REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HUU NDIO MWILI WA MAREHEMU DAUDI MWANGOSI PUNDE BAADA YA KUUAWA....INASIKITISHA

2:30:00 AM Add Comment




Huwezi Kuamini huyu Ni Binadamu aliyeafariki Kifo Hiki. Huu Ni mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi, Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel Ten, na mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Iringa

Ni kweli Wanahabari wa taifa hili la Tanzania lilijaa kila aina Ya Uonevu kwa Nguzo muhimu kwa Nchi, Tutakuwa tunakufa Vifo vya Aina Hii?

Haki Yetu ya Msingi Tunaipata Wapi?...ni Lini Wanahabari Tutathaminika?...Hii ndiyo Stahili yetu, ama Haki Yetu tunayopata katika Kuisaidia Serikali na Nchi Nzima Kiujumla?

LILAANIWE JESHI LA POLISI...NARUDIA TENA LILAANIWE...NIKO TAYARI KWA LOLOTE IKIWA NINAFAHAMU NITAKUFA KIFO KAMA HIKI NA MIMI.

REST IN PEACE MY LOVELY BROTHER DAUD MWANGOSI

1:54:00 AM Add Comment

Na Frank M. Joachim


                                                  Marehemu Daudi Mwangosi


Marehemu Daud Mwangosi (Kulia) akiteta Jambo katika Kikao cha wanahabri Mkoani Iringa, Siku Moja kabla ya Kifo Chake.

Marehemu Mwangosi katika Majadiliano, pembeni ya Kibanda Cha Magazeti, Mkoani Iringa



Marehemu Mwangosi akiwa Mtaani katika Harakati za Kuufahamisha Umma.



Hilo ndilo lilikuwa Zoezi lake la Mwisho ili kuufahamisha Umma kuhusu Mkutano wa CHADEMA, uliosababisha Vurugu na hatimaye Umauti Kumkuta. Hapo Marehemu Mwangosi (Aliyevaa sweta la Kaki na Suruali Nyeupe huku amenyanyua Mikono kupiga Picha) akipiga Picha siku ya Kifo Chake. Hakujua kama hayo yangemkuta, na sasa ni hadithi nyingine Tena



Polisi wakionekana Kumshambulia Marehemu Daudi Mwangosi (Mguu wake ni huo unaonekana ukiwa na Suruali Nyeupe).
*****************************************

Pumzika Kwa Amani Mpendwa Wetu Daudi Mwangosi. Tuko nyuma Yako katika kupigania Haki za Watanzania Wanyonge. Tutaimarisha Msingi uliouanzisha.



WAFUASI WA GADDAFI WALIOSALIA< WAKAMATWA LIBYA

1:20:00 AM Add Comment





Na Frank M. Joachim

Duru za usalama nchini Libya zimetangaza habari ya kutiwa mbaroni wanamgambo wenye silaha wanaoaminiwa kuwa ni mabaki ya utawala wa Kanali Muammar Gaddafi uliopinduliwa nchini humo.

Watu hao wametiwa mbaroni kwa tuhuma za kushambulia maeneo nyeti na muhimu ya mji wa bandari wa Sirte wa kaskazini mwa Libya pamoja na kupanga kufanya mashambulizi katika maeneo mengine ya nchi hiyo.

Shirika rasmi la habari la Libya (WAL) limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, maafisa usalama wa nchi hiyo wamewatia mbaroni watu kadhaa ambao inaaminiwa ni wafuasi wa utawala uliopinduliwa wa nchi hiyo na ambao walifanya mashambulizi katika maeneo muhimu ya mji huo.



Kwa mujibu wa ripoti hiyo, miongoni mwa maeneo muhimu yaliyoshambuliwa na wanamgambo hao ni kituo cha kuzalisha umeme cha az Zaafaran ambacho kinazalisha umeme wa mji wa Sirte. Maafisa usalama wa Libaya wamesema kuwa, watu hao walikishambulia kwa roketi kituo hicho.

WATU 9 WAUAWA MADAGASCAR

12:48:00 AM Add Comment




Na Frank M. Joachim

Habari kutoka Madagascar zinaarifu kuwa, watu 9 wameuawa katika mapigano yaliyozuka kati ya polisi na watu wenye silaha kusini mwa nchi hiyo. 

Duru za habari zinaaru kuwa, 6 kati ya watu hao waliouawa walikuwa miongoni mwa wanachama wa kundi hilo lililokuwa na silaha, huku wengine 3 wakiwa wakiwa wanajeshi. Hadi sasa makumi ya watu wamekwishauawa katika ufyatulianaji risasi kati ya wanajeshi na watu wenye silaha ambao wanajihusisha na wizi nchini Madagascar. 

Ni vyema kuashiria hapa kwamba, Madagascar imekuwa ikikabiliwa na hali ya mchafukoge tangu kulipotokea mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'oa madarakani rais wa nchi hiyo miaka minne iliyopita.  

Ndege Za Kijeshi za Marekani zaua Watu 13

12:38:00 AM Add Comment




Na Frank M. Joachim

Ndege za kijeshi zisizo na rubani za Marekani zimetekeleza shambulio nchini Yemen na kuua watu wasiopungua 13. 

Hayo yamethibitishwa na kingozi mmoja wa ngazi za juu wa Yemen ambaye hakutaka jina lake litajwe  na kuongeza kuwa, shambulio hilo lililofanywa na ndege za Marekani zisizo na rubani, lilifanyika hapo jana dhidi ya watu wanaodhaniwa kuwa na mahusiano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaida.

 Amesema kuwa, shambulio hilo halikuweza kupiga eneo husika na badala yake lililenga magari mawili ya raia katika mji wa Radda unaopatikana katika mkoa wa Al Bayda ambapo watu 13 waliuawa papo hapo wakiwemo wanawake wawili na wengine wakijeruhiwa vibaya.

 Wananchi wa Yemen wamekuwa wakipinga vikali uingiliaji wa Marekani nchi mwao sambamba na kufanya maandamano makubwa huku wakitoa nara za "Mauti kwa Marekani, Mauti kwa Israel." Mbali na Wayemeni hao kupinga uingiliaji wa Marekani nchini kwao, wanapinga na kulaani mashambulizi ya ndege hizo zisizo na Rubani nchini humo ambayo mwezi uliopita yaliua idadi kubwa ya raia wasio na hatia. 

Hivi karibuni Rais Barack Obama wa Marekani alijigamba akidai kuwa, kila Mmarekani anaona fakhari kwamba nchini yake ina nguvu na inaheshimiwa kwa kuendesha vitani zaidi duniani.

MNADA BANNER