REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

NEW TRACK : NGORI - Kisu Kikali ( Produced By P-SILLA -Acute Music) -VERY HOT !!

2:36:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Another New Talent Kutoka Jiji La Miamba (ROCK CITY) Mwanza. Anaitwa KISU KIKALI, na Mkwaju wake Unaitwa "NGORI".

Production imefanyika Jijini Mwanza, chini ya Producer P-Silla. Unaweza Kuiskiliza na Kuidownload Moja kwa Moja


KIMENUKA !!! : RAPPERS WA KIKE WAWILI WAKIRI KUWA WALILIPWA MAMILIONI YA FEDHA ILI WATENGENEZE BIFU NA NICKI MINAJ ( VIDEO)

2:05:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu Kimenuka Si Kitoto, na hii inaweza kuwafanya watu waanzae kuelewa ama kuhisi tofauti hasa kile kinachoendelea katika Game la Muziki

Record label ya Nicki Minaj inadaiwa kuwalipa Rappers wa Kike wawili USD 250,000 ili watengeneze Bifu na Nicki Minaj


Kwa Mujibu wa Info ambayo Tuko nayo mpaka hivi sasa, ni kwamba Rapper wa Kike wa Kwanza, anayefahamika kwa jina la LADY LESHURR aliweka wazi kuwa Atlantic Records ambayo inamiliki Warner Record ambayo ndiyo Minaj amesainiwa Hivi karibuni, ilimuita na kukaa naye mezani, wakimuahidi kitita Hicho cha Fedha, ili atengeneze "Bifu" na Nicki Minaj
Sasa Baada ya kuibuka Suala hilo, alijitokeza Bibie Mwingine ambaye ni Rapper pia, anayefahamika kwa jina la Queen ElizaBitch na kudai kuwa nayeye alishawahi kuitwa ili afanye Hivyo
kupitia Twitter account Yake, Queen ElizaBitch aliandika Hivi

"Yah, ninakumbuka Nilikaa nao pia, ila nikapiga Chini maana niliamini katika siku hizi, msanii anaweza akazitengeneza hizo USD 250,000 mwenyewe kwa nguvu zake"

Hata Hivyo Nicki Minaj alijitokeza na kukanusha Madai hayo kupitia Instagram account yake

R.I.P PRODIGY : 50 CENTS- "WALIMUAMURU P ANICHOME LAKINI HAKUFANYA HIVYO

1:29:00 AM Add Comment

Na Baba Juti.  
#WatuWaMungu Siku Ya Jana , Jamii ya Hip Hop ilikumbwa na Majonzi Mazito baada ya kumpoteza mmoja kati ya Members ambao wanaunda kundi la Mob Deep ALBERT JOHNSPN a.k.a PRODIGY

Taarifa ambazo Team Hit Zone tulizipata Siku ya Jana, zinadai kuwa Rapper huyo ambaye amefariki akiwa na Umri wa Miaka 42, alikutwa akiwa amefariki Nyumbani kwake huku sababu ama chanzo kikiwa hakijabainika mpaka Hivi sasa

Lakini kwa Taarifa ambazo tuko nazo mpaka Hivi sasa, ni kwamba Prodigy alikuwa akisumbuliwa na Tatizo la Sickle Cell Anemia siku chache Zilizopita, na kulazwa Hospital baada ya Perfomance yake huko LAS VEGAS, Marekani

Tatizo hilo limekuwa Likimsumbua tangu amezaliwa, na amekuwa akifanya Juu Chini ili kusurvive katika Maisha Yake ya Kila Siku

50 CENTS: PRODIGY ALINILINDA SANA !   
Mwaka 2005, Mobb Deep walisain Mkataba na G UNIT na kuanza kufanya Kazi pamoja. Mkwaju wa OUTTA CONTROL (Remix) wakiwa na 50 Cents ndio uliowafanya wathibitishe Uwezo wao

Siku Hiyo hiyo ya Jana, 50 Cents alilazimika kuondoka katika Tuzo za GOLDEN NYMPH (Golden Nymph Academy Awards 57) baada ya kupata Taarifa Hizo, huku akiandika Mengi kuhusu Yeye.

Katika Hatua ya Kwanza, 50 Cents aliandika Hivi:
"Police walijitahidi kumtumia P ili wanikamate. Walimuuliza kama nilikuwa ninamiliki silaha ama Dawa za Kulevya. Kisha walimuamuru  aweke Bunduki katika Gari langu . hakufanya Hivyo, na badala yake aliniambia kila kitu ambacho walikuwa wanajaribu kufanya."

katika hatua Nyingine, Hit Maker huyo wa In Da Club aliandika hivi
"Pumzika kwa amani Prodigy, utapendwa na kukumbukwa Milele. Mungu akubariki na Familia yako. Nimekosa maneno ya kuzungumza. ilinilazimu kuondoka katika sherehe za Tuzo"


MNADA BANNER