REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MUNGUA OKOA JAHAZI !!!!! : WABUNGE NCHINI KENYA WALALAMIKA KUTUMIWA PICHA ZA UTUPU

3:26:00 AM Add Comment

Na Joe Mwangi  
INAWEZEKANA kabisa baadaye mambo ya Mitandao na hata matumizi yake Nchini Kenya, yaakanza kubanwa vilivyo kama ambavyo inafanyika Nchini Tanzania, na hii itakuwa Very Soon

Hii inatokana na hatua ambayo imeonekana kuwa "Chungu Kumeza" na haitoweza kuvumilika baada ya binti mmoja Nchini humo kufanya jambo "korofi " kidogo kwa Waheshimiwa Wabunge, bila kujali kuwa wao ndio wanaotunga Sheria

Wakiwa Bungeni, Baadhi ya Wabunge wa Kiume wameamua kutoa Malalamiko yao ya kutumiwa picha za Utupu kabisa kutoka kwa binti ambaye hajafahamika, kitu ambacho kimeonekana kuwasumbua na kuwakwaza kwa asilimia kubwa.

Mmoja wa wabunge alisimama na kutoa lawama zake kuwa inaonekana binti huyo anazo namba za wabunge wote wa kiume, na huamua kutuma Picha za Utupu ili kuwatega na hata kuwarubuni kitu ambacho hakistahimiliki kwa upande wao

Aidha mbunge mwingine alisimama na kusema kuwa, kwa mara ya kwanza alipotumiwa picha hizo na kuzifungua, ilimuwia vigumu sana kuendelea kuzitazama, na akasema pia kama akimpatia Mheshimiwa Spika azione, hawezi kuzitizama kwa macho hivi hivi, lazima awe amevaa kifaa maalumu ili kuona kama atapunguza makali


Ukiachilia mbali Mbunge huyo, mwingine alisimama na kudai kuwa, picha hizo zinazotumwa na binti huyo zilipoingia katika simu yake, zilileta mgogoro mkubwa sana katika Familia yake

Wabunge hao wameomba kuwa, iwapo utaletwa muswada bungeni kuhusu Sheria ya Makosa ya kimitandao basi ni vema wakashirikiana kuuweka sawa na kutilia mkazo zaidi katika makosa kama hayo ili kuepusha mengi sana

MWANAMKE ALIYEPIGWA NA MSANII TREY SONGS AKIRI KUWA, WATU WALIKUWA WAMESIMAMA WAKATI ANAPEWA KIFINYO NA HAWAKUTOA MSAADA WOWOTE

2:08:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
HATIMAYE Mwanamke ambaye alifungua Mashtaka dhidi ya Msanii Trey Songs kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi hadharani kisa  kaongea na mwanaume mwingine , ameamua kuweka wazi na kuanika namna ambavyo amejeruhiwa na Msanii huyo

Awali tulitoa Taarifa kuwa Trey Songs alifunguliwa mashtaka na Bibie ANDREA BUERA kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi katika upande wa Parking walipokuwa wakitoka kula bata, huku tatizo kubwa likiwa ni bibie huyo kuongea na mwanaume, yaani kwa tafsiri ya Fasta ni kwamba, kulikuwa na Ishu ya WIVU

Akiwa na mwanasheria wake, Andrea aliweka wazi maeneo ambayo amejeruhiwa FEBRUARY 18 wakati wanatoka kunako After Party ya NBA ALL STARS WEEKEND na kudai kuwa ameamua kujitokeza mbele ya umma kuweka wazi kilichotokea ili uwe mfano bora hata kwa binti yake ambaye ana umri wa miaka 7

Katika Maelezo yake huku akitokwa na machozi, Andrea ambaye alikuwa ameambatana na Mwanasheria wake LISA BLOOM alizungumza haya, tunamnukuu

" Nilikuwa nimehudhuria After Party hiyo na ndipo Trey alianza kunifokea, kunikaba na kunipiga mitama na kunipiga ngumi na hata kunipiga mpaka nikaanguka Chini."

Kitu kilichoonesha kumuuma zaidi, ni namna ambavyo watu walishindwa kutoa msaada kwake wakati zoezi zima la kipigo kutoka kwa HIT MAKER huyo wa BOTTOMS UP linaendelea, tunamnukuu tena

"Watu walikuwa wamesimama tu na wanatazama namna ambavyo ninapewa kipigo. Nilipoona hali imekuwa mbaya, nilichukua simu nimpigie mtu wa usafiri aje kunichukua, lakini alichukua simu yangu na kuipiga chini, halafu akachukua na simu yangu nyingine akafanya hivyo hivyo. Nililia sana katika Mshtuko mkubwa na nilitaka kwenda nyumbani

Nilijitahidi sana kwenda hosiptali kwa sababu aliniumiza sana, na hata nilipoamka usiku wa manane, bado nilikuwa nasumbuliwa na kumbu kumbu za ajabu na tukio lile"



MAKUBWA !!!: MTUHUMIWA WA KOSA LA UDHALILISHAJI KWA MWANAMKE KWA KUMSHIKA SEHEMU ZAKE NYETI AACHIWA HURU...KISA?

1:36:00 AM Add Comment

Na Joe Mwangi-KENYA
IMAGINE wewe ni Binti na umefanyiwa jambo la "Udhalilishaji" na mtu tena mbele ya kadamnasi, halafu hukumu inayotoka ni kwamba jamaa alokufanyia hivyo hana hatia....utajiskiaje?

Kutoka Nchini Kenya, Ndugu yetu anayetambulika kwa jina la ALEXANDER MBONDO, alifunguliwa mashtaka na binti mmoja (jina limefichwa) ya kudhalilishwa hadharani mnamo Mwezi April na September 2016 katika Jengo la FONTANELLA huko Mombasa tena kwa makusudi kabisa

Kwa mujibu wa Mlalamikaji, inasemekana kuwa, Bwana Alexander alimkamata Sehemu Za "Makalio na Matiti" mbele ya umati wa watu katika mazingira tofauti, kwanza ilikuwa ni Ndani ya Basi na mara ya Pili ilikuwa ni katika Duka ambalo linapatikana katika maeneo hayo, na jamaa alikamatwa baada ya binti huyo kupiga kelele

Akijibu tuhuma hizo, Alexander ambaye ni mtuhumiwa, alikana kumshika mwanamke huyo katika sehemu zake Hizo nyeti, ila akaiambia mahakama kuwa uzuri wa mwanamke huyo umekuwa ukimchanganya mpaka kufikia hatua ya kuanza kumtongoza ili awe Mke wake, lakini bibie alikuwa akigoma kwa asilimia kubwa

Tunamnukuu:
"Ninampenda Mwanamke huyu mpaka nahisi kufa, na siwezi kujizuia kumpenda kwa sababu ya Urembo alio nao. Niko Tayari kumuoa muda wowote endapo atakubali ombi langu la muda Mrefu"

Kauli hiyo ya Mbondo iliiacha mahakama Katika Butwaa, ukizingatia alishakaa mahakamani tangu mwaka 2016 kwa kukosa dhamana ya Shilingi za kenya 20,000

Katika Kujazia zaidi, Mtuhumiwa aliiomba Mahakama na kudai kuwa itakuwa haijamtendea haki kumhukumu kifungo chochote kwa kumtongoza mwanamke anayempenda, maana alichokionesha ni Hisia

Tunamnukuu
"Ninaiomba Mahakama iniachie Huru , ili niweze kutimiza azma yangu ya kumuoa mwanamke ambaye ni Pendo la Maisha yangu"

Baada ya kusikiliza kesi hiyo, Hakimu aliyekabidhiwa kesi hiyo, HENRY NYANKWEBA alidai kuwa, upande wa mlalamikaji haukutoa Ushahidi wa kutosha kuhusu kudhalilishwa kwa mwanamke huyo, hivyo akaamua kumuachia Huru Bwana Alexander Mbondo


MNADA BANNER