REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HIVI NDIVYO MSANII WA MAIGIZO NCHINI , RAYUU, ALIVYOONGEZA TATUU YA JUU YA MAKALIONI

10:15:00 AM Add Comment


Rais Kikwete Atembelea Kanisa Liliharibiwa na Vurugu za Baadhi ya WAISLAAM , Mbagala

10:11:00 AM Add Comment





BONGO MOVIES - HIZI NDIZO MOVIE ZILIZOKO SOKONI...PATA NAKALA YAKO HALISI

1:25:00 AM Add Comment










WAISLAAM 20 WAUAWA

12:32:00 AM Add Comment
LAGOS, Nigeria


Waislamu wasiopungua 20 wameuliwa na watu waliokuwa na silaha baada ya watu hao kuushambulia msikiti katika kijiji kimoja cha kaskazini mwa Nigeria. 

Mauaji hayo yametokea leo katika kijiji cha Dogo Dawa cha jimbo la Kaduna. Abdullahi Muhammad, afisa katika eneo hilo amesema kuwa wanashuku kuwa mauaji hayo huwenda ni ya kulipiza kisasi na huenda yamefanywa na magenge ya majambazi yenye silaha baada ya kuwapoteza baadhi ya wanachama wake katika ufyatulianaji risasi uliojiri hivi karibuni kijijini hapo kati ya majambazi hao na wanavijiji.  

Amesema wakazi wa kijiji hicho wamekuwa wakivamiwa mara kwa mara na watu wenye silaha wanaofanya mashambulizi kutokea kwenye kambi zao zilizoko msituni.

UCHAGUZI TUNISIA, KUFANYIKA JUNE 2013

12:25:00 AM Add Comment

TUNIS, Tunisia


Serikali ya mseto ya Tunisia inayooongozwa na harakati ya Kiislamu ya an Nahdha imetangaza kuwa imekubali kuendesha chaguzi za rais na bunge tarehe 23 mwezi Juni ambapo rais atachaguliwa moja kwa moja na wapiga kura.

 Makubaliano hayo yamejiri baada ya mrengo wa upinzani kukosoa vikali kwamba harakati ya an Nahdha inataka kudhibiti serikali na kukwepa uchaguzi.

 Harakati ya Kiislamu ya an Nahdha ya huko Tunisia ilishinda uchaguzi wa kwanza huru nchini humo mwezi Oktoba mwaka jana kufuatia mapinduzi ya wananchi yaliyomng'oa madarakani Rais Zainul Abidin bin Ali. 

Serikali ya mseto ya Tunisia imesema kuwa wamefikia makubaliano ya kuendesha chaguzi za rais na bunge tarehe 23 mwezi Juni mwaka huu, na duru ya pili ya uchaguzi wa rais tarehe saba Julai.

29 Wauawa Nchini Somalia

12:17:00 AM Add Comment




Watu wasiopungua 29 wameuawa nchini Somalia kufuatia mashambulio ya kigaidi ya ndege zisizo na rubani za Marekani. 

Habari kutoka Somalia zinasema kwamba, ndege zisizo na rubani za Marekani zimefanya mashambulio katika maeneo yanayosadikiwa kuwa ya wanamgambo wa Al-Shabab katika mji wa Merka kusini mwa nchi hiyo.

 Mashambulio hayo ya ndege zisizo na rubani za Marekani yamefanywa siku chache tu baada ya watu wengine kadhaa kuuawa kufuatia mashambulio kama hayo nchini Somalia. 

Ndege zisizo na rubani za Marekani zimekuwa zikitumiwa kushambulia maeneo mbalimbali katika nchi za Afghanistan, Somalia, Yemen, Libya na Pakistan.

 Umoja wa Mataifa unailaumu Marekani kwa mauaji yanayofanywa na ndege zisizo na rubani za nchi hiyo katika nchi mbalimbali ukisema kuwa yanakiuka sheria za kimataifa; lakini hadi sasa haujaichukulia hatua yoyote ile serikali ya Marekani.

MNADA BANNER