REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KERI HILSON : NILIJITAHIDI KUKATA WATU ILI NITENGENEZE MAISHA YANGU TOFAUTI

1:35:00 AM Add Comment

Na Baba Juti 


MWAKA 2017 Ulikuwa ni mwaka wa ahadi nyingi sana kutoka kwa wasanii mbali mbali ambao hawakufanya Vizuri ..sio kitaifa tu, bali hata kimataifa

KERI HILSON ni mmoja kati yao na tulimzungumzia kwa Mengi sana ikiwemo yeye mwenyewe kukiri kuwa yuko mbioni kuachia Hits kadhaa na ikibidi Album kabisa, lakini ilikuwa ni tofauti na ahadi ambayo aliitoa.

Hitmaker Huyu wa TURN ME ON na LOOSE CONTROL amekuwa kimya kwa Takriban Miaka kama Mitano au sita, kitu ambacho kilitufanya baadhi ya watu tumsahau kidogo, lakini kumbe nyuma ya hayo yote, ilikuwa ni ushauri kutoka kwa marehemu bibi yake ambaye alimshauri kutulia kwanza na kutengeneza maisha yake upya, maana ni kama alikuwa ameshahisi kupagawa.

Tofauti na Hilo, Keri anadai kuwa, Ilimlazimu kukata baadhi ya marafiki na watu waliokuwa karibu naye maana ilikuwa ni kama wanampa Prersha tu na hata kumpa Stress, kitu ambacho kilimlazimu ajikute akifanya matukio ya kuumiza hasa katika Saikolojia yake

Katika kukazia Zaidi, Keri Hilson anadai kuwa, kitendo cha kuona kuwa hawezi kufika tena katika nafasi za Juu kwenye Charts tofauti za muziki Duniani, ilimlazimu aweke kando kidogo muziki ili aweze kujiweka sawa kabisa

UBAGUZI WA RANGI: RAPPER P. DIDDY YUKO MBIONI KUMPA DEAL MTOTO ALIYEDHALILISHWA?

1:05:00 AM Add Comment



Na RICH SAM
WATU WA MUNGU wanasemaga kabisa kuwa, ukikutana na mabaya, huenda ukawa umepata njia ya kukutana na mazuri hata kama utakuwa na maumivu kiasi Gani ndani ya Mtima wako ama moyo wako kiujumla.

Kwa Mujibu wa Taarifa ambazo tumezinyaka fasta kwa hivi sasa, ni kwamba Rapper na Mfanyabiashara kutoka Nchini Marekani, Sean Combs maarufu kama P.Diddy huenda akamwaga Deal nono kwa Mtoto aliyefanyiwa Ubaguzi wa Rangi na kampuni ya Mavazi ya H&M.

Taarifa hizo ambazo zimeenea maeneo lukuki, zinadai kuwa Mtoto huyo ambaye alitumika katika kutangaza Bidhaa ya kampuni hiyo, ambayo ilikuwa imeandikwa “THE COOLEST MONKEY IN THE JUNGLE” yaani “NGEDELE MTULIVU NDANI YA MSITU” ilihali kijana huyo ana Ngozi Nyeusi, ni Kwamba Diddy yupo katika harakati ya kusaini mkataba na Dogo huyo kwa ajili ya kumtumia kama Model wa kutangaza mavazi yake ya SEAN JOHN

Kama haitoshi, inasadikika kuwa, Diddy yuko mbioni kumwaga Kitita cha USD 1,000,000 sawa na Tsh 2,283,000,000 za kitanzania, endapo motto huyo pamoja na familia yake watakubali kumwaga wino na yeye

Tofauti na hilo, Watu kadhaa wameshaanza kujitokeza kutangaza Deal na motto huyo kwa gharama mbali mbali endapo atakubali.

MNADA BANNER