REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

#SAYMYNAME: 5 ZA SHILOLE KATIKA HOVER BOARD... AMEPENDEZA?, AU KABOA?

8:32:00 AM Add Comment






MZAZI MWENZAKE NA AKA AMUWASHIA MOTO BABA HUYO WA MTOTO WAKE

8:24:00 AM Add Comment
DJ Zinhle, Mzazi Mwenzake na Ex wa Rapper AKA

Na baba Juti
MZAZI Mwenzake na Rapper A.K.A wa South Africa, DJ Zinhle amemwambia Rapper Huyo Kumheshimu

Kauli Hiyo ya Dj Zinle imetokana na Rapper A.K.A kulalamika kupitia Tweeter kuwa, amekuwa akinyimwa nafasi ya kumuona Binti Yake
Rapper AKA anadai kuwa, hapewi nafasi ya Kumuona Binti yake

Akijibu Mapigo ya Rpper Huyo, Bibie huyu ameandika kupitia account yake ya Twitter kuwa anahitaji kuheshimiwa kama mama wa Mtoto aliyezaa naye

Tizama Tweet Hizo:



SABABU YA SNOOP KUCHUKIA FILAMU HII YA UTUMWA

7:59:00 AM Add Comment
Rapper Snoop Doggy

Na Baba Juti
SNOOP DOGGY anaungana na Wengine Wengi ambao kwa asilim,ia kubwa, Sio Mashabiki wa Filamu zinazowaonesha Waafrica, na hata Wamarekani Weusi wakiwa katika Utumwa

Hii Imeweza kutokea siku za Hivi karibuni baada ya Snoopy Kuiona Filamu ya Historia ya Ukweli, inayofahamika kwa Jina la ROOTS, inayoonesha Masuala ya Utumwa hasa kwa Wamarekani Weusi.
Sehemu Ya Filamu ya ROOTS ambayo SNOOP haitaki na wala haikubali

Kinachomkwaza Snoopy, ni Kuona watu bado wanazidi kuonesha Ukatili tuliofanyiwa Mamia ya Melf na Maelfu ya Miaka Iliyopita, kitu ambacho si kibaya kwa Historia, lakini kwa asilimia kubwa kinadharirisha Ngozi Nyeusi.

Tofauti na Hilo, Snoopy anaamini kuwa, Kuonesha Historia Hizo hasa zenye Mateso makali, ni Kuzidi kuwapa Kichwa Wazungu waliotukandamiza, na hata kuhamasisha kitu hicho kuendelea mahali popote.

Pia Snoopy amekazia kuwa, Unyanyasaji wa aina hiyo nunaooneshwa katika Filamu hizo, bado unazidi kufanyika katika Baadhi ya Maeneo, hivyo hataki kabisa na hapendi mambo hayo yazidi Kutukuzwa

HAYA HAPA MAWILI KUHUSU SHAA: IKIWEMO KUHUSU RUNGU LA MAADILI

7:46:00 AM Add Comment
Shaa

Na Baba Juti
SARAH amaarufu Kama Shaa amezungumzia Experience yake ya Kukaa Kimya Katika Music Industry huku Rungu la Maadili likiwa ni Chanzo cha Yeye Kutokuachia Kazi zake.

Akizungumza Kuhusu Hilo, Shaa amedai kuwa, Ni Kweli amkaa Kimya kama Mwaka Mzima pasipo Kuachia kazi mpya, kitu ambacho kinaweza kikampelekea Shabiki kumsahau pia katika Music Industry

Tofauti na Hilo, Pia Shaa ameongeza Kuwa, Kilichomkwamisha zaidi ni Rungu la Maadili katika Kazi yake Mpya ya SAWA, ambayo angetakiwa kuiachia, lakini Video yake ambayo aliifanya na JUSTIN CAMPOS ilikuwa Nje Kidogo ya Maadili, hali ambayo ilimfanya apokee Ushauri na Kumrudishia Bwana Campos ili abadilishe na hivi sasa kila kitu kipo sawa.


NIMEKUCHOTEA HII KUHUSU ADHABU MPYA ALIYOPEWA MEEK MILL, NA SABABU ZAKE

1:56:00 AM Add Comment
Rapper Meek Mill

Na Baba Juti
RAPPER MEEK MILL alitakiwa Kumaliza Kifungo cha Nyumbani Siku ya Jana, lakini mambo yamekuwa tofauti baada ya kuongezewa Kifungo Kingine baada ya kukiuka Masharti ya Kipindi cha uangalizi.

Kwa Mujibu wa Mahakama, Meek Mill alikiuka Masharti ya Kifungo na adhabu ambayo alikuwa amepewa na Mahakama, ikiwemo kutokukamilisha Shughuli za Kijamii tofauti na namna ambavyo alitakiwa Kufanya.

Meek Mill aliongezewa Siku Nyingine 8 zaidi ikiwa ni kama Kufidia na Kuonya Kile ambacho alikuwa amekiuka.

Meek Mill alishindwa kufanya Shughuli za Kijamii katika Sehemu ambazo alikuwa amepangiwa, Siku 9 za kufanya Kazi za Kijamii na hasa kuwalenga zaidi wale Raia wasio na makazi

Kitu ambacho Meek anadaiwa kukifanya zaidi, ni kutumia Muda Mwingi akiwa katika Shule Tofauti, Kusaidia tatizo la Maji, na Kutoa Hotuba za Kuhamasisha
Kwa Mantiki Hiyo, Meek Mill alispend siku 6 Tu Kwa Wiki

UKO WAPI RIHANNA: DRAKE HIVI SASA KAHAMISHIA MAHABA KWA BINTI HUYU?

1:53:00 AM Add Comment
DRAKE

Na Baba Juti
MJINI kuna fununu Mpya kuhusiana na Mahaba mapya ambayo Rapper Kutoka YMCMB -Drake, licha ya kuhisiwa kuwqa karibu sana na Rihanna.

Katika Party la MEMORIAL ambalo Dreezy aliliandaa, wadakuzi walitilia shaka Ukaribu wa Mkali huyo wa HOTLINE BLING na Mwanamitindo mmoja Msexy hatari, HAILWEY BALDWIN.
Mwanamitindo Hailwey Baldwin anayedaiwa Kudate na Rapper DRAKE

Katika Party Hiyo, wawili hao walionekana katika Nyakati Tofauti toufauti wakionesha hali na hisia za Ukaribu, kitu ambacho kiliweza kuamsha hisia za watu Wengi kuwa, Huenda Drake tayari ameshaanza Mchezo wake wa kutaka kumdandia mwanamama huyo mwenye mafanikio zaidi katika "Mitindo Industry."

Tofauti na Hilo, Drake na Hailwey walionekana siku iliyofuata katika Moja ya Machimbo ya Bata, Huku Snap Chat ikihusioka kuonesha Ukaribu wao.
Mwanamitindo Hailwey Baldwin alidaiwa ku-date na Justin Bieber. Pia Justin Bieber anadai Kutokufurahiswa na Ukaribu wa Drake na Mrembo Huyo

hata hivyo, mpaka hivi sasa, Sio Drake, sio Hailwey ambao wamezungumza chochote kuhusu Mahusiano yao, Lakini Huyu atakuwa ni Mwanamke wa Pili Kudate naye, ikiwa ni baada ya Kudate na Msakata Tennisi Hatari kwa Upande wa wanawake, SERENA WILLIAMS.

MNADA BANNER