REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

NICKI MINAJI NA ALIYEKUWA DESINGNER WAKE WA MAWIG, NGOMA HAIKAI.

7:28:00 AM Add Comment

NEW YORK , Marekani.
Nicki Minaji na aliyekuwa designer wa mawig yake anayefahamika kwa jina la TRRENCE DAVIDSON, bado ngoma ni ngumu baada ya wawili hao kuonekana kuingia katika Bifu ambalo linatarajiwa kuwa la aina yake, TTM Jo vile tushazinyaka.

Kwa Mujibu wa CHIMBUA CHIMBUA, Mwezi February Designer Huyo alimfungulia Mashtaka Nicki Minaji hasa ya madai ya kiasi cha USD Milioni 30 kwa madai ya Kudhurumiwa na Bibie huyo Kutoka YMCMB, lakini Hivi Nicki Minaj ameamua kuvunja Ukimya na kufunguka kama Sio kumiminika.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Chimbua Chimbua wameshusha Ripoti kuwa, Nicki Minaji amesema kwamba, Desiogner huyo, amini Msiamini Si lolote, Si chochote bila yeye, maana yeye ndiye amemfanya kufikia hapo alipo, na hata kipaji chake kimefikishwa mbali na Nicki Minaj Mwenyewe.

Mkali Huyo wa Looking Back Fella (Looking Ass Niggah), na Moment For life, amesema kuwa, awali designer huyo, daidson, alitaka akajihusishe na masuala ya Reality TV shows, kipaji ambacho hakuwa nacho, lakini alimshauri afanye naye kazi katika Suala Zima la mawigi, jambo ambalo ana 

Ushahidi wa maandishi hasa katika makubaliano yao.

Hata Hivyo, Mpalka hivi sasa Nicki Minaj Bado hajakubaliana na madai ya Desgnerhuyo, hivyo anabaki tu kuchekelea Kuhusu mashitaka hayo.

IS DRAKE MOVING ON?..AONEKANA NA MCHUCHU MWINGINE BAADA YA KUTEAMANA NA RIHANA

7:22:00 AM Add Comment

NEW YORK, Marekani
Kuna Uwezekabno Mkubwa Kwamba Rapper Drake kutoka YMCMB akaaamua kupiga hatua ya kuenjoy maisha ya Kimahusiano, baada ya kutemana na Rihanna

Rapper huyo Mwenye Umri wa miaka 27, amepost Picha yake na Bibie mmoja ambaye inasadikika kuwa aliwahi kuwa mahaba Niue wake kipindi cha Nyuma, anayefahamika kwa jina la BRANDY PRINCE.

Tofauti na Kupost Picha Hiyo, Dreezy ambaye Hivi sasa ameingia katika kinyang’anyiro cha BET AWARDS-2014, aliandika Maelezo kuwea, yuko na Mpenzi wake wa toka kitambo, hivi sasa, na Tena na tena.

Ikiwa ni baada tu ya Drake kupost Picha hiyo, mamito huyo naye alipost Picha ya kaka yake anayefahamika kwa jina la JAS PRINCE, akiwa ameketi meza Moja na Drake (Shemejiiiii), huku wakigonga 
Mvinyo wa kutosha Pamoja na kupiga story za hapa na pale.

Mpaka hivi sasa Rihanna hajaonesha makali yake Ingawa wengi wanahisi huenda akarudisha majeshi kwa Aliyekuwa Honey wake Chris Brown, Pindi tu atakapomaliza Kifungo chake cha mwaka mmoja Jela, na Kukaa sawa.


Dreezy na Rihanna walilripotiwa kurudisha mahusiano yao mnamo Mezi February, lakini hivi majuzi tulipata mtonyo kuwa wawili hawa wamepigana Chini kwa kile kinachosadikika kuwa ni Drake kumpenda kupita maelezo Rihanna , na hata kufikia Kugombana haswa mara kadhaa

ALBUM YA MARIAH CAREY IKO TAYARI HIVI SASA

7:12:00 AM Add Comment

NEW YORK , Marekani.
Hatimaye Albam ya 14 iko tayari kutoka Baada ya Wiki Moja kuanzia sasa, na hatimaye kurudisha Hadhi na heshima ya Mariah Carey katika Muziki wa R&B.

Albamu hiyo ambayo itafahamika kwa Jina la ME. I AM MARIAH CAREY, inatarajiwa kuachiwa Mnamo May 27, huku ikiwa imeshirikisha Vichwa Mbali mbali katika Soko la Muziki Kimataifa, akiwemo NAS, MARY J. BLIDGE, FABULOUS na WALE.

Pia katika Suala Zima la Production, Mikono iliyosimama pale ni pamoja na Mkono wa JERMAIN DUPRI, HIT-BOY,RODNEY JERKINS na MIKE WILL MADE IT

Albam Hiyo ambayo unaweza kui-order hivi sasa kupitia I TUNES, imesheni Mikwaju kama Ifuatavyo





1. Cry.
2. Faded
3. Dedicated (feat. Nas)
4. #Beautiful (feat. Miguel)
5. Thirsty
6. Make It Look Good
7. You’re Mine (Eternal)
8. You Don’t Know What To Do (feat. Wale)
9. Supernatural
10. Meteorite
11. Camouflage
12. Money ($ * / …) (feat. Fabolous)
13. One More Try
14. Heavenly (No Ways Tired/Can’t Give Up Now)
15. It’s a Wrap (feat. Mary J. Blige)


Deluxe Version:
16. Betcha Gon’ Know (feat. R. Kelly)
17. The Art of Letting Go
18. Me. I Am Mariah…The Elusive Chanteuse

HATIMAYE CIARA AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME

7:10:00 AM Add Comment

LOS ANGELS, Marekani.
Kama Obama Land hawatosema  “Hayawi hayawai sasa yamekuwa”, kibongo Bongo inabidi Tuseme hivyo Tu, kama ambavyo TTM tumeweza kuinyaka

Finally Ciara hivi sasa anaingia katika jukumu Jingine Jipya kabisa baada ya kujifungua Mtoto wa kiume mapema Jumatatu ya Wiki hii
Ciara ambaye ujauzito wake umekuja kubainika Mnamo DECEMBER Mwaka jana kabla hata hajaweka wazi kama Kweli tayari ama lah, Hivi sasa yuko katika Furaha ya aina Yake na Mchumba wake Future ambaye ni rapper, Mtunzi, Muimbaji na Producer

Akizungumzia furaha Aliyonayo Ciara ambaye alikita na Kwaju la BODY PARTY, anasema hawezi kuielezea kiujumla, kwa sababu anaamini kila kitu kimeenda Vizuri, na anashukuru kamwe hakutamani kuishia Njiani katika safari yake ya kumpata motto wake.

Pia akielezea kuhusu Changamoto za Ujauzito wake, Ciara amesema kuwa, ujauzito huo haujampatia Changamoto ngumu yoyote, bali imekuwa Ni hatua Nzuri kwake, na umekuwa ni uzoefu Mzuri sana kwake.


Kupitia Account yake ya Instagram, Ciara amesema kuwa, mtoto wao amepewa Jina la FUTURE ZAHIR WILBURN, n hata hivyo Picha bado hazijaachiwa rasmi kunako Mitandao ya Kijamii, kasoro Tu, Mkono wa Kuchanga hicho amao uliachiwa na mama yake Ciara.

MNADA BANNER