REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MISRI : Msafara wa Waziri Mkuu washambuliwa

11:28:00 PM Add Comment

Waziri Mkuu wa Misri Hisham Qandil, amenusurika kifo baada ya mtu mmoja mwenye silaha kuushambulia msafara wake.

Tukio hilo lilijiri baada ya mtu mmoja aliyekuwa na silaha kuushambulia kwa risasi msafara wa Qandil, katika viunga vya mji mkuu Cairo. Kwa mujibu wa polisi ya Misri, waziri mkuu huyo hakuathirika katika shambulizi hilo.

 Aidha polisi imetangaza kuwa, imefanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa wa shambulizi hilo na kwamba, tukio hilo halina uhusiano wowote na masuala ya kisiasa. Wakati huohuo serikali ya Misri na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwa pamoja, zimelaani chokochoko na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni nchini Syria.

Serikali ya Misri na Arab League jana zililaani mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni huko Syria na kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua kali kuhusiana na suala hilo.

SYRIA:20 wauawa kwa mashambulizi ya magaidi

11:18:00 PM Add Comment

Watu 20 wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya magaidi yaliyotokea katika maeneo tofauti nchini Syria.

Mauaji hayo yamejiri katika mashambulizi ya mabomu ya kutupwa kwa mkono yaliyotokea katika maeneo ya Kafr Nabl mkoani Idlib na Al-Zahraa katika mkoa wa Aleppo nchini humo ambapo pia watu wengine kadhaa wamejeruhiwa vibaya.

Kabla ya hapo Wizara ya Ulinzi ya Syria ilikuwa imetangaza pia habari ya kuuawa kamanda mkuu katika uwanja wa ndege wa kijeshi katika viunga vya mkoa wa Aleppo kaskazini mwa nchi hiyo. Wakati huo huo, muungano wa wapinzani wa serikali ya Damascus, wamelaani vikali mashambulizi ya hapo jana ya utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya nchi hiyo.

Katika ripoti iliyosambazwa hapo jana, wapinzani hao pia wamelaani hatua ya Israel ya kutumia vibaya matukio yanayojiri hivi sasa nchini humo kutekeleza mashambulizi dhidi ya Syria na kwamba hatua hiyo haikubaliki.

Aidha muungano huo, umeyataja mashambulizi ya Wazayuni nchini Syria kuwa yanayofanyika kwa malengo maalumu yaliyo nyuma ya pazia.

NIGERIA: Watu 10 wauawa mashariki mwa Nigeria

11:15:00 PM Add Comment

Polisi ya Nigeria imetangaza habari ya kuuliwa watu 10 huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Polisi hiyo imetangaza kuwa, mauaji hayo yalijiri hapo jana baada ya kundi moja la watu wenye silaha kukishambulia kijiji cha Njilang katika mkoa wa Adamawa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Watu tisa wengine wamejeruhiwa katika shambulizi hilo. Mashambulizi ya kijiji cha Njilang ni katika mfululizo wa mashambulizi yanayoendelea dhidi ya maeneo ya mpakani kati ya Nigeria na Cameroon. Baada ya watu wenye silaha kutekeleza shambulio hilo, walikimbilia nchini Cameroon.


 Siku ya Ijumaa Martin Nesirky Msemaji wa Umoja wa Mataifa alitangaza kuwa, watetezi wa haki za binaadamu wana wasiwasi mkubwa kutokana na kuendelea kwa machafuko huko kaskazini mashariki mwa Nigeria, machafuko ambayo yamekuwa yakisababisha mauaji na majeraha kwa raia wa kawaida.

MNADA BANNER