REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PETER MSECHU NA BABA LEVO WANAPOMLILIA RUGE...KUHUSU KUKOSA CHANCE YA KUPERFORM FIESTA

8:24:00 AM Add Comment


INSTACOP: HIVI NDIVYO WALIVYOMVAA DIVA LOVENESS LOVE WA CLOUDS FM, KUHUSU WEAVING LAKE

8:17:00 AM Add Comment



DAVIDO...

8:12:00 AM Add Comment


UGONJWA wa EBOLA umemgusa Super Artist Kutoka Nchini Nigeria, DAVIDO, kushiriki katika Mchakato ambao unaendelea Hivi sasa katika mitandao ya Kijamii , unaofahamika kwa Jina la ICE BUCKET CHALLENGE, yaani Kujimwagia Maji ya Barafu.

Aidha , baada ya davido kupendekezwa kuingia katika Challenge Hiyo, na Producer Don Jazzy , Basi hakutia Ngumu wala kupingana nayo, bali alifanya Hivyo na Kumwagiwa maji hayo yenye Barafu.

Kupitia account yake ya Instagram, Davido amepost Video Hiyo, na Kutoa Kiasi cha Dolari za Kimarekani 100 kwenda katika Account ya ALS FOUNDATION, ambayo ndiyo inayoguswa zaidi katika Kupata Mchango huo wa Fedha kutoka kwa watu mbakli mbali Ulimwenguni, na Kusaidia walengwa ambao kamwe hawajiwezi.

Tofauti na Hilo, Pia Davido amewataja watu tofauti kushiriki, akiwemo 2 FACE IDIBIA, na Wengineo.

ICE BUCKET CHALLENGE, ni Mchakato ambao umekuwa ukichukua nafasi kubwa sana katika Mitandao mbali mbali ya Kijamii, hasa Instagram, ambapo Mtu anayetajwa kushiriki, basi hana budi kushiriki kwa Kumwagiwa ama kujimwagia Ndoo ya Maji yenye Barafu na kuchangia kiasi Kadhaa


Mpaka Kufika AUGUST  18, Kiwango cha Fedha ambacho kilikuwa kimeshakusanywa kutokana na Mchezo huo ni USD MILION 15.6, na watu ambao wameshashiriki katika Mchezo huo, ni kama Vile CRISTIANO RONALDO, LADY GAGA, JUSTIN BIEBER, ICE PRINCE, DON JAZZY, OPRAH WINFREY, LEBRON JAMES, BILLIONEA BILL GATES, MACLEMORE, MMILIKI WA FACE BOOK MARK ZUCKERBERG, SELENA GOMEZ, JUSTIN TIMBERLAKE, na wengineo Kibao.

KIDUDU MCHEPUKO ETI KIMEINGIA KATIKA NDOA YA MARIAH CAREY

7:53:00 AM Add Comment


KUNA tetesi ambazo zimeanza kuzagaa kuwa Nick Cannon na Mkewe Mariah Carey wameshaingiliwa na Kidudu Mchepuko, hali ambayo inaweza kuleta athari kubwa katika Ndoa yao.

Kitengo Chimbua Chiombua, kimenyaka Mchakato Mgumu kweli kuutabiri, na kudai kuwa, kumekuwa na Ugomvi wa hapa na pale baina ya wanandoa hao wawili huku sababu ikiwa ni tuhuma za kuchepuka zinazomkabili Nick Cannon.

Aidha Mtonyo haujaishia hapo tu, pia inasemekana Nick Cannon hivi sasa amehamishia Maskani ya Muda, katika Hotel moja hivi ambayo bado hatujalinyaka Jina

Tofauti na Hilo, Pia Kuna mmoja wa Ndugu wa karibu kwa wanandoa hao, ambaye alidai kuwa, Mariah carey amechoshwa na Suala la Mchepuko ambalo mara Nyingi  amekuwa akilifanya Nick Cannon, hali ambayo imemfanya amuwekee walinzi ambao watazuia warembo wote wanaomsogelea Nick, hali ambayo ilidhihirika Katika POOL  

PARTY  moja iliyofanyika Las Vegas, huku Nick Cannon akiwa ni MC wa Shughuli hiyo.


Mariah na Nick walifunga ndoa mwaka 2008, na Mpaka Hivi sasa bado wanamaisha yao katika Ndoa Hiyo, licha ya Mariah Carey kutokufanya Vizuri katika Muziki kama ilivyokuwa awali.

BUSTED: JENIFFER LOPEZ NA KISERENGETI BOY CHAKE WAMERUDIANA.

7:38:00 AM Add Comment

MAREKANI....
WANASEMAGA penzi ni kikohozi na kulificha kamwe huwezi hata siku moja..sasa chukua hii hapa..

JENNIFER LOPEZ inawezekana kabisa akawa amerejesha mahba yake niue kwa Kiserengeti boy chake, Casper Smart

Siku ya Jumatatu mapema, JLo pamoja na Casper Smart walikamatika na camera za Wadaku wakiwa Ndani ya gari ambalo linalosadikika kuwa ni la Jennifer Lopez.

Hata Hivyo basi, baada ya Mwanamama Jennifer kubaini kuwa, kuna wakali wa Maudaku wanawafuatilia na Kuwadungua mafoto kadhaa, basi alijificha kwa Kuinama ndani ya gari hilo, lakini kiserengeti Boy 
Chake casper Smart, kikibaki kawaida, sababu ndiye alikuwa anaendesha Gari.


JLO na Smart walipigana Chini Mwezi Juni, huku lawama zikiangukia kwa Casper Smart kuwa amekuwa akichepuka na Mtu ambaye alibadili Jinsia, jambo ambalo alipingana nalo huku akiahidi kufungua mashtaka kwa yeyote anayeanzisha mastor Hizo

MNADA BANNER