser appear elegant and attractive. It stands to reason, therefore, that they should be properly celebrated.

Arguably the best way to celebrate the day, and to show thanks, is to wear a suit or outfit that was professionally tailored to fit. However, some people that are especially grateful choose to buy cards and even gift baskets for their tailors.

Arranging for a new suit could be considered an appreciable means of showing love for a tailor, because it means that they will be enjoying new custom and the sale of their skilled service.

MNADA BANNER