REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MOUSTAPHA COLONEL KWA HUDDAH: KAMA SIYO CLASS YAKO KWANINI ULINIVULIA NGUO?

6:00:00 AM Add Comment

BAADA ya TTM Kukaa Chonjo kusikia kitakachozungumzwa na MOUSTAPHA COLONEL juu ya kumtumia Huddah na Jina lake ili kujipatia “Title” tena katika Game, Finally Yametimia.

Baada ya jana Huddah kukaririwa katika interview akimkana MUSTAPHA COLONEL ambaye hivi majuzi amekuwa akijitapa “Kubiringika” naye mara kadhaa katika “Uwanja wa Seremala”, bali alitaka kutumia Jina lake ili kujikomboa katika anguko baya la Kimuziki na Mishe nyinginezo.

Lakini baada ya kutafutwa azungumzie ishu hiyo, COLONEL naye hakusita “kumininika” na kutoa kauli ambayo ni Short and CLEAR -:

“Huo ni Uwongo. Kama Mtu hayuko class yako mbona mnapigaje ukiwa sindiria? Mboona hukupiga na watu wengine?”..alimaliza COLONEL MOUSTAPHA


ENHEE !!!...wacha tukae Chonjo tena !!!!!

YALE MAJEMBE YA ROCK CITY- TWEN'ZETU TUKANG'AE EMMY'S LAMODA

4:47:00 AM Add Comment










MWANZA IS THE BEST: MUZIKI WA MWANZA TUMEUSUSA, LAKINI MABINTI HAWA WANAHITAJI SUPPORT KATIKA AINA YA MUZIKI WANAOFANYA (R&B na ZOUK)

4:38:00 AM Add Comment

Nimebahatika kusikia Nyimbo tofauti sana za wasanii wengi wa kike kutoka jijini Mwanza. Tunashukuru wengine walitangulia katika mafanikio huku wakiibeba Heshima ya jiji Hili na Kuifikisha Sehemu Nzuri. Naweza kusema Ahsanteni sana.

Lakini hivi sasa Muziki umekuwa sana, na Vizazi vipya zinazidi Kuusukuma mpaka kuufikisha hapa ulipo.

Pasipo Kificho, Muziki wa Mwanza ni Mzuri sana, na kwa mtu yeyote anayeishi Mwanza, hakika hawezi kupingana na Hilo. Lakini kumekuwa na Changamoto kubwa sana ambayo inaukabili Muziki huu, na hata kufikia hatua ya kujenga “Ukuta” mkubwa baina ya mafanikio haya ya Muziki wa jiji hili, pamoja na soko kiujumla.

WAKAZI WA MWANZA wamekuwa ni sehemu kubwa ya kukwamisha maendeleo ya Muziki wa jiji hili tofauti na ilivyo katika JIJI la ARUSHA. Kuanzia kuusikiliza, kuufuatilia, kuusambaza na hata kuuandalia matamasha mbali mbali, vitu hivi vimekuwa ni historia kwa wasanii wa Mwanza na kazi zao. Ni sehemu chache sana hasa za Ndani, ambazo zimekuwa zikupa “Kik” Muziki huu, Mfano Mzuri ni UKEREWE.

Tofauti na Hilo, WADAU WA MUZIKI “FEKI” wamekuwa Wengi sana. Tukubali tukatae, Suala la “Menejimenti” Limekuwa ni tatizo kwa Mwanza Tu, bali hata Nchi nzima. Tumekuwa tukisikia wasanii kadhaa wakubwa wakilalamika Utapeli na ujinga unaofanywa na Wanaojiita mameneja, lakini Mwisho wa siku hakuna kinachofanyika katika kufaidika na Muziki wao. Tunakubali, ni vema kujitolea kumsaidia Msanii kuanzi kumsimamia katika kazi zake, lakini ukweli ni kwamba, mameneja hawa pamoja na Wadau wengine “feki” wanaongeza kila siku, na wanawatumia sana wasanii hasa hawa chipukizi ama wenye hamu ya kufanikisha kazi zao, kujinufaisha wao wenyewe.

UDHAMINI hasa katika matamasha, umekuwa kikwazo pia. Iko hivi, katika jiji la Mwanza, ukiandaa Tamasha (Shows, Events) ambazo zitawahusisha wasanii wa Mwanza tu, halafu ukaombe udhamini, Hesabu maumivu kabisa. Lakini ukiandaa tamasha ambalo litamuhusisha Diamond, Madee, Chege, na wengineo wengi tu, wenye majina, basi hapo utawapata unaowataka. Undhani hii itaufanya Muziki wa Mwanza ufikie pale unapotakiwa Kufika?

EMMY SANGO NA HONEYA…WANAHITAJI KUFIKA PAZURI.

  •   EMMY SANGO

Usinibanie Ndiyo Track ambayo Kiujumla ilimtambulisha Emmy katika Muziki wa Zouk hapa Mwanza, na hata kwingineko. Uwezo wake ulidhihirishwa na Track yake ya Pili inayofahamika kwa Jina La RADIO PRESENTER.
Kiufupi, Uwezo wake uko Vizuri sana, tangia nimeanza kumsikiliza, kuurudia mara kadhaa, kuwahusisha wenzangu, hakika anaweza kushindana na Wasnii wa kike kama akina linah, na Wengineo.


  •  HONEYA.

Infact, UWE WANGU, ndiyo Track yake ya Kwanza kaisa kurecord na hata Kuiachia. Ukiisikiliza kwa Umakini, unabaini kabisa kuwa bnti huyu anaimba kwa hisia sana, na anajua kipi ambacho anatakiwa kufanya katika “TOPIC” ya Wimbo anaouimba.
Sauti yake na mpangilio wa uimbaji wake, lazima utadhani amepitia “Training “ yoyote ya sauti, lakini nilipozungumza naye alisema hajawahi kupitia Training College yoyote hasa ya Sauti.
KWA MANTIKI HIYO, hebu tutafanye kitu kimoja. Sisi wasikilizaji, Wadau wa Muziki, watangazaji wa Redio mbali mbali kama Mie, Bloggers wote ambao tumejitambulisha ku-support Muziki wa Tanzania, tuwasikilize mabinti hawa, na tuwasukume. Ingawa ni kweli mapungufu yapo, lakini kupitia wewe, kila kitu kitakuwa ni funzo tosha kwao, na hatua nyingine nzuri zaidi kwao.

Mwanza is the Best


PATA NAFASI YA KUZISIKILIZA NYIMBO ZAO KWA UMAKINI

MFUNGWA AMBAKA MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI GEITA

3:11:00 AM Add Comment

Mfungwa wa gereza la Butundwe wilayani Geita mkoani Geita, mwenye amba 224/2013 Godfrey Selemani (19) anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa shule ya msingi Luhuha kata ya Nyakagomba wakati akichanja kuni porini.

Kamanda wa polisi mkoani Geita Bw. leonard Paul alisema kuwa tukio hilo lilitokea February 26, mwaka huu majira ya saa tisa ambapo mwanafunzi huyo jina limehifadhiwa anayesoma darasa la tano katika shule hiyo alipokuwa akichanja kuni na wenzake watano.

Wanafunzi hao wakisimuliatukio hilo walisema kuwa alipita mtu mmoja akiwa amevaa sare za wafungwa na baada ya muda mfupi mtu huyo alirudi akiwa amejipaka majivu kifuani huku akikimbia kuelekea walikokuwa wakichanja kuni.


Baada ya kuona hivyo alianza kukimbia kila mtu uelekeo wake na wakiwa wanapiga kelele zakuomba msaada na kwa bahati mbaye aFukire James alijikwaa  na kuanguka chini na ndipo mtuhumiwa alipomvamia na kumbaka.

Kwa upande wake mama wa binti huyo Bi. Pendo Mashauri alisemakuwa kitendo alichofanyiwa mtoto wake ni cha kinyama na kuomba serikali kumchukulia hatua kali mtuhumiwa huyo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Geita Bw. Adam Sijaona alithibitisha kumpokea mwanafunzi huyo Februari 27, mwaka huu na kumpatia matibabu.

Uchunguzi uliofanywana umebaini kwamba mfungwa huyo anatumikia kifungo cha miezi sita jela katika gereza la Butundwe.

CREDIT: BARUTI

JODIE WA KUCHI KUCHI: SINA UZOEFU NA MAPENZI

3:02:00 AM Add Comment

UNAWEZA Kujiuliza huyo mtoto alimpata wapi, lakini Swali hilo wala sina jibu, Ila Mtonyo uko hivi…

“MNAIJERIA” aliyelifanyia haki Vilivyo Kwaju lake la KUCHI KUCHI, JODIE ODIETE amevunjia ukimya swali aliloulizakuhusu Suala la mapenzi ama Ndoa kiujumla, wakati akipiga Moja ya Interview Nchini Nigeria.

Katika maelezo yake baada ya kuulizwa analichukuliaje suala la mapenzi Kiujumla, Jodie alikiri Kuwa kwa upande wake haoni kitu chochote cha Muhimu katika Suala Hilo, maana hana Uzoefu:

“Binafsi, silichukulii kiulazima kiasi hicho maana SIJAOLEWA, na haya ni mawazo yangu wala simgusi Mtu yeyote. Siwezi kuwa na Mtizamo wowote katika mapenzi kwa sababu kwanza sina UZOEFU na Kitu kinachoitwa mapenzi. Kwa maana hiyo, kufanya mapenzi,ama mapenzi kiujumla, si lolote si chochote kwangu, na ndiyo maana siwezi kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi kwa sababu hiyo.” Alisema Jodie..

Tofauti Na hilo, Bado Jodie alizidi “Kumiminika” baada ya kuulizwa kuhusu Mwanamme ambaye anamtamani na hata kumfikiri kuwa nae maishani, :


“Ninahitaji Mwanaume ambaye ni Rafiki yangu, ambaye atakuwepo kwa ajili yangu muda wowote. Ni ngumu sana kumpata mwanaume wa aina hiyo katika Dunia hii hatarishi. Hivyo kwa upande wangu ninahitaji Mwanaume rafiki ambaye kiujumla atajitolea kwa ajili yangu. Siwezi kusema anatakiwa awe Mrefu, mweusi, Mfupi, mnene, na mengineyo, bali ninahitaji Mwanaume ambaye ni rafiki wa Dhati”

MOZE RADIO WA GOODLIFE NCHINI UGANDA HATAKI MTU AINGILIE FAMILIA YAKE,….

2:58:00 AM Add Comment

KUNA mawili ya kuzungumzia kuhusu hili ambalo kama ulikuwa huklifahamu, basi TTM tumekutana nalo..

KUVUNJIKA KWA KUNDI LA GOODLIFE…
Awali zilivuma kuwa washkaji wawili wanaounda kundi la Goodlife, MOZEE RADIO na WEASEL wamemwagana Chini kutokana na tatizo ambalo lipo baina yao. Lakini wakati wakipiga Interview na Moja ya kituo cha TV nchini Humo, wawili hao walidai kuwa sio kweli, na wala hakuna tatizo katika kundi lao.

Tofauti na hilo , Moze radi aliongeza kuwa hivi sasa wanatarajia kushusha kwaju lao jipya ambalo wamelifanya wao kama wao wakiunda Kundi lao la GOOD LIFE

“Nina Magari mawili, Moze anayo Matatu. Hivyo muda mwingi huwa hatuko pamoja, na hicho Ndicho hao “Ng’ombe”(Wanahabari) wanakuwa wakiandika kuwa tumetengana. Hawana cha Kufanyaalisema

RADIO NA WEASEL KUMPA MIMBA LILIAN..

Katika Kujibu swali ambalo Moze Radio aliulizwa kuhusu wawili hao Kumpa Ujauzito Mwanamuziki wa Kundi la BLU 3, Lilian, kama ambavyo ilizagaa, Radio aling’aka kwa hasira akitoa Onyo kali la kuulizwa na Kufuatiliwa katika masuala yake ya kifamilia

“Hey Hey hey !!. Unaizungumzia familia yangu. Naomba usisemechochote kuhusu familia yangu. Sijawahi kumzungumzia Mama yako, Shangazi yako au baba yako, maana Siwafamu. Hivyo tafadhari, sahau kuhusu familia yangu”

Alifunga kila kitu Weasel



MALAYSIA AIRLINES:MWANAFUNZI WA TAIWANI ADAI SATELITE IMEONESHA PICHA YA NDEGE KATIKA POLI KUBWA LA THAILAND.

2:46:00 AM Add Comment

ZIMEPITA almost Siku 12 tangia kupotea kwa Ndege kubwa ya MALAYSIA AIRLINES, na bado jitihada za kuipata Ndege hiyo na Abiria wake hazijafanikiwa.

Lakini kwa mujibu wa taarifa iliyotufikia kuhusu mchakato huo, ni kwamba Mwanafunzi mmoja kutika Taiwan, amedai kupata Picha za satellite ambazo zinaonesha picha ya ndege ya Abiria ikikatisha Angani, katika pori kubwa la Nchi ya Thailand.


Hata hivyo bado uhakika Wa Picha hiyo haujawa rasmi na hata baadhi ya vielelezo vinapungua.


Aidha mamlaka ambayo inafuatilia kwa ukaribu Zoezi zima la Utafutwaji wa ndege hiyo, wamedai kuwa Siku Kadhaa zilizopita, baadhi ya wavuvi wanaopatikana Kusini mwa Mpaka wa Thailand, walisema kuwa Waliona Kitu kama Ndege iliyokatisha mitaa yao ikiwa katika Kasi Kali huku kukiwa na Muungurumo Mkubwa wa Engine, lakini baadaye haikusikika Tena

DUH….KANYE WEST HIVI SASA NI “MDOGO KAMA PILITON”

2:42:00 AM Add Comment

PENGINE ninaweza kusema ahsantee kwa mahakama iliyotoa adhabu kwa Rapa Kanye West kutoka nchini marekani, maana hivi sasa ameonekana kuwa mdogo na kujishusha kwa waandishi wa habari na hata wapiga Picha.

Akiwa amejifunika Kitambaa katika Eneo la Pua na Mdomo, Kanye alionekana kuwa Mpole katika Jiji la New York baada ya kufuatwa na Mpiga Picha na kuanza kumpiga Picha, bila kurusha Ngumi wala Teke.

Kwa mujibu wa Mtandao wa TMZ, baada ya Mpiga Picha wao kumuona Kanye akishuka ndani ya Gari, alinza kumfuata na kumrecord huku huku akimuuliza maswali kadhaa kuhusu Kesi na maamuzi ya mahakama yaliyotolewa siku chache zilizopita, lakini hakujibu Maswali hayo wala Kusukuma Ngumi kama ambavyo imezoeleka.

Kanye west amekuwa ni Msanii ambaye hapatani na wapiga Picha, kutokana na kuwapa kifinyo mara kadhaa na kuwatishia pindi wanapomsogelea na kumpiga Picha.


Kanye amepewa adhabu ya kuhudhuria Huduma ya Kupunguza hasira kwa Muda wa masaa 24 mapema leo hii, huku akitakiwa kufanya kazi za kijamii pamoja na Kuwa chini ya uangalizi wa mahakama ndani ya Miaka , baada ya kubainika na Kosa la Kumpiga Mpiga Picha Mmoja huko LOS ANGELS

UNAMKUMBUKA JOE?..ANASHUKA UGANDA

2:38:00 AM Add Comment

LONG TIME Sana hatujamsikia kunako Music Industr ulimwenguni, licha ya kufanya Vema kupitia Trax kama Vile ALL THE THINGS na STUTTER.

Lakini kama wewe ni Mkazi wa Uganda na Afrika mashariki kiujumla, Good News ni Kwamba, JOE anatarajiwa kushuka Nchini UGANDA kwa ajili ya Shughuli zake za kimuziki.


Stay Connected na Black touchez kupata mzuka Zaidi na kila kitakachoendelea

MNADA BANNER