REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

Meri Ya Mafuta Yaripuka NIGERIA

Meri Ya Mafuta Yaripuka NIGERIA

5:15:00 AM Add Comment
KIMATAIFA
Taarifa kutoka Nigeria zinasema watu kama kumi wamekufa kwenye moto uliotokea kwenye meli iliyobeba mafuta, kwenye bandari ya Port Harcourt.
Matangi ya mafuta nchini Nigeria
Inaarifiwa moto huo ulisababishwa na cheche za moto kutoka ukarabati uliokuwa ukifanywa.
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema baadhi ya watu waliorushwa majini na mripuko huo, walinusurika, lakini wengi wengine walinasa ndani wa meli.
Inadaiwa wazima moto hawakuweza kufikia meli hiyo, kwa sababu mipira ya maji ilikuwa mifupi.

Sudani Kusini yafuta Mazungumzo ya Amani na Sudani Kaskazini

5:12:00 AM Add Comment
Sudan kusini imefutilia mbali mazungumzo ya amani yaliokuwa yafanyike kati yake na Sudan Kaskazini huku ikiishutumu nchi hiyo kwa kushambulia moja ya miji yake karibu na mpakani. 
Msemaji wa jeshi Kanali Philip Aguer jana alisema kulikuwa na shambulizi la bomu katika eneo la Rubaker. 
Aguer alisema mabomu takriban manane yalirushwa katika eneo hilo na ndege za kijeshi za Sudan na kuwajeruhi watu wawili. 
                                                   Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir

 Mzozo wa mafuta na maswala ya mipaka kati ya nchi hizo mbili umendelea baada ya Sudan Kusini kujitenga na Sudan mwaka mmoja uliopita. Habari hii ya mashambulizi inakuja takriban wiki mbili baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhimiza mataifa hayo mawili kusuluhisha tofauti zao  kabla ya tarehe 2 Agosti ambao ndio muda wa mwisho uliowekwa na umoja huo kwa mataifa hayo kuelewana.

MNADA BANNER