REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

JOSEE CHAMELEONE ANA HILI LINGINE

11:56:00 PM Add Comment

THE UG. Dance Hall Undefeatable, DR.JOSEE CHAMELEONE, ameongeza tattoo ya baba Yake Mzazi…

Lakini Pia kupitia ukurasa wake Wa facebook, Hiki ndicho alichokiandika

"YES!!!! Another one for you haters who hated on my "DANIELLA"tattoo. Ohoooooo!!!!!! I am an artiste, My body is becoming an art piece. Where I am deliberately Decorating my love.

 I am not going to wait for "Fathers"Day Mr.MAYANJA Senior-My Dad, you are worthy more than anything in this world, YOU grow me, know me, inspire me and all me. This one is for you!"

INSTAPIC: CHEKI KIM KARDASHIAN ALIVYONYODOLEWA INSTAGRAM

11:44:00 PM Add Comment

KIM KARDASHIAN alipost Vizuri Tu Picha ya Pete yake ya uchumba aliyovalishwa na Mchumba wake KANYE WEST ambaye Pia Ni mzazi mwezake.


Lakini kilichotokea katika Comment sasa, Duh.!!!!!!!

INSTAPIC: DAVIDO NA HUYU DADAA......KUNANINI?

11:34:00 PM Add Comment

PICHA HII..Ilipostiwa na DAVIDO Mwenyewe katika Account yake ya INSTAGRAM..lakini Ghafla, aliitoa haraka katika Account hiyo.


Sijafahamu kama ndo Shemeji yetu, maana Sijaelewa Chanzo cha Kuitoa haraka ni Nini

TUZO ZA KILIMANJARO ZIMEZINDULIWA

5:12:00 AM Add Comment


George Kavishe kutoka TBL ambao ndio Wadhamini wa tuzo hizi amesema

“‘Maboresho makubwa ambayo tumefanya mwaka huu ni tofauti na mara zote ambazo tumekua tukihusisha Watanzania dakika za kupiga kura tu hivyo wanakosa nafasi ya kupendekeza nani aingie kwenye category gani, mwaka huu tumebadilisha kutokana na matakwa ya soko hivyo Watanzania ndio watapendekeza nani aingizwe kwenye category gani. Kupitia Magazeti, website ya Kilimanjaro na vipeperushi kuanzia kesho February 18 2014 kutaonyeshwa category zote za mwaka huu za kupigiwa kura na Wananchi, Watanzania watatuma kura zao kupitia simu ya mkononi kupitia 15440, unapendekeza msanii, kikundi au producer gani aingie kwenye kipengele’’

‘’Kwa hiyo Mwaka huu Watanzania watapiga kura mara mbili ambapo ya kwanza ni nani aingie kwenye category alafu tutarudi tena kupiga kura nani awe mshindi wa kwanza, yani mwaka huu ile timu ya watu 100 ya Waandishi, Watangazaji na wadau wa muziki kuchagua nani na nani aingie kwenye category haitofanya hivyo bali itakutana kuhakikisha tu kama wimbo uliopendekezwa na Wananchi ni wa mwaka husika, uko sehemu husika na pia kama umekidhi vigezo vya kuingia KTMA’’ – Kavishe aliongeza

MABADILIKO KATIKA MWAKA HUU

Kwa mujibu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA), mabadiliko yaliyofanywa kwenye tuzo za mwaka huu wa 2014 ni kutokana na maoni na mapendekezo ya wadau wa tasnia ya muziki kutoa sababu mbalimbali.
Mwaka huu KTMA itakua na category 36 ambapo category 34 ni za kuchaguliwa na mbili zilizobaki ni zile maalum za kuteuliwa.
Mwaka 2013 kulikua na category 37 ambapo Mwaka huu imeondolewa moja kutokana na maoni mbalimbali ya wadau wa muziki ambapo category yenyewe ni Mtayarishaji chipukizi wa mwaka.
Category zilizobadilishwa majina mwaka huu 2014 ni Mtumbuizaji bora wa kike wa muziki badala ya msanii bora wa kike ilivyokua mwaka jana, mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki badala ya msanii bora wa kiume mwaka jana, mwimbaji bora wa kiume Taarab ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume Taarab.
Mwimbaji bora wa kiume bongofleva badala ya mwaka jana Msanii bora wa kiume bongofleva, mwimbaji bora kiume  band ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume band, mwimbaji bora wa kike bongofleva badala ya mwaka jana msanii bora wa kike bongofleva.
Mwimbaji bora wa kike Taarab badala ya mwaka jana msanii bora wa kike Taarab, mwimbaji bora wa kike band badala ya msanii bora wa kike band.

UPANDE WA BARAZA LA SANAA TANZANIA (BASATA)

BASATA katika maelezo yao, wamesema:

 ‘’kwa nini kumekua na mabadiliko haya? ukiangalia maana halisi ya neno Msanii linasadifu au linaleta maana za kuingia zaidi ya kitu kimoja, kunaweza kuwepo na msanii wa uchongaji, msanii wa Uchoraji n.k kwa sababu wanafanya kazi ya sanaa ndio maana tunatumia majina ya kimuziki kwa sababu huku tuko kwenye muziki’

PIA Wakaongeza ‘ ‘mwaka huu tutakua na video bora ya muziki ya mwaka badala ya video bora ya wimbo, neno muziki lina uwanja mpana kuliko wimbo…….. pia tutakua na wimbo bora wa Afropop badala ya wimbo bora wa bongopop, kutakua na wimbo bora wenye vionjo vya asili ya kitanzania badala ya wimbo bora wenye vionjo vya asili.Jingine ni Msanii bora chipukizi anaeibukia badala ya msanii bora anaechipukia…. wapo wasanii wengi sana chipukizi huko mtaani na miziki yao haijasikika, inawezekana amekaa miaka mingi akifanya kazi zake lakini akaibuka na ameonekana’’


HOW IT WAS: THIS IS HOW THEY SEEM TO BE HAPPY BAADA YA KUSPEND SOME TIMES KATIKA JIJI LA MWANZA. CINDY SANYU (UGANDA) & DAYNA NYANGE (TANZANIA)

4:29:00 AM Add Comment







THE FAST ONE FOR FIRST ONE : PICHA YA ELIZABETH "LULU" MICHAEL AKIWA MAHAKAMANI LEO,

4:21:00 AM Add Comment

MSANII WA FILAMU Nchini TANZANIA, ELIZABETH “LULU” MICHAEL , akiwa Mahakamani Kusikiliza Kesi yake, Dhidi ya Kifo cha Msanii Mwenzake wa Filamu, Marehemu STEVEN KANUMBA

MWANZA; MGOMO WA DALA DALA JIJINI MWANZA LEO

2:24:00 AM Add Comment

NA GEORGE BINAGI

MKUU WA (W) NYAMAGANA BARAKA KONISAGA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, MDA MFUPI BAADA YA KUKUTANA NA VIONGOZI MBALI MBALI WA SERIKALI, MADEREVA, NA WADAU WOTE WA USAFIRISHAKI JUU YA MGOMO WA DALADALA JIJINI MWANZA.


ZAIDI KIKAO KIMETOA WITO KWA MADEREVA KUSITISHA MGOMO MARA MOJA, AMBAPO AMESEMA KUWA AMEWAAGIZA WAHUSIKA WA JAMBO HILI KUFUATILIA SUALA HILI MARA MOJA IKIWA NI PAMOJA NA KUJUA NINI MALALAMIKO YA MADEREVA ILI YASHUGHULIKIWE HARAKA IWEZEKANAVYO.


ZAIDI UTASIKIA ALICHOKIONGEA KUPITIA 99.4 METRO FM.

TANGAZO RASMI KWA VYOMBO VYA HABARI

2:19:00 AM Add Comment


Uongozi wa Swahili Media Group unapenda kuufahamisha umma kuwa Alex Kassuwi sio mtendaji wala mkurugenzi katika kampuni hii na tunapenda kuwatahadharisha wadau wote  kuacha kuwasiliana  au kufanya mikataba  ya aina yeyote kwa jina la Swahili Media Group na  kampuni zake tanzu na Kassuwi kwani haitatambuliwa.Kuhusu taarifa potofu ambazo zimekuwa zikitolewa na aliyekuwa hisa  mwenza katika kampuni hii Bwana Alex Kassuwi.

Kwa mujibu wa kumbukumbu zetu, Alex Kassuwi sio mmiliki na hahusiki na uendeshaji wa Swahili Media Group kuanzia mwezi Januari 21, 2014 baada ya wanahisa na menejimenti  kumuondoa kwa maslahi ya kampuni hii ni baada ya  kumsimamisha tangu mwezi Octoba 2013 kutokana na ubadhilifu wa mali za kampuni ambao aliufanya akiwa mmoja wa wakurugenzi wa  Swahili Media Group.

Katika kikao hicho Bwana Alex alikiri kuiba mali za kampuni zenye thamani ya zaidi ya dola $15,000 na kuzipeleka kuweka rehani (Pawn Shop) bila ya idhini ya uongozi, alikubaliana na hukumu ya kusimamishwa katika nafasi ya menejimenti na kubakia mwana hisa tu.ushahidi wa nyaraka za wizi kutoka Pawn Shops na mazungumzo ya mkutano yalirekodiwa.

Januari 8,2014 Bwana Alex aliomba  arudishwe kwenye  menejimenti na uendeshaji wa siku kwa siku wa kampuni, kwa njia ya email baada ya jitihada zake za kuomba kwa njia ya simu na text kushindikana, menejimenti ilikataa ombi lake la kumrudisha kazini hasa ikizingatiwa kwamba  nafasi hiyo itaweza kumuweka karibu na vyombo vya ofisi ikiwemo vile  ambavyo aliviiba awali lakini alifahamishwa kuwa hisa zake zitaendelea kuwepo.

Januari 19,2014 Bwana  Alex aliomba kujiondoa rasmi kwenye kampuni kama mmoja wa wanahisa ombi ambalo lilikubaliwa rasmi Januari 21 baada ya kikao cha wanahisa na menejimenti kumkubalia.
Kwa taarifa hii, tunawaomba wadau wote kutambua  kuwa Alex Kassuwi sio mfanyakazi wala mkurugenzi na hivyo haruhusiwi kuisemea  wala kufanya  mikataba yeyote ya Swahili Media Group ikiwemo maidhinisho kwa niaba ya Swahili Media Group.
Uongozi wa Swahili Media Group unamtakia Mafanikio mema bwana Kassuwi popote aendako.

Uongozi Swahili
Media Group / Swahili Media International.



NEW VIDEO: MARIAH CAREY & TREY SONGZ “YOU’RE MINE (ETERNAL)”

1:58:00 AM Add Comment

TREY SONGZ HUYOOOOOOOO…ANAKUJA.

1:56:00 AM Add Comment

I CANT WAIT BUT HELP ndo Track ambayo ilimuweka Ulimwenguni Mkali wa Slow with Sweet Voice , Trey Songz.

Lakini kama ulikuwa hujui kuwa this Guy anajiandaa kulivaa soko la Muziki Duniani, Basii TTM tunakupa Mtonyo Kamili LikeThis…:


TREY SONGZ anakuja na Albam yake Mpya aliyoibatiza Jina la TRIGGA.
Trey amebainisha hilo pia wakati akizungumza na wanafunzi wa wanafunzi wa ERA HIGH huko BALTIMORE, katika Event yake ya kujitolea ya kutembelea Shule Mbali mbali na Kutoa Elimu ya Muziki na Maisha.


TREY alisema Kuwa, Albam hiyo ya TRIGGA itaachiwa Rasmi Mwezi wa JUNI Mwaka Huu 2014, tarehe 30

YMCMB KUMEIVA…..ALBAM COVER YA ALBAM YA MPYA IMEACHIWA.

1:49:00 AM Add Comment

KIU ya Kufahamu ujio Mzito wa The Hottest Crew, YOUNG MONEY CASH MONEY BROTHERS (YMCMB), bado inazidi kupamba Moto baada ya Wawili hao kuachia Albam Cover Yao pamoja na tarehe ya Kuachiwa kwa THE RISE OF AN EMPIRE

Baada ya TTM kuzisaka Updates za Mchakato huo, Tumeweza kubaini COVER hiyo ambayo imetawaliwa na rangi Nyekundu, Jina la Crew yaani YMCMB na Jina la ALBAM.

Aidha tarehe Rasmi ambayo Mzigo huo utaingia Sokoni Rasmi ni MARCH 11, Mwaka huu wa 2014.

Akizungumza kwa Niaba ya Kundi, COO wa YMCMB CORTEZ BRYANT amesema kuwa, Historia yao bado itazidi kuwa na Muendelezo wenye mafanikio, kwani itasheheni vitu amvyo haviishi Utamu katika Masikio 
ya fanzi na wapenzi wa Muziki waYMCMB

Pia Amesema bado wanaamini Vichwa Vipya Vilivyoingia vitakuwa balaa kama ilivyokuwa kwa DRAKE, NICKI MINAJ na TYGA

Mpaka Hivi sasa, Bado Uongozi haujaachia TRACKLIST ya Albam hiyo, lakini Track ya WE ALRIGHT ya LIL WAYNE, EURO na BIRDMAN itapatikana humo , na Video yake tayari ishaachiwa  

LIL WAYNE AWAONYA WALIMU WA SHULE……

1:44:00 AM Add Comment

KAMA Utakuwa Unakumbuka kipindi cha Nyuma, TTM tulikupa mtonyo kuwa Mwalimu Mmoja Huko FROLIDA, Nchini Marekani alipigwa SUNSPENSION baada ya Kubainika kuwa alimpatia Home Work Mwanafunzi wake wa Darasa la 8, yenye LYRICS za Track ya LIL WAYNE

Sasa baada ya Kusikilizia nini Kitakachotokea kwa Ticha huyo, KITENGO CHA CHIMBUA CHIMBUA kilibaini kuwa WEEZY F BABY alitoa onyo kwa walimu wote ambao wanatumia LYRICS zake kwa ajili ya Wanafunzi wao.

Akizungumza katika moja ya Interview Nchini marekani, Weezy alisema Kuwa, Si jambo jema kwa WALIMU kutumia wanafunzi LYRICS za Wimbo wake wowote kwa ajili ya matumizi ya Darasani.


WEEZY ameongeza kuwa, asilimia Kuwa ya Nyimbo zake, huwa Sio mahususi kwa ajili ya watoto na Watoto hawatakiwi kusikilza hata Kidogo, kwani hata maneno yaliyomo Humo hayaendani na hadhi yao.


Pia Weezy amesema kuwa, hatua aliyoifanya Mwalimu huyo haikuwa sahihi kabisa maana Huwa haandiki na Kurecord kwa ajili ya Watoto, bali huwa ni maalum kwa Fanz wake ambao ni watu wazima na wanaostahili kufahamu kile anachokisemakatika Nyimbo zake.

Katika kukazia hilo, Wayne aliongeza Kuwa Kuna tofauti kubwa kati ya KUSIKILIZA na KUSIKIA. Unapozungumzia KUSIKILIZA Moja kwa moja unazungumzia Kudhamiria, lakini KUSIKIA, unazungumzia kitu ambacho haujadhamiria lakini kimetokea tu.

Hivyo yeye huwa anaandika Kwa ajili ya watu wazima, labda ikatokea watoto wakasikia.

MNADA BANNER