REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

HATIMAYE: KERI HILSON AMEZUNGUMZA SABABU YA KUACHIKA.

1:09:00 AM Add Comment

BLACK TOUCHEZ
MDUDU wa Usaliti katika Mahusiano ya Watu Maarufu hasa wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, ambapo safari hii, Keri Hilson naye ameamua kuvunja Kimya.

Hit Maker huyo wa Loose Control aliomshirikisha Rapper Nelly, amesema kuwa, sababu kubwa ya yeye kupigana Chini na Mchumba wake SERGE IBAKA ambaye ni Mtupia Kikapu wa NBA, ni baada ya kubaini kuwa amempata mtu tofauti na alivyotarajia.

Akifyatuka kwa Hisia kuhusu hilo, Kerry Hilson anadai kuwa akiwa kama mtu mwenye msimamo kama ambavyo anafahamika katika Muziki wa RnB, basi alidhani pia amepata Mtu mwenye msimamo dhahir, lakini ikawa topfauti, kitu ambacho kilimuangusha

Pia Keri Hilson aliongeza Hivi :
"Katika maisha yangu ya Mahusiano, sheria yangu ilikuwa ni kutokuwa na mwanaume ambaye ni mwanamichezo, Rapper, au Muigizaji, lakini ghafla nikavunja sheria yangu baada ya kukutana na Huyu mtu. Ila ameniangusha kabisa kwa kuwa tofauti na Matarajio yangu. "

Pia Katika kauli Nyingine, Keri Hilson amesema hivi
"Sina Tofauti na Wanawake wengine linapokuja suala zima la Mvuto na Ubora kwa Mwanaume. Level yangu iko mbele sana. Ninamtaka Mwanaume ambaye anampenda Mungu vizuri sana, na kumuheshimu mwanamke, na Mstaarabu. Yale yale ambayo kila mwanamke bora anayapenda"

KEISHA: AHSANTE MUME WANGU !!!!

12:22:00 AM Add Comment

NA BABA JUTI
HATIMAYE Msanii ambaye amekuwa Kimya kwa Muda Mrefu sana katika Muziki Industry, ameweza kuibua jambo lingine ambalo ni la kufurahia na hata kujivunia, huku shukrani kubwa zikienda kwa Mwenyezi Mungu na Watu wawili ambao ni Muhimu kwake.

KEISHA, ambaye hivi karibuni amehitimu elimu ya Chuo Kikuu, sanjari na kupata mtoto mwingine wa Tatu, amemshukuru sana Mume wake JAM JAYS kwa kuwa naye kwa Takriban muda wote na hata kuvumilia mengi ambayo wameyapitia na hata kufanikiwa watoto watatu...

Nukuu !!
"Nimebarikiwa, ninafuraha na niajivunia. Shukrani sana Mume wangu Mpendwa kwa kuwa Sehemu ya Maisha Yangu siku zote. Ni bahati kubwa sana kuwa na wewe Maishani Mwangu. Shukrani tena kwa kuwa Baba Bora wa Watoto wangu watatu kwa mapenzi yako yote, na kuendelea kusupport na kutimiza ndoto zangu. Ni 100% kweli kabis, katika Mafanikio ya Mwanamke, basi kuna mwanamume nyuima ya mafanikio hayo. Nakupenda sana Mume wangu JAMYJYS"


Tofauti na hilo, Kesha pia amemshukuru Mama yake, na kusema kabisa kuwa yeye ni Mungu wa Pili kwake

Pia Keisha amedai kuwa, mama yake alikomaa na kila kitu ili ampatie maisha ikiwemo kuuza biashara ndogo ndogo

Nukuu
"Ana nafasi ya kipekee sana mama yangu kama nilivyonayo mimi kwake nakiri kusema bila yeye mimi si kitu huyu ni mungu wangu wa pili hakuna anebisha furaha yangu ni yake maumivu yangu ni yake shida zangu ni zake mimi ni wapekee kwake hana mwingine kwenye maisha yake mapenzi yake kwangu siwezi yaelezea hakuna ambacho hajafanya kwaajili yangu anauza kila aina ya biashara ndogondogo zote mimi nifurahie maisha hata ingetokea nizaliwe upya ningeomba nizaliwe na huyu mwajuma binti salum mama khadija mwenyewe. Nakupenda sana mama yangu mungu pekee ndo anajua nani kama mama jamani???"

Neno Moja kwa Keisha Tafadhari !!

MNADA BANNER