REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WANAUME: KUWENI MAKINI NA KUNDI HILI LA WANAWAKE HIVI SASA

3:05:00 AM Add Comment

Kuna muda unaweza ukajiuliza ni kwanini haya yote yanatokea, lakini kubali ukatae, ni ubunifu wa Kutafuta maisha, na unasambaa kwa kasi Katika Majiji ya Afrika Mashariki
Sikilizeni….

Kipindi cha Awali, tulikuwa tunaamini kuwa, Wizi wa Kupitia Mitandao Mbali mbali ya kijamii, hautokuja kuzuilika, lakini hivi sasa kila kitu kimeshakuwa wazi na hadanganyiki mtu Kupitia Mitandao ya kijamii hasa facebook.
Sasa, Mchakato Mpya Umeingia Town ambako kuna kundi la wanawake walioko katika Ndoa na wengine wajanja wajanja , wanawaibia Wanaume Mikwanja na hata mali zao kwa Kutumia Njia ya mahaba Niue.

Leo TTM tunakuibia Utundu huu kutoka kwa kundi hili linalotumia akili Ndefu na Nyiongi kuweza kumlaghai mwanaume mpaka akaingia Mkenge na kujikuta anaohonga ikiwemo kusalimisha kila kitu pasipo kujua anaibiwa au la.

Kuna Vitu Vingi sana ambavyo wanavitumia Akina dada hawa, na Leo TTM tunakusasambulia Baadhi, ili upate kushtukia.

1. ANAKUSOMA KWA KUKUFUATILIA.
Mara ya Kwanza, anaweza kukuona jinsi ulivyo we mwanaume, muonekano wako, na kila unachokipenda. Mara Nyingi hukufuatilia nyendo zako hasa katika kazi unayofanya, mali unazomiliki, na hata ofisi unayofanya kazi.


2. KUANDAA MAZINGIRA YA KUKUPATA.
Akina mama hawa watovu wa Huruma, hutumia Mbinu zxa Pekee sana kuandaa mazimngira ya kukuvuta iili Mwisho wa Siku ukae katika Tego lenyewe ambalo hukulitarajia.
Kwa kufanikisha hili, hukufuata katika mazingira yako ya kazi na kujifanya wanahitaji huduma, huku wakijitahidi kuweka appointment ya Siku Nyingine. Huja ni Vitu vya gharama ambavyo “Vimegongewa “ sehemu, mfano mavazi, Simu, Saa, Heleni, Mikoba/Pochi, Vito vyote vya thamani, n.k, mabvyo vitakushawishi kuwa kamwe sio matapeli wa Mujini.
Katiko hilo pia, watachukua Contact ama kuuliza mahali unapopendelea kupiga Lunch, ama Dinner huku wakijifanya kuwa wanakuwaga very Bize.

3. KUTUMIA MITANDAO/ MAWASILIANO.
Sasa bandugu ba Kiume, mkishatoa Contacts, basi wataanza kuwasumbua kwa Chartings au Calls ambazo ni zaa akili sana. Pengine hutumia marafiki zao wasomi kuwapa Madini ya kuzungumza na wewe.

4. HUJIFANYA WAKO SERIOUS NA KAZI PAMOJA NA MAISHA
Hakuna akili nzuri inayochezwa hapa. Unaweza ukashangaa anakuambia yuko Ofisini, ana kikao, anahitaji uwe on time, ni mchapa kazi, ni mwanamke wa Kikazi zaidi.
Huzuga kuwa ratiba zao zinabana sana kiasi kwamba atakuwa anakupiga karenda kila mkiplan kukutana.

5. HUJIFANYA KUJALI SANA HASA KABLA HUJAMTAKIA KUWA UNAMPENDA:
Muda Mwingi huwa makini sana na wewe. Atakukumbusha kula Lunch, kuwahi kazini, atajifanya kukunulia hata baadhi ya Nguo, ama zawadi za hapa na pale, hawezi kupata amani kama uko sehemu yenye mazingira magumu, na anapenda kukupa ushauri na mawazo Mengi ya kimaisha.

6.UKIWA NAYE KATIKA MAHUSIANO, TAJIFANYA NI MBUNIFU WA MIRADI.
Yaani hapo ndo kwanza mwanaume unaanza kuibiwa huku unajiona. Leo atakuambia amebuni Mradi Fulani ambao utakuja kuwaboreshea familia zenu na hata maisha kiujumla. Yuko tayari akupeleke kwenye Saloon au Duka la Nguo la rafiki yake, kukuzuga kuwa ni Mradi wake, ili uweze kumuona anaakili ya Biashara na Mpenda Maendeleo.
Sasa Utaasikia “Tuanzishe Mradi wa PUB, nadhani utagharimu milioni 9, ila mie ntaongeza Milioni 5 jkutoka kwenye Faida niliyopata hapa”
Ukijishaua kutoa, kudadadeki, ushaingizwa Mkenge Jombaaaa








MKOSI JUU YA MKOSI KWA BEYONCE: SAFARI HII BABA YAKE BEYONCE ASHTAKIWA NA MCHEPUKO WAKE

2:54:00 AM Add Comment
BABA BEYONCE

KAMA ilivyo kwa Jay Z, sasa Beyonce naye amekutana na Janga linguine ikiwa ni baada ya baba Yake Mzazi, MATHEW KNOWLES kufunguliwa Mashtaka na Kishtobe wake ambaye inasadikika amezaa naye Mtoto.

Sasa..suala lenyewe liko hivi kama ambavyo TTM tumelinyaka,

Bibie TAQOYA BRANSCOMB, amefungua kwa Mara Nyingine Tena Mashtaka huko TEXAS Marekani, kwa kudai kuwa alimpa ujauzito mnamo mwaka 2010, ikiwa ni baada tu ya mama Yake Beyonce, TINA KNOWLES kufungua Mashtaka ya kudai talaka toka kwa Mzee Huyo.
BEYONCE

Aidha, Mama Wa Beyonce aliamua Kuomba talaka Hiyo baada ya kubaini kuwa , Mumewe alikuwa akimsaliti na mwanamke mwingine ambaye walikutana mnamo mwaka 2009.

TAQOYA BARNSCOMB ambaye hivi sasa ana miaka 30, anasema alikutana na Mzee Mathew Knowles Mwaka 2010 na kupata ujauzito, na hivi sasa anaomba Wakachukue Vipimo vya Damu (DNA) ili kuthibitisha kuwa Yule ni Mtoto wake na lazima suala la malezi lizingatie Sehemu zote.

TAQORA

Ili kudhirisha kuwa Mzee huyu ni Kipenzi cha Michepuko, Pia aliwahi kukiri kuwa alimpa Ujauziti Mwanamke mwingine anayefahamika kwa jina la ALEXSANDRA WRIGHT, huku akiagizwa na mahakama kulipakiasi kadhaa kwa ajili ya matumizi, kabla ya kupunguziwa, baada ya Beyonce Kumfukuza kazi baba ake huyo, na kukosa Mkwanja kabisa

ETI 20% ANAKUTANAGA NA MIYEYUSHO YA HATARI

2:49:00 AM Add Comment
·      


Infact WENGI TUKITAMKA Jina la 20%, mnapata kumbukumbu ya Jombaa ambaye aliwahi kunyakua tuzo 5 za KTMA, kabla ya kumpata Mbabe wake Diamond Platnumz ambaye kazinyakua Tuzo 7.

Sasa baada ya Kukaa Kimya kwa Muda Mrefu sana huku akijaribu kutafuta Angle ya Ujio Mpya, Twenty ameshusha Moja ya Malalamiko kuwa, Miyeyusho ndo imemfanya Awe Kimya, na kutokufanikisha kazi ambayo aliplan kuja nayo…

Awali TTM tulisikia Vijifununu kuwa Mkali huyo wa MONEY kipindi cha Nyuma, kuwa yuko mbioni kuachia Brand New Song pamoja na Video ya SUBIRA ambayo pengine huenda ingemvuta vuta katika Ushindani 

Mgumu wa Soko la Muziki hapa Nchini Tanzania.
Baada ya kuul;izwa kuhusu hiyo ishu na Kudorora kwa Ujio wa Video Hiyo, Twenty alidai kuwa ni kweli hajatoa Video ya Wimbo wake huo wa SUBIRA, lakini kuna watu wanamzingua na Ndio maana mpaka Hivi sasa hajaaachia Chochote.


Pia TWENTY amemaliza kwa Kudai kuwa, alikuwa ameshaanza mchakato wa Video vizuri sana, lakini kuna watu ambao wana miyeyusho ya hatari na wamempotezea muda.

WHAAAT?: CHRIS BROWN NA KARRUECHE WAMERUDIANA TENA?

2:45:00 AM Add Comment

DAH…Hii inaweza ikawa ni “Mchanganyo” wa aina yake ambao tunatengenezewa na wawili hawa ambapo siku ya jana TTM tulikupa Mtonyo kuwa, wawili hawa wamepigana Chini baada ya Chris Kumtamkia neon bay asana Karrueche.

Sasa leo baada ya TTM kuzama kunako Kuchek updates za Ishu ya wawili hao, tumekutana na hili ambalo linaashiria kuna uwezekano wawili hawa wakarudiana Tena.

Chris Brown ambaye ni Mkali wa Miondoko ya POP na RnB, kupitia account yake ya Instagram, alipost Picha ya Kikatuni chake ambacho kilikuwa kimevaa Tisheti yenye Picha ya Karrueche ambaye Ni Mwanamitindo.

Kwa Mujibu wa Picha Hiyo, inawezekana kabisa Wawili hawa wakawa wanatafuta namna ya kurudisha Mahusiano yao ambayo ni asilimia kubwa yamekwisha Vunjika

Ikiwa ni Muda Mchache baada ya Kupigana Chini, Chris alifuta Picha zote za Karrueche katika Account yake ya Instagram, pamoja na kumu-unfollow, huku Bibie Karrueche akifanya Vivyo Hivyo.

Sasa Baada ya Chris Kupost Picha Hiyo, kuna Uwezekano mkubwa wakarudiana kama ilivyotabiliwa awali.

JAY Z BADO ANA MAJANGA: SASA YAMEHAMIA KATIKA STUDIO YAKE

2:42:00 AM Add Comment

KUNA MUDA TTM huwa tunajiuliza hivi sasa Rapper Jay Z yuko katika hali gani, baada ya majanga kuzidi kumuandama , ikiwa ni baada ya kuvuja kwa Video Clip akizxunguliwa na Shemeji ake Solange Knowles..Sasa Kuna Jipya hili nalo.

PRODUCER, na ENGINEER CHAUNCEY MAHAN, amedai kuwa Yeye ni mmoja wa wamiliki wa Studio ya JAY Z, inayofahamika kwa jina ROC-A-FELLA RECORDS.

Ishu hiyo imeshafikishwa Mahakamani mpaka hivi sasa, na kuna uwezekano ikafika mbali zaidi, baada ya kila kitu konekana kwenda mlama hasa kimaelewano baina ya wawili hawa.

Aidha Mahan ameshafungua Kesi ya Pili, huku akidai kuwa yeye ndiye Producer wa Kwanza kabisa, huku akisisitiza kuwa yeye ndiye Mbunifu wa Kazi za kwanza kabisa za ROC-A-FELLA RECORDS zilizotoka mnamo Miaka ya 1990 pamoja na Mikwaju Mingine amabyo ilitoka kuanzia Miaka ya 2000.

Tofauti na Hilo, Engineer na Producer Mahan ameongeza kuwa, kiujumla yeye ndiye amebopresha zaidi Instrumentals hasa katika Sound, katika mikwaju ambayo imepata mauzo bora katika Soko la Muziki Ulimwenguni.

Moja kati ya Mifano aliyotoa, ni pamoja na  THE LIFE AND TIMES OF S. CARTER VOL. 3 ya Jay Z, na THE DYNASTIC ROC LA FAMILIA ya Mwaka 2000.


Hata Hivyo Mahan anataka Hakimuamuidhinishe kama Mmiliki mwenza wa Hakimiliki katika Kazi ambazo amewahi kuzifanya akiwa hapo.

MNADA BANNER