REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

JAY Z NA BEYONCE WAKO KATIKA DARASA LA NDOA……..

1:39:00 AM Add Comment
KAMA kuna watu waalikuwa bado hawaamini kuwa Ndoa ya Jay Z na Beyonce ina Tatizo tena Lisilo dogo…basi “Kalagabaho”..Kuna hili Jipya kabisa Kutoka TTM
Ukweli ni Kwamba, JAY Z na BEYONCE hivi sasa wanapokea Ushauri  Nasaha hasa kuhusu Ndoa yao, kwa Njia ya Mtandao…
Kwa Mujibu wa Full Info, ishu ni kwamba, wanandoa hao ambao kumekuwa na taarifa kadhaa kuwa Ndoa yao bado iko katika Mgogoro wa aina yake, wanapewa ushauri na mafunzo mbadala hasa kuhusu kuhimili changamoto ambazo zinawakabili, kutoka kwa mtaalam ambaye hutoa somo hilo kwa njia ya Mtandao wa Skype
Aidha Chanzo ambacho kipo karibu sana na Wanandoa hao, kimedai kuwa, Mtaalamu huyo wanamfahamu kwa Muda Mrefu, hivyo wanamuamini na huwa wanapata Somo la Nguvu Kila Week, ili kuweka Mahusiano yao sawa, na kuepuka  Mikwaruzano ya hapa na pale.
Tofauti na Hilo, pia inasemekana kuwa, wameamua kuhakikisha kwamba wanadumisha Furaha yaoa hasa katika Mahusiano, ukizingatia hawataki kuathiri hasa maisha ya Mtoto wao Blue Ivy

JAY Z na Beyonce walifunga Ndoa Mwaka 2008, huku Mikwaruzano ya Ndoa ikianza Mwaka huu hasa baada ya JAY Z kuzinguana na SOLANGE, ambaye ni Mdogo wake Beyonce.

UNAJUA NI KWANINI KANYE WEST HUWA HATAKI KUSUMBULIWA AKIWA AIRPORT?

1:33:00 AM Add Comment
KANYE WEST
Infact ni kweli kabisa kuna baadhi ya Watu huwa hawapendi kusumbuliwa hata kidogo wakiwa katika mazingira flani, sasa kuna hili ambalo huwa ni Kinyaa na Ugomvi kwa rapper Kanye West ambaye huwa hapendi kusumbuliwa akiwa Airport….
KITENGO CHIMBUA CHIMBUA kimeshusha Ripoti Kuwa, Baba North West himself huwa hapendi hata kidogo kusumbuliwa na Watu wa aina yeyote ile, hasa mapaparazi, maana huwa wanamfanya apate Stress na hasira sana, ukizingatia muda Wote huwa anafikiria Safari na Kufika Salama
Kanye West na Mkewe Kim Kardashian
Katika Upande Mwingine, Yeezy amedai kuwa, kinachomuudhi zaidi , ni maswali yasiyo na Mantiki yoyote kuhusu Yeye, huku wengi wakimuuliza kuwa kama kweli yeye ni Kanye West au Lah..

Katika Njia ambayo Rapper Huyu aliyetisha na POWER, huwa anaitumia ili kuepukana na Shida Hizo, basi ni kujifanya anaongea na Simu, ili watu wamuache, na kuepuka kumsumbua siku Zote.

HIKI NDICHO ALICHOKISEMA KARRUECHE, GIRLFRIEND WA CHRIS BROWN, KUHUSU RIHANNA

1:29:00 AM Add Comment

WENGI wanaweza kuwa na Maswali kuhusu Mahusiano ya koje kati ya Girlfriend wa sasa wa Chris Brown, KARRUECHE TRAN, na Ex-Girlfriend wa Brown, Rihanna, lakini TTM tushapata Mtonyo.

Akishuka kunako Moja ya Interview katika Kituo cha BET, Karrueche kwa mara ya Kwanza kabisa, amesema kuwa wengi huwa wanadhani yeye anachuana Vikali na Rihanna katika Kulifaidi Penzi la Breezy, lakini Kiukweli, anachuana mamilioniya Mashabiki wa Rihanna

Kaurrueche ambaye ni Mwana mitindo, anayemwagana na kurudiana na Mkali huyo wa Royal katika Suala zima la Mahusiano ya Kimapenzi, amedai kuwa kiujumla hiyo ni changamoto kubwa sana kwake, lakini amekuwa akijikaza ili kuyasukuma maisha yake ya Kawaida.


Tofauti na Hilo, Karrueche amedai kuwa, katika Maisha yake, hajawahi kuwa na Mahusiano na SUPER STAR yeyote Yule, hivyo kila kinachotokea, ni sehemu ya Changamoto katika Mahusiano yake

MNADA BANNER