REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

BOW WOW !!! : NINAHITAJI MWANAMKE WA KUFANYA NAYE MAPENZI, MAHUSIANO YA KIMAPENZI YANARUDISHA NYUMA

3:18:00 AM Add Comment

Na Baba Juti    
#Hii Inaweza ikawa ni wiki ya Suala la Mahusiano maana kuna baadhi wanaonekana kuyafurahia lakini pia kuna wengine wanaonekana kuyachukia kabisa

Rapper Bow Wow ambaye Jina lake Halisi ni SHAD MOSS amedai kuwa hivi sasa hahitaji kabisa kitu kinachoitwa MAHUSIANO YA KIMAPENZI, bali anahitaji Mwanamke au rafiki wa Kulala Naye na kula BATA

Bow Weezy amepost kauli hiyo kupitia Instagram account yake, hali ambayo inaashiria kuwa tayari ni nkama amechoshwa na kitu kunachoitwa MAHABA ama MAPENZI


Tunamnukuu  
" Sihitaji Mahusiano ya Kimapenzi, maana yanakubana na kukurudisha Nyuma. Ninahitaji Rafiki wa Dhati ambaye nitalala naye, nitafanya naye mapenzi, nitapigania naye maisha, nitakayepata naye pesa, tukafanye shopping, tukafurahie club, na nitakayeishi naye maishani. ninahitaji Mshirika katika yote, yaani mwenzangu wa maisha. yule ambaye nitacheka naye na kujenga naye. Mwanamke ambaye sintoogopa kumpoteza sababu nafahamu muda wote atakuwepo. Mahusiano hutumika kuchezea ila mshirika nitampokea 100%"


JAMANI NYIE !!! : J LO ANADAI KUWA MAHUSIANO YAKE YA SASA NA A-ROD NDIYO MAHUSIANO YAKE YA FURAHA NA DHATI KWA MARA YA KWANZA, LICHA YA KUOLEWA MARA KIBAO

2:58:00 AM Add Comment

Na Baba Juti 
#WatuWaMungu Hakika kama umeshawahi kuwa na mahusiano na Mwanamke yeyote, halafu baada ya kuachana naye nausikia yuko na mshikaji mwingine, halafu anasema kuwa ...hayo ndio mahusaino yake ya kwanza yenye furaha kuliko mengine

Hiyo ndiyo kauli ya Jeniffer Lopez ambaye tunafahamu ameshawahi kuolewa na Wanaume Wengi sana na hata kukunjuka na wanaume Wengi Pia

Akizungumza hilo kwa ujasiri mkubwa, Jennifer Lopez ambaye kipindi cha nyuma pia alikuwa na mahusiano na Rapper Drake, amesema kuwa ni kweli kipindi cha nyuma amewahi kuwa na mahusiano kadha wa kadjha, lakini mahusiano ambayo yuko nayo hivi sasa na Alex Rodriguez a.k.a A- Rod ndiyo mahusiano yake ya kwanza kabisa kufurahia

Akifafanua kuhusu kauli yake, J-Lo alidai kuwa wanafurahishana pamoja, na wanapeana kile ambacho hawajawahi kukipata popote pale. Pia bibie huyo ambaye ni hitmaker wa LOVE DONT COST A THING, aliongeza kuwa, katika mapenzi yao ambayo wanayaita ni mapenzai ya dhati, hupeana support kila mmoja kwa mwenzie, na hawajui nini maana ya maumivu, hivyo hajawahi kufurahia kitu kama hicho

JAMANI NYIE !!! : FERGIE WA BLACK EYED PEAS AACHANA NA MUMEWE WALIYEDUMU KATIKA NDOA KWA MIAKA 8

2:17:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
#WatuWaMungu Tunakumbuka Vizuri kabisa mikwaju ambayo iliwahi kutikisa Dunia bila Kificho, yaani mizgo kama HEY MAMA !, WHERE IS THE LOVE na Mingineyo Mingi

Mizigo hiyo ilikuwa inaundwa na kundi moja lilikuwa na utofauti wa aina yake na makundi mengine ya Muziki, linaloitwa BLACK EYED PEAS ambalo lilindwa mwaka 1995 huko Los Angels Califonia, Marekani.

Vichwa vilivyokuwa vinaunda Kundi hilo , ni pamoja na WILL. I AM, TABOO, APL.DE.AP pamoja na mwanamkee Pekee FERGIE.

Sasa, leop ndo tunamzungumzia huyu Bibie ambaye anaitwa Fergie, ambaye kuna kipindi cha Nyuma kidogo zilikuja kuibuka taarifa kuwa ameamua kama kukaa kando kidogo na kundi hili, huku tafsiri kubwa ikiwa ni Majukumu ya kifamilia, Yaani Ndoa

Sasa baada ya kudumu katika Ndoa yake na mumewe anayeitwa JOSH DUHAMEL kwa Miaka 8, hatimaye safari yao imefikia Mwisho kabisaaaa

Ingawa Mpaka Hivi sasa haijawekwa wazi chanzo cha wanadoa hao kufikia maamuzi ya kupeana talaka, Bado wote yaani Fergie na Josh Duhamel walitoa taarifa ifuatayo kama ambavyo tunainukuu

" Kwa Heshima na Upendo, tumeamua kuachana kama wapenzi mapema mwaka huu. Hii ni kuipa nafasi bora familia yetu. Tulihitaji kuifanya hii kama ishu binafsi au ya siri kabla ya kuitoa kwa umma. Tupo na tutazidi kuwa pamoja katika kusaidiana kati yetu na familia nzima"


SAY WHAAAAAT?..TRUE LOVE NEVER DIE? ...NAS NA NICK MINAJ WAMEYARUDISHA MAHABA?

1:35:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWa Mungu hapo awali tulikuwa tunafahamu vizuri kuwa Mahusiano ya Nick Minaj na Rapper Nas ni kama yamefikia kikomo baada ya kutokudumu kwa muda mrefu kama ambavyo tulitarajia.

Baada ya hapo tulianza kusikia fununu za huku na kule kuwa Nicki Minaj na Rapper kutoka kundi la THE MIGOS , Quavo, mambo ya kimahaba sasa hivi yako wazi, yaani "halifichiki"

Lakini katika hali isiyo ya kawaida, Kunako Usiku wa Rapper Nas, yaani Birthday yake ya kutimiza Miaka 44, Nicki Minaj alikuwa ni moja kati ya watu ambao walihudhuria ukiachilia mbali akina Swizz Beatz, na kulikuwa na kila aina ya Furaha baina ya Wawili hawa

Na ili kuonesha mahaba ya Dhati, Nicki Minaj alihuisika Vizuri tu katika Kuzima Mishumaa ambayo ilikuwa katika Keki ya Nas, hali ambayo iliashiria kuwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa wawili hawa kuendelea kupendana katika Maisha yao


MNADA BANNER