REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

INSTA COP: HUYU HAPA SASA MKE WA ABBY SKILLZ

3:12:00 AM Add Comment

Insta Cop    
WENGI tunafahamu kuwa Msanii Mkongwe katika Muziki wa Kizazi kipya hapa Nchini Tanzania, ABBY SKILLS hivi sasa ni Rasmi yuko katika Ndoa

Abby Skills alifunga Ndoa mwezi uliopita na Binti Mrembo ANDOYA KHALIFAN MRIMI ambaye Leo Insta Cop imeona Bora imlete Kwenu ili tumfahamu Shemeji Yetu

Tazama Picha zake







PICHA: THE GAME AFUMWA TENA AKIMNYEMELEA KIMAHABA BINTI WA MIAKA 17

2:45:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
Waungwana, Rapper The Game ameakamatika Tena akimnyemelea Binti mdogo mwenye umri wa Miaka 17.

Kwa mujibu wa Taarifa kupitia Dada wa Binti huyo ambaye alaimua kufunguka bila kificho kupitia Twitter account yake, ameshangazwa sana na kitendo cha Rapper The Game (41) kufanya kitendo hicho na kumchkulia mdogo wake kama ni mwanamke rahisi sana.

SYMPHANI ambaye Ndiye dada wa Ki-Binti hicho ambacho ni "under 18" alisema kuwa ilimlazimu amshauri mdogo wake abadili BIOGRAPHY yake baada ya kubaini kuwa huenda akaingia katika matatizo makubwa

Katika Bio Hiyo, Binti huyo aliamua kuandika umri wake kuwa "I am Seventeen" yaani "Nina Miaka 17"

Hii itakuwa ni mara yake ya 3 kuingia katika Kashfa ya kuwa-DM mabinti wenye Umri Mdogo sana kuingia katika mahusiano.

BINTI MWENYEWE HUYU HAPA 
 





BIRTHDAY VIBES: HAPPY BIRTHDAY CHEMICAL

2:27:00 AM Add Comment


Na Baba Juti  
WAUNGWANA tulianza kumshuhudia Bibie huyu hapa kupitia Track ya SIELEWI ambayo kamshirikisha SOPRANO, na kila mtu kuzungumzia uwezo wake kwa namna tofauti.

Ukiachilia mikwaju Mingine ambayo ameachia na hata kufanya Vizuri katika "kona" kadha wa kadha, Muonekano wake hasa katika kuvaa mavazi ya Kiume, uliwafanya Wengi sana wahisi kuwa ni Tom Boy kitu ambacho alikuwa akikipinga mara kwa mara

Baadaye Chemical aliingia katika HEADLINE kubwa ikiwa ni baada ya Rapper Mwenzake wa Kiume, STEREO "Singa Singa" kujitokeza hadharani na kudai kuwa, anampenda sana Chemical na anahitaji kumuoa.

Ingawa wengi tulikuwa Tunahisi hiyo ni "Kick" tu, Stereo alikuwa anaonekana kama yuko Serious, lakini kile alichoambulia kutoka kwa Chemiucal, ni Kibuti.

Mbali na hayo yote, Chemical aliushangaza Ulimwengu wa Muziki wa Bongo Flava baada ya kuweka hadharani kuwa yeye hamjui mwanaume anavyofanana hasa Kiundani zaidi, yaani yeye ni B!K!RA.

lakini kubwa zaidi, ilikuwa ni baada ya Chemical kuonekana kwa Mara ya kwanza kabisa akiwa amevalia Mavazi ya Kike na hasa ya Ufukweni mpaka kutupia Weaving, kitu ambacho kiliwashangaza wengi hasa Uzuri na Urembo ambao yuko nao.

LEO NI Siku yake ya Kuzaliwa...HAPPY BIRTHDAY CHEMICAL !!!!!

CALISAH: "KAMA UNA MILIONI 10, NITAVAA GAUNI LAKO WALA HAKUNA TATIZO"

2:08:00 AM Add Comment

Na Baba juti
WATU WA MUNGU yamesemwa Meeeengi sana kuhusu "Model" wa Kiume Hapa Nchini Tanzania, CALISAH ikiwa ni baada ya kuvaa kile kiatu cha kike ikiwa ni njia yake ya kuvuta mkwanja

Sasa baada ya kukutana na Kichambo, Ex-Huyu wa Wema Sepetu amedai kuwa, ni kitu ambacho kweli kimezungumzwa sana na hata kumuathiri katika Ngazi ya Familia hasa Upande wa Baba, lakini kila kitu kiko sawa mpaka hivi sasa

Calisah amedai kuwa, licha ya kuambulia matusi Makali na hata wengine kumuita "Shoga" bado kwake haijamuumiza kiasi hicho maana kubwa zaidi ni mkwanja ambao tayari ameshauvuta na wala hana tatizo

Kuhusu Mpenzi wake ambaye pia huenda labda aliathirika kwa namna moja ama nyingine au lah, Calisah amedai kuwa Mwanamke wake alikuwa anafahamu ishu hiyo kuanzia Siku ambayo anapigiwa simu kupewa Mchongo huo, na yeye pia ndiye alikuwa akimshauri kutokujibu chochote ama kutokushika Simu kabisa

Lakini katika kukazia Zaidi, MODEL huyu ambaye haishiwi na Majanga ya hapa na pale, amedai kuwa kama akatokea mtu mwingine labda anataka kupiga naye mishe hata ya Gauni, basi haina tatizo, yeye cha msingi aandae mkwanja kuanzia Milioni 10

MSIKILIZE        

ALICHOKISEMA T.I KUHUSU TUHUMA ZA NELLY KUBAKA

1:20:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
RAPPER T.I amedhihirisha kuguswa kwa asilimia kubwa sana na Ishu ya Ubakaji ambayo imemkumba Msanii mwenzake NELLY ambaye ni Hit Maker wa Mkwaju wa DILLEMA

Taarifa za awali zilidai kuwa Rapper Nelly anatuhumiwa na Binti mmoja mwenye miaka 21 ambaye ni shabiki wake kuwa, alimbaka katika After Party yake ambayo aliifanya Huko huko Washington

Pia Binti huyo alidai kuwa, Nelly alimualika yeye na Rafiki yake katika Chumba chake na kisha akampa kilevi na kufanikisha zoezi lake, tuhuma ambzo zilimfanya Nelly akamatwe na kisha kuachiwa.

Rapper T.I ameamua kutolea uvivu namna ambavyo watu wanamzungumzia vibaya Nelly na kumuamini Binti huyo, kitu ambacho kinahitaji ufikiriaji wa hali ya Juu sana

Katika kukazia Zaidi, T.I aliongeza kuwa, sawa Imeshatokea tayari Nelly kakamatwa, lakini itakuwaje iwapo itabainika kuwa Binti huyo anaudanganya umma, atachukuliwa hatua Gani?

MKWAJU WA SIKU: KITU-King Silver

1:05:00 AM Add Comment

Na Rich Sam 
WAKUBWA wa Kazi Safari hii tumeamua kumshusha kijana KING SILVER kunako "Mkwaju Wa Siku" ikiwa leo ni Jumanne

Mzigo umesimamiwa na Producer mwenye Umri Mdogo Jijini Mwanza, Charlee Best na umeachiwa Rasmi Mwezi September

LEO NI MAADHIMISHO YA SIKU YA MIKOBA

12:53:00 AM Add Comment

Days Of The Year
HAKUNA siri kabisa kuwa Wanawake wanapenda sana Mikoba, ingawa kuna muda inakuwa inazidishwa sana, lakini ni adhabu kubwa sana kumwambia Mwanmke ama Binti yoyote asibebe mkoba katika siku nzima akiwa katika "harakati" ama mihangaiko ya haraka 

Amini usiamini, siku ya Mikoba ipo na huwa inaadhimishwa kila OCTOBER 10, na kuna mataifa kadha wa kadha ambayo hutumia siku hii kufanya shughuli mbali mbali huku wakiwa na mikoba

Ukiachilia mbali suala hilo, Pia Wanawake wengi hutumia nafasi hii kufanya "shopping" ya Mikoba ambayo wanaifurahia na hata kutamani kuwa nayo, hali kadharika kwa wanaume ambao wanapenda kuwanunulia mikoba Wenzi wao mfano mke, mchumba, mama, dada, na kadharika

Wafanyabiashara wa Mikoba pia hutumia nafasi hii kuuza mikoba ya aina mbali mbali ambayo huwavutia wanawake kiujumla. na kama haitoshi, wabunifu mbali mbali hutumia nafasi ama siku hii kuonesha ubunifu wao katika maonesho ya mikoba

MNADA BANNER