REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

TAARIFA: KARDASHIAN AKIMBIZWA HOSPITALI BAADA YA KUDONDOKA

4:37:00 AM Add Comment
KWA UFUPI TU NI KWAMBA..........
MAMA KIJACHO Kim Kardashian ambaye mpia ni Mpenzi wa Rapper wa GOOD MUSIC, Kanye West amekimbizwa katika Hospitali ya Los Angeles maarufu L.A baada ya kudondoka, ikiwa ni baada ya Kutoka katika Fashion Show Nchini Ufaransa

HALI YAKE NA KICHANGA TUMBONI
Lakini Inabidi uondoe shaka kuhusu Yeye na Mtoto Mtarajiwa, maana inasemekana kuwa hali yao wote wawili ni SWALAMAAA



MAUAJI: MKWE AUAWA WAKATI AKIJARIBU KUFUATILIA MAHARI, TARIME

4:25:00 AM Add Comment
Kamanda wa Polisi wa Mkoa Maalum wa Tarime Rorya, JUSTUS KAMUGISHA


Na Samson Chacha, Tarime



MKAZI wa Kijiji cha Genkuru, Marwa George (38), anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa mkuki kwenye paja la kushoto na baba mkwe, John Mhabe (67).

Tukio hilo lilitokea juzi asubuhi katika Kijiji cha Kitawasi, anakoishi baba mkwe huyo, baada ya George kwenda kudai mahari aliyotoa ili kuoa kwenye nyumba hiyo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa Maalumu wa Tarime Rorya, Justus Kamugisha, alisema jana kuwa George alipooa, alitoa mahari ya ng’ombe 10.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Kamanda Kamugisha, miaka mitatu iliyopita, George alikimbiwa na mkewe huyo ambaye jina lake halijapatikana, kutokana na migogoro ya ndani, ambayo haikufafanuliwa na inasemekana, alikwenda Geita na kujiunga na wachimbaji wadogo wa dhahabu.

Alisema baada ya kukimbiwa na mkewe, George alikwenda kudai ng’ombe aliotoa kama mahari na alipofika nyumbani kwa baba mkwe, moja kwa moja aliingia zizini na kuchagua ng’ombe.

Inadaiwa alichagua mafahari watano na kuwatoa zizini ingawa baadhi ya mashuhuda wakati akiwatoa mafahari hao walimsihi kuacha kitendo hicho, lakini alikaidi na kuwaswaga kuelekea kwake.

Wakati akiondoka nao, inadaiwa baba mkwe alikasirika na kuchukua mkuki na kumchoma kwenye paja la kushoto na kumsababishia kuvuja damu nyingi na kufariki dunia.

Kamanda Kamugisha alisema Polisi inamshikilia mtuhumiwa huyo na baada ya mahojiano, anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya mauaji.

Tayari mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi na kuchukuliwa na ndugu zake kwa mazishi kijijini kwake Genkuru.

Kamanda Kamugisha alitaka wananchi kutojichukulia sheria mkononi, badala yake wafuate sheria na kupunguza hasira wakati wakitaka kuchukua uamuzi.

Aliwataka kama watashindwa kudhibiti hasira, washirikishe wana ndugu badala ya kujiamulia, ili kuepuka maafa kama hayo.

TAARIFA: ABSALOM KIBANDA AMEATHIRIKA SANA....

4:17:00 AM Add Comment

Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko, Halima Mlacha na Lucy Lyatuu



BAADA ya uchunguzi wa awali wa madaktari katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam kubaini kwamba Mhariri Mtendaji wa New Habari Corporation, Absalom Kibanda mbali na kujeruhiwa kichwani, kung’olewa meno, kucha na kukatwa kidole, zimebainika athari nyingine kwake.

Uchunguzi uliofanywa jana na madaktari wa Hospitali ya Milpark, Johannesburg, Afrika Kusini alikolazwa, umeonesha kuwa mbali na hayo, fizi kati ya pua na kinywa imekatika kutokana na nguvu na nyenzo walizotumia watesaji wake kumng’oa meno na kumsababishia maumivu makali.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena akikariri taarifa za Johannesburg, ilisema Kibanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa TEF, meno yake sita yamelegea.

Ilisema tangu awasili jana Milpark, amekuwa akiendelea na matibabu kwa maana ya kufanyiwa vipimo vikiwamo vya CT Scan na X Ray hasa kichwani na sehemu nyingine za mwili ambazo zilipata majeraha.

“Baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo, jopo la madaktari wenye ujuzi wa aina tofauti, walikuwa wakitarajiwa kukutana ili kusoma taarifa ya matokeo ya uchunguzi huo, ili kutafsiri maana ya matokeo hayo, kisha kutoa mwelekeo wa nini kinafuata au aina ya tiba anayopaswa kupata,” ilisema taarifa.

Jana uongozi wa Jukwaa la Habari za Kiuchunguzi la Afrika Kusini ulimtembelea Kibanda hospitalini Milpark na kueleza masikitiko yake kuhusu yaliyomkuta.

Waliahidi kushirikiana na taasisi za kihabari za Tanzania, kuchunguza tukio hilo kwa lengo la kupata majawabu ya nini kilichojiri na sababu za unyama huo.

Akizungumza na gazeti hili jana mchana, mke wa Kibanda, Angela Semaya alisema kwa mujibu wa muuguzi anayemshughulikia mumewe, walikuwa wakimsubiri daktari na wataalamu wengine ili kusoma vipimo kujua kiwango cha athari.

Alisema baada ya kusoma vipimo na kujua alivyoathirika ataanza matibabu ya jumla. Semaya alisema kwa sasa mumewe anaendelea vizuri kwani ana kumbukumbu zote, lakini mara nyingine analalamika maumivu sehemu alizojeruhiwa.

Kituo chalaani Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimesema kimepokea kwa mshituko na mshangao taarifa za kuvamiwa na kushambuliwa kwa Kibanda na kulaani wahusika na tukio hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kituo hicho, James Mbatia, aliliita tukio hilo kuwa ni ovu na la kiharamia lisilopaswa kuvumiliwa.

“Kikao chetu cha TCD kinatoa pole nyingi kwa ndugu wa Kibanda na kumwombea heri aweze kupona haraka ili aendelee na majukumu yake. Lakini pia tunalaani kwa nguvu zote tukio hili,” alisema Mbatia.

Alisema kituo hicho kinavitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo kwa haraka ili wahusika wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.

“Lakini tunasisitiza kuwa Serikali iwe makini zaidi kukomesha matukio ya namna hii ambayo yameanza kukithiri nchini, kwani yanajenga wasiwasi, chuki, uhasama na hasira miongoni mwa raia wa Tanzania na kuhatarisha usalama wa amani ya nchi yetu,” alisema.

Warioba azungumzia Naye Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji mstaafu Joseph Warioba alisema ni tukio linaloleta wasiwasi katika jamii na kutaka wananchi kushirikiana na Polisi katika kuyatokomeza.

Alisema tukio hilo linaonesha kuwa si la kijambazi ni kisasi cha kukomoana na ambayo yanaweza kuleta hatari kubwa katika jamii. “Tukio hili si la ujambazi ni la kulipiza kisasi cha kukomoana … yanatakiwa kudhibitiwa, kwani tofauti na hivyo yatakuwa hatari sana katika jamii,” alisema Warioba.

Kibanda alivamiwa saa sita usiku wa kuamkia juzi, nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake wakati akirejea nyumbani akitoka kazini na alitobolewa jicho, kung’olewa meno, kukatwa kidole cha mkono, kupigwa mapanga mguuni, kupigwa na nondo kichwani na mikononi ambapo wavamizi hawakuchukua chochote.

Kabla ya kusafirishwa nchini Afrika Kusini alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI).


PICHA: JUSTIN BIEBER AKIWA HOSPITALI, BAADA YA KUDONDOKA AKIWA KWENYE SHOW

4:03:00 AM Add Comment

THE RICH KID Justin Bieber alidondoka Back Stage alipokuwa katika Concert lililopigwa katika Ukumbi wa O2 Arena....

Baada ya Msala huo kumkumba bwana Mdogo huyo mwenye Mkwanja Mrefu, alipelekwa katika Chumba maalum na kupatiwa huduma ya Kwanza ya OXYGEN ili kuweza kumrudisha katika Hali yake ya Kawaida.

Aidha chanzo cha UDAKUZI kinadai kuwa, Bwana Mdogo huyo alishauriwa kupelekwa hospitali kwa ajili ya Check up na Matibabu zaidi, ila Mkali huyo wa Kibao cha BELIEVER na AS LONGER AS YOU LOVE ME aligoma na kudai kuwa yuko fiti na ataweza kumaliza Show yake ambayo alitakiwa aikamue katika Kumbi hilo

Baada ya kumaliza Show, JB alopelekwa hospitali na kupatiwa Matibabu...na hivi sasa yuko Pouwar bin Fit kabisa

PICHA: HUU NDIO MNATO WA UTUPU ALIOUPIGA JACKLINE PATRICK KWA AJILI YA JARIDA LA PLAYBOY

3:42:00 AM Add Comment

MNADA BANNER