REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

UKATILI: ALBINO AUAWA KIKATILI, HUKU WAWILI WAKIJERUHIWA

11:54:00 PM Add Comment

Na Vicky Ntetema
HALI ya wasiwasi imetanda miongoni mwa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) nchini, baada ya watu watatu kukatwa viungo na mmoja wao kuuawa mwezi huu.


Katika miaka ya hivi karibuni, jumla ya albino 72 wameuawa, 34 wamenusurika, wengi wao kwa kukatwa viungo au kuumizwa. Makaburi 15 yamefukuliwa na viungo kuchukuliwa na kumekuwa na majaribio manne ya kufukua makaburi.

Katika matukio ya hivi karibuni, walemavu hao wakazi wa Tabora na Sumbawanga wamekatwa mikono ya kushoto. Ukatili huo safari hii umekwenda kinyume na ilivyokuwa mwaka 2010-2011 wakati mikono ya kuume ndiyo iliyokuwa inakisiwa.
Aliyeuawa ni
Lugolola Bunzari (7) na waliojeruhiwa ni Mwigulu Matonange (10) na Maria Chambanenge (39).


Katika matukio hayo, mtoto mwenye umri wa miezi saba alinusurika kuuawa baada ya watu wasiojulikana kuvamia nyumba ya mama yake usiku katika eneo la Lamadi, Wilaya ya Busega, Mwanza siku moja baada ya kupokea ujumbe mfupi wa simu kwamba mtoto wake anawindwa.


Marehemu Lugolola
Kijiji cha Kanoge kina umbali wa takriban kilomita 75 kutoka Tabora Mjini, barabara iendayo Ulyankulu kwenye machimbo ya dhahabu.
Imenichukua saa mbili na nusu kufika huko. Saa moja na nusu kati ya hizo, nilizitumia katika safari ya kilomita 15 tu kutoka Kanoge makao makuu ya kijiji hadi Kitongoji cha Kinondoni alikouawa mtoto Lugolola.


Nyumbani kwa Bunzari niliwakuta ndugu na jamaa kutoka vijiji vya jirani vya Wilaya hiyo ya Kaliua, Tabora. Bibi mzaa baba wa Lugolola, Gama Zengabuyanda (60), ndiyo kwanza alikuwa amerejea kutoka Hospitali ya Mkoa ya Kitete alikokuwa akitibiwa baada ya kushambuliwa na majambazi alipotaka kumwokoa mjukuu wake.


Huku akilia kwa huzuni, Zengabuyanda alinisimulia jinsi mjukuu wake na baba yake mzazi, Zengabuyanda Meli (95) walivyouawa kikatili.


Katika muda wa kati ya saa 10 na 11 alfajiri ya kuamkia Februari Mosi mwaka huu, Lugolola aliuawa kikatili baada ya kukatwa mkono kwa panga, kukwanguliwa nywele, kujeruhiwa mkono wa kulia na sikioni na kuondolewa ngozi kwenye sehemu ya paji la uso.


Katika mashambulizi hayo, babu yake Meli pia aliuawa alipojaribu kumwokoa mjukuu wake. Vilevile baba yake mzazi, Bunzari Shinga alijeruhiwa wakati alipojaribu kumlinda mwanaye.
Nilimkuta mama mzazi wa Lugolola aitwaye Kulwa akisaidiana na ndugu zake kumenya maharage mabichi waliyoyatoa shambani mwao muda mfupi tu uliopita.


Yeye ni mke mkubwa wa Bunzari Shinga (35). Walibahatika kupata watoto sita, wawili kati yao ni albino. Lugolola na marehemu mdogo wake aitwaye Maganga aliyefariki kwa malaria mwaka 2011.


Usiku wa mashambulizi hayo, Kulwa anasema alikuwa amelala na watoto wake wadogo wa kike (mmoja, Shija mkubwa) na Lugolola kwenye nyumba yake inayotazamana na ile ya mke mwenzake Pili, umbali wa takriban mita 20. Bunzari alikuwa amelala kwa mke huyo mdogo na binti yao mwenye umri wa mwaka mmoja hivi.


Mzee Meli alikuwa amelala na watoto wa kiume upande wa kulia wa nyumba ya Kulwa.
“Aliamshwa usingizini na kelele za watoto waliokuwa wakilalamika kwamba wanapigwa na fimbo. Alipotaka kwenda chumbani kwa watoto alishambuliwa kwa mapanga kichwani, usoni, mgongoni, mikononi na miguuni,” Gama anaelezea huku akilia.

OFISI YA WAZIRI MKUU: TUMETOKELEZEYAAA!!!!

11:49:00 PM Add Comment

TUNAFURAHA: Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akifurahia jambo wakati wa mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi  Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh (kushoto) na Mkaguzi  Mkuu  wa hesabu za Serikali wa Sweden  Jan Lindahr Hjelmaker. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MNADA BANNER