REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

R.I.P SHARO MILLIONAIRE (INNALILAH WA INALILAH RAJIUN)

11:16:00 PM Add Comment



 PICHA BAADA YA KIFO CHAKE.................................





HIVI NDIVYO MSANII DIAMOND PLATNUM ALIVYONG'ARA KWENYE TUZO ZA NZUMARI 2012 (NZUMARI AWARDS 2012), NCHIN KENYA, KAMA "MSANII BORA WA KIUME"

8:33:00 AM Add Comment



















HIVI NDIVYO MUHAS ITAKAVYONG'ARA...

8:24:00 AM Add Comment

  • NI KATIKA KAMPASI (CAMPUS) MPYA YENYE KUVUTIA



Michoro ya ujenzi wa Kampasi ya Mloganzila iliyo kijijini Kwembe katikati ya Wilaya za Kisarawe Mkoa wa Pwani na Kinondoni Mkoa wa Dar es salaam. 

Hii ni sehemu ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) inayojengwa kwenye eneo la ekari 3800 kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa wanafunzi wa udaktari na huduma za Afya wapatao 15,000 kwa mwaka, na pia itakua sehemu ya kutolea matibabu ya maradhi yote makuu na ya kawaida nchini. Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, ujenzi wa Hospitali hii, ambayo pesa ya ujenzi wake imeshapatikana, unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Januari, 2013 na unatarajiwa kukamilika miaka miwili baada ya ujenzi kuanza. Kwa maneno mengine Kampasi ya Muhimbili ya Mloganzila inategemewa kuanza kazi mwanzoni mwa mwaka 2015. 

Tayari wataalamu na wafanyakazi wanaotarajiwa kufanya kazi katika kampasi ya Mloganzila wameshaanza mafunzo ndani na nje ya nchi. Mara hospitali hiyo kubwa na ya kisasa itakapokamilika itakua na uwezo wa vitanda vya kulaza wagonjwa mia sita (600). Sambamba na kampasi ya MUHAS ya Mloganzila pia ujenzi wa Kampasi ya Afya ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) umeshaanza na kufikia hatua ya juu na ambapo pia hospitali hiyo inatarajiwa kuanza shughuli zake rasmi mwaka 2015. 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii (National Health Insurance Fund) NHIF Bw. Emmanuel Humba mchakato wa kufanikisha uanzishaji wa Chuo Hospitali hiyo vimeshaanza ambapo baadhi ya wataalamu wakiwemo Madaktari na watumishi wengine wako nchini na nje ya nchi kwa ajili ya masomo na mafunzo mbalimbali. 

Chuo hicho kinatarajia kuwa na vifaa vya kisasa vya tiba vinavyokidhi mahitaji ya Afya na Elimu ya Udaktari wa kiwango cha Kimataifa, ikiwa ni mikakati kabambe ya serikali ya awamu ya nne katika kuhakikisha nchi ina wataalamu wengi na huduma za kisasa za afya ili kuondokana na adha ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu. Kwa sasa MUHAS inachukua takriban wanafunzi 2442 wa udaktari na huduma za afya kwa mwaka. 

Hivyo ujio wa kampasi ya Afya Mloganzila na Kampasi ya afya ya UDOM utaharakisha mpango wa serikali wa kupunguza wastani wa wagonjwa kwa daktari mmoja kwa kiwango kikubwa. Hivi sasa wastani ni daktari mmoja anahudumia wagonjwa 30,000.

AHSANTE MUNGU...Kweli SAJUKI AMEPONA...Hivi Ndivyo alivyoonekana IRINGA

8:12:00 AM Add Comment






MAANDAMANO ya KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA Nje ya Ukumbi wa Diamond Jubilee

7:59:00 AM Add Comment



IVORY COAST yaingiwa Na Utata

7:50:00 AM Add Comment





Serikali ya Ivory Coast imeingiwa na kiwewe juu ya kutekeleza agizo la Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC la kumkabidhi mke wa Laurent Gbagbo Rais wa zamani wa nchi hiyo, kwa kuhofia kuvurugika mapatano ya umoja wa kitaifa nchini humo. 

Taarifa zinasema kuwa, hatua ya kukabidhiwa Simone Gbagbo kwa Mahakama ya ICC itaitumbukiza nchi hiyo kwenye hatari zaidi serikali ya Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast. 

Taarifa hizo zinasema kuwa, Rais Ouattara yuko njia panda kati ya kutekeleza agizo hilo la kimataifa na kuitumbukiza nchi yake kwenye mfyatuko na mpasuko. 

Mahakama ya ICC imeeleza kuwa, Simone Gbagbo ana kesi ya kujibu kwani anakabiliwa na tuhuma za kutenda jinai dhidi ya binadamu kuanzia tarehe 16 Oktoba 2010 hadi Aprili 12, 2011 nchini humo. Waranti uliotolewa na ICC wa kutiwa mbaroni na kukabidhiwa mke wa Rais wa zamani wa Ivory Coast umekabiliwa na upinzani mkali kutoka Ivorian Popular Front FPI chama kikuu cha upinzani nchini humo.

MNADA BANNER