REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MUNGU ASHUKURIWE : HATIMAYE RAY C AMEPONA NA KUREJEA KATIKA HALI YAKE BAADA YA RAIS KIKWETE KUMSAIDIA KUPATA MATIBABU.....

9:21:00 AM Add Comment
Mh.Raisi Kikwete akiwa na mwanamuziki Rehema Chalamila aka Ray C leo Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati mwanamuziki huyo alipoenda kumtembelea Raisi na kumpa shukrani kwa kumsaidia kwenye matibabu ya juu ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua. Aidha Ray C alimueleza Raisi kwamba afya yake imeimarika na kwamba muda mfupi ujao atarudi kuendelea na kazi yake ya muziki. Kwa upande wa mama yake Ray C amemshukuru Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanae kwa kugharamia matibabu yote ya mwanae.




Raisi Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Ray C, Mama yake mzazi Ray C - Margreth Mtweve na aliyevaa nguo za pinki upande wa kulia ni dada yake Ray C - Sarah Mtweve.

Picha na Freddy Maro

MBABE NI MBABE TU...MIYEYUSHO ALIMTOA NASIB KWA "KNOK OUT"...

7:37:00 AM Add Comment
 KITUUUUUUU....Yalabi Tobaaaa..Miyeyusho alimsukumia Konde Gumu Mpinzani wake NASIB
 Mhe. Dr. Fenella Mukangara akimkabidhi Rasmi Ushindi Bondia Francis Miyeyusho

   WATU WEWEEEEE...Mashabiki wakimshangilia Bondia FRANCIS MIYEYUSHO

HIVI NDIVYO KINANA ALIVYOKUTANA NA MAKATIBU WAKUU WA MIKOA WA CCM

7:26:00 AM Add Comment
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao chake cha Sekretarieti na Makatibu wa CCM wa mikoa, leo, Desemba 11, 2012, katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na wengine kutoka kushoto ni Makatibu wa NEC,  Asha-Rose Migoro (Siasa na Mambo ya Nje), Zakia Meghji (Uchumi na Fedha), Nape Nnauye (Itikadi na Uenezi) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai.


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao chake cha Sekretarieti na Makatibu wa CCM wa mikoa, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai


Makatibu wa CCM wa mikoa wakiwa kwenye mkutano wao na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.




Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar) Vuai Ali Vuai akisalimiana na Katibu wa NEC, Siasa na Mambo ya Nje, Asha-Rose Migiro, kabla ya kuanza kikao cha Sekretarieti na Makatibu wa CCM wa mikoa, leo katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Oganaizesheni Muhammed Seif Khatib. (Picha na Bashir Nkoromo).

MNADA BANNER