REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HAKI YA MBONGOOO !!! : MKE WA T.I ADAI MUMEWE HAVAI VIATU VYA KUMFANYA AWE MREFU

3:20:00 AM Add Comment

Na Baba Juti. 
KAMA huwezi kumtetea Mumeo ama Boyfriend wako, basi usidhani wengine wanaweza kumkandia ama kuacha kumtetea. wako serious in love

Mke wa T.I, Tameka Harris maarufu kama Tinny, ameamua kuwatolea uvivu wale wote ambao wanamzunguimiza kuwa ni Kifupi Nyundo, na ndio maan hupenda kutengeneza urefu wake kwa kuweka baadhi ya vitu maalumu vya kumfanya aonekane mrefu hasa kupitia Viatu vyake

Sakata hilo lilianzaishwa na Wendy Williams maarufu kwa kuwakosoa watu maarufu Nchini humo, ikiwa ni baada ya yeye kuambiwa kuwa amepigwa Pasi.

Katika kulifafanua sasa suala Hilo, Mke wa T.I ameweka wazi kuwa, amekuwa akiishi na T.I kwa Miaka 16, lakini hajawahi kuona hivyo vifaa vya kurefusha kupitia Viatu, maarufu kama Shoes Lift, labda kama alikuwa anamficha.

Katika kukazia Zaidi, Tinny amedai kuwa T. I anajiamini akiwa yeye kama yeye na ukizingatia yeye ni mwanaume. Hivyo jalishi kama urefu wake ni kwenda juu au kwenda chini.

Na katika kuzungumzia Bifu la Mumewe na huyo Bi Mkubwa Wendy, alidai kuwa anatamani kabisa watu wasimuhusishe mumewe na Mabifu ya Kijinga ambayo hayana Faida kama Hayo

UBAGUZI NDIO BASI TENA!!!!?: ARIANA GRANDE AMTIMUA DANCER KIONGOZI WAKE KWA KUTUMIA NENO NI*****

2:38:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWa Mungu wenyewe mtatuambia kama hii adhabu iliyotolewa ilikuwa ni sawa ama ilikuwa ni ya kiuonevu

ARIANA GRANDE, ameamua kumfukuza kazi Dancer-Kiongozi wake kwa kitendo cha Kutumia N-WORD (NIGGA) kunako katika account yake ya mtandao wa Kijamii

Kwa mujibu wa Taarifa za kichini chini zinafafanua kuwa, uamuzi huo ulichukuliwa na Ariana kutokana na yeye kutokuruhusu suala lolote la kibaguzi katika Maisha yake na hata katika Kazi yake ya aina yoyote ile.

LADY CULTURAL ambaye inasemekana ni moja kati ya viungo muhimu sana katika Timu ya Ariana Grande hasa katika Upande wa Kucheza, aliandika neno hilo kama Caption katika Instagram Story yake, na hapo ndipo dude lilipoamshiwa

Kwa Upande wake Lady Cultural, aliamua kuweka wazi kile ambacho amekisikia, sasa kupitia instagram account hiyo hiyo, aliamua kujitetea kama ifuatavyo

"Kusema ninampenda huyu N***, haimaanishi kukufanya wewe uwe mbaguzi. Unatakiwa kuelewa kinachosemwa. Kama ningesema Ninawachukia Watu Weusi, hiyo ni Ubaguzi wa moja kwa moja. Ni Vitu viwili tofauti. Na kusema jina hilo ama neno hilo, haikufanyi kuwa mbaguzi. Binafsi sikubali maana mie sio mbaguzi. Hata Hivyo, Marafiki zangu weusi hawajaonesha kumaindi chochote. Wote wanapenda na kufurahia nikilitamka hilo neno"

MNADA BANNER