REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

USWAZI-TAKE –AWAY: MWENYEKITI MSTAAFU..TAFADHARI TUHESHIMIANE…KINYESI CHAKO HUKOOOO

4:43:00 AM Add Comment







WIKI hii nzima, UTA (Uswaz-Take-Away) inajikita katika Mtaa wa BUGARIKA hapa Jijini Mwanza, sasa leo nina Hili.

Katika Mtaa huo Husika, kuna Mwenyekiti wa Mtaa Mstaafu (Jina Kinywani) ambaye tunaona anajisukuma na ujasiriamali wake wa vitu tofauti, ameamua kabisaaa…kuliruhusu Tanki la “KINYESI” kujaa na kuanza kutiririsha “Juisi ya Kinyesi” katika Maeneo ambayo tunapita, na hata kuweka Vituo kwa ajili ya Mazungumzo binafsi.

Kama ambavyo unaona hizo picha, kuna baadhi ya Waungwana wanadai kuwa, walishawahi kumwambia Kiongozi huyo ambaye nafasi yake ni EXPIRED kwa hivi sasa, lakini amekuwa akipiga kimya tu, jambo ambalo UTA, tumetafsiri kama “NYODO”

DOH !!!!!

CHRIS BROWN NA KARREUCHE HAWAKUSOMEKA KABISA CLUB

3:06:00 AM Add Comment

KUNA uwezekano Mkubwa kabisa ukajiuliza maswali mengi kuhusu Kurudi kwa mahusiano ya Chris Brown na KarreucheTran, baada ya Breezy kutoka Jela, huku awali ikibainika kuwa alikuwa amepigana Chini na mamito huyo, lakini Hivi Ndivyo inavyoanza kuhisiwa.

Siku ya jana , TTM tulipata Mtonyo na Baadhi ya Picha ambazo zilimuonesha Chris Brown akiingia na Kutoka kunako Night Club Moja, akiwa na Girlfriend wake Huyo, Karreuche, kwa ajili ya Bata za hapa na Pale, lakini baada ya kitengo CHIMBUA CHIMBUA kuzama Kiundani zaidi, kuna hili ambalo limesomeka.

Karreuche Tran hakuwa karibu sana na Chris Brown ndani ya Night Club Hiyo tofauti na ilivyokuwa ikidhaniwa, zaidi ya Kustick na Bibie wa YMCMB, CHRISTINA MILLIAN.

Tofauti na kuwa na Christina, Karreuche alikuwa busy akipiga mtungi wake kawaida, pamoja na Kucheza Mikwaju kadhaa ambayo ilionekana kumuingia, huku Breezy akiwa haishi kumkata Jicho mara kadhaa, hali ambayo iliashiria kuwa huendawawili hao, hawakuwa Vizuri.

Aidha katika Hali Nyingine ambayo ilizua maswali kwa Wengi, Chris Brown alionekana kutokufurahia kabisa Usiku huo ndani ya Club hiyo inayofahamika kwa Jina la SOCIALITE CLUB, inayosifika kwa Kuwahusisha Wapenzi wa Jinsia Moja, huku karreuche akiwa katika Mood Nzuri.

Pia Bibie huyo alionekana kuwa Bize zaidi na Simu kulikokuwa Busy na Chris Brown, lakini baadaye inasemekana kuwa baada ya kutoka Nje kupokea Simu aliyopigiwa na Mtu ambaye hakufahamika mara Moja,aliizima kabisa.


Chris Brown na Karreuche, wamekuwa wakipigana Chini na Kurudiana tangia wameanzisha Mahusiano yao mwaka 2010, ikiwa ni baada ya Breezy kuachana na Rihanna mwaka 2009.

KANYE WEST KUWEKA HOSPITALI NDOGO NDANI YA JUMBA LAKE LA KIFAHARI, LAKINI KIM KARDASHIAN HAONI UMUHIMU...

2:46:00 AM Add Comment

WANASEMAGA, Ukiwa na Mkwanja, basi unaweza fanya chochote ambacho unajiskia kufanya, na hicho Ndicho Rapper Kanye West amthibitisha, TTM tuna Mtonyo Kamili.

Kuna uwezekano Mkubwa kabisa kuwa katika Jengo kubwa la Kifahari ambalo linajengwa Kwa ajili ya Familia ya Kanye West huko, LOS ANGELS, Nchini Marekani, itapatikana Hospitali Ndogo ambayo itakuwa ni Maalum kwa ajili ya Familia Yake.

Kwa Mujibu wa Kitengo aminifu cha Chimbua Chimbua kutoka TTM, Kanye ambaye hivi sasa ana umri wa Miaka 37, anatarajia kutumia EURO MILIONI 3 kwa ajili ya kujenga Hospital Hiyo ndogo ambayo ni mahsusi kabisa kwa ajili ya Afya yake, Mke wake Kim kardashian, pamoja na Mtoto wao North West Mwenye Umri wa Mwaka mmoja hivi sasa.

Aidha katika Hospitali ndogo hiyo ya Ndani, itajumuisha Vitu vifaa kama Vile Mashine ya X-RAY, CT Scanner, ULTRA SOUND MACHINE, na Vifaa vingine kwaajili ya Kuchukua na Kupima Damu.

Tofauti na Vifaa hivyo, Pia Kanye anatarajia Kuwaajili Madaktari na Wauguzi ambao watakuwa wakifuatilia afya za Familia Hiyo mara kwa mara, pamoja na Timu maalum ya kumtizama na kuwa makini na Mtoto wake North West..

Katika hali Nyingine, Kim Kardashian anaamini kuwa Mme wake Huyo Kanye, anaenda Mbali sana katika maamuzi hasa ya Kujenga Hospitali hiyo katika jumba lao, kwani ni kitu ambacho hakina ulazima sana kuwa nacho, lakini hakuna ambacho anaweza fanya ili kumzuia Yeezy.

Moja kati ya watu maarufu ambao wamewahi kujenga Hospital Ndogo katika Nyumba zao ni pamoja na Muimbaji mkongwe wa POP, MADONNA.

Kanye West na Familia yake hivi sasa wanaishi katika Nyumba ya Mama Mkwe Wake, KRIS JENNERS, wakati wakisubiri kumalizika kwa Ukarabati wa Jumba lao hilo huko LA, na wanatarajia kuhamia katika jumba hilo baada ya kila kitu kuwa sawa

UNADHANI RAY C, ATAKUWA KIOO SIKU YA ALHAMIS 26 JUNE?...

2:20:00 AM Add Comment


Harakati za Kupiga Vita matumizi ya Madawa ya Kulevya hasa kwa rika la Vijana, zinazidi kutanuka, baada ya Mwanaharakati RAY C kujitosa katika SIKU YA KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA.

Kupitia account yake ya Instagram, Ray C ambaye aliwahi kufanya Vizuri na Track ya SIKUHITAJI, amepost PICHA za maandalizi ya Banda La taasisi yake ya RAY C FOUNDATION, litakaloonesha shughuli mbali mbali ambazo anazozifanya, katika Siku Hiyo itakayoadimishwa ALHAMIS ya Tarehe 26 Mwezi wa 6, Jijini Mbeya.


Mgeni Rasmi katika Siku hiyo maalum kabisa Duniani, atakuwa Dr.Galib Bilal, makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Ray C amekuwa katika Harakati za kupiga Vita Matumizi ya Madawa ya Kulevya, ikiwa ni Baada tu ya Kusaidiwa Kuepukana na matumizi hayo ambayo yalikuwa yamemuathiri kwa kiasi kikubwa, na mpaka hivi sasa ameshasaidia baadhi ya Vijana ambao wataungana Naye huko Jijini Mbeya katika banda lake.

Kwa Mtazamo wako, Unadhani RAY C atakuwa Kioo cha Watu Wengi Siku Hiyo?

MNADA BANNER