REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

FREEDOM IS ON THE WAY. 01.06.2014

6:44:00 AM Add Comment

MWEZI JUNI Utakuwa ni Mwezi wa Kupokea Balaa jingine Toka Kwa KENYAN-BORN-RAPPER anayefahamika kwa Jina la JAMAA TU FLANI, Mweny maskani yake Nchini CANADA.

Kwaju hilo ambalo Limepwa Title La FREEDOM, litaanza Kukita Kunako Social Medias na Jumatatu, huku tarehe 02 JUNE, likiachiwa Exclusively Kunako kipindi cha Jam Session Cha 99.4 Metro FM, Mwanza.


FREEDOM ni Wimbo ambao Umepikwa na Producer Deey Classic kutoka Revolution Sound-Mwanza, Huku Vichwa Viwili Kutoka Mwanza, FEMALE MC – NATTY E BRADY na Bibie anayeonea sana kunako R&B na ZOUK –Honeya, ndio waliokamilisha “KOLABO” zito kunako Track Hiyo

OXS- MWEZI WA SITA ITAKUWA NI PROJECT AFTER PROJECT

6:04:00 AM Add Comment

BAADA ya Kutambulisha Mixtape yake ya OXY-GEN, rapper na Producer wa Metro Fm , Mwanza, Abdallah “Oxs” Okelleky, amesema kuwa Mwezi wa Sita Ni “Project After Project”

Akipiga Story na Black Touchez, Oxs amesema Kuwa, Hivi sasa anakamilisha Utafiti wa Soko lake hasa baada ya Kuachia Mixtape yake, na kitakachofuata na Kuanza kupiga Project Moja Baada ya Nyingine na Producers Wa Mwanza.

Pia Oxs ambaye Bado anakita na Kwaju la “PARTY” ambalo ameshirikiana na Juma Nature na Q-The Don, amesema Kuwa Traxx zake Zitashirikisha wasanii Mbali mbali, ambao anaamini wako vizuri katika Music Industry , na wanajua wanachokifanya

“Ninawakubali Wasanii Wote Nchini Tanzania, na Afrika Mashariki Kiujumla. Ila Niko tayari kufanya kazi na wasanii ambao Ninaamini Wanajitambua, na wako serious na Game. Nikishapata Ushauri toka Kwa Meneja wangu kuhusu Msanii ambaye nitafanya naye kazi, basi amini Msiamini, Mwezi wa Sita itakuwa ni PROJECT AFTER PROJECT”


Mixtape ya OXY-GEN ipo Sokoni Hivi sasa, na Inapatikana kwa yeyote anayehitaji

RADIO WA GOODLIFE, UGANDA, AKAMATWA BAADA YA KUKUTWA AMEPANDA BANGI NYUMBANI KWAKE

5:29:00 AM Add Comment
(c) NEW VISION
KAMPALA, Uganda
Inaonekana Kitu BANGI imaeanza kuchukua Sura Mpya katika maisha ya watu maarufu, ikiwa ni baada tu ya WIZ KHALIFA kukamatwa Airport akiwa na Mmea korofi , yaani bangi.

Sasa , Some where in East Afrika, Kwa –abalunji, ba-sssebo, Nazungumzia Uganda, Msanii Kutoka Kundi la Goodlife, Radio, ameingia kunako mbwadidi la hatari baada ya jeswhi la Polisi nchini humo Kubaini Kuwa amepanda mmea wa bangi katika Nyumba ambayo anaishi
(c) NEW VISION-UGANDA

Tukio hilo ambalo limetokea ndani ya Wiki Hii, lilisababishwa na Ugomvi ambao ulitokea katika baa ya CASSABLANKA, ambayo Radio na Weasel hupenda kutembelea, ambapo RADIO aligombana na Msanii AK47, na wasanii wengineo akiwamo SHEEBAH,PALLASO, KING SAHA.
(c) NEW VISION

Data Zinazidi kumiminika Kuwa, ugomvi huo ulidumu kwa Muda Kadhaa, na Kisha Kufika Mpaka Nyumbani kwa Msanii huyo MOZEH RADIO, hali ambayo ilisababisha Uharibifu wa vitu kama Vile madirisha na Vioo Vya gari lake.
(c) NEW VISION

Sasa wakati jeshi la polisi lilipotia Timu Nyumbani Kwa Weasel kwa ajili ya kutuliza Ghasia, Mbwadidi linguine likaibuka, na hatimaye Kukamatwa kwa Mimea kadhaa ya BANGI ambayo radio alikuwa ameipanda katika mazingira ya Nyumba yake.
Hata hivyo bangi hiyo Iling’olewa na Kuchomwa moto kama ilivyo kawaida..

(c) NEW VISION

SSSSSSSSSS..PUFF,,OHOHOHOOO…

CINDY SANYU AMEMCHANA SHABIKI MZEE ALIYEMTUMIA PICHA YA UUME WAKE

5:17:00 AM Add Comment

KAMPALA, Uganda
Within This Week, Vitu Kibao tu Zimetokea ila la Kushangaza ni hili ambalo Limemtokea Cindy, Kitengo Chimbua Chimbua Kinatoa Ripoti…

Hivi majuzi, Sweet baby na muimbaji Mtamu sana Kutoka Nchini Uganda, Cindy Sanyu, aliamua kumlipukia Shabiki ake Mzee ambaye alimtumia Picha ya UUME katika Upande wa Meseji kunako Mtandao wa facebook.

Baada ya Kukutana na Mbwadidi la Mzee huyo kunako Inbox yake, aliamua Kumuanika Mzee huyo katika Wall yake, lakini jambo la kumshukuru mwenyezi mungu ni Kwamba, hakuanika Zile Private Messeges ambazio zilikuwa zimetumwa na Mzee Huyo.

Wakati akimuanika Mzee huyo, Cindy alipost kuwa, badio yuko katika Mshtuko baada ya Kibabu hicho kumtumia Picha ya Uume wake, kwa sababu kwanza hakutarajia kama Mtu Mzima kama huyo anweza kufanya kitu cha kipumbavu, huku akiomba Msaada, ni hatua gani azichukue dhidi yake.


Hata hivyo baada ya kupokea Ushauri mwingi katika Comments, Cindy aliwashukuru fans wake, huku akiamini kuwa, kibabu hicho kitakuwa kimejifunza Heshima nidhamu na Adabu.

HII NDIYO SABABU YA JAY Z NA BEYONCE KUTOKUHUDHURIA NDOA YA KANYE NA KIM.

5:10:00 AM Add Comment

NEW YORK, Marekani.
INFACT Kila mtu atakuwa bado anajiuliza kuhusiana na sababu Kubwa ya msingi ambayo ilimfanya Jay Z na Beyonce washudhurie Ndoa ya Rafiki zao wa karibu, Kanye West na Kim Kardashian iliyofnyika Huko Florencia, Italy.

Baada ya TTM kuzama Rasmi kunako Vyanzo mbali mbali, Finaly tumepata ukweli kuhusu sababu ambayo ilisababisha wawili hao Kutokuhudhuria.

Kwa mujibu wa Info za Kuaminika, inasemekana kuwa, sababu kubwa ambayo inapewa nafasi ya Juu, Ni Kuwepo kwa Mwanamke mmoja anayefahamika RACHEL ROY Katika harusi Hiyo, Sikia sasa Undani Wake.

RACHEL ROY (c) HNH
Rachel Roy, Ni Mwanamke ambaye ndiye alikuwa chanzo cha Ugomvi wa JAY Z na SOLANGE, uliotokea Wiki kadhaa Zilizopita katika Lift ya Hotel ya Standard, wakati Wa MEET GALA AFTER PARTY, ambapo inasemekana kuwa, Jiggah alionekana kuanza Kuwa karibu zaidi na Mwanamke Huyo.

Pia Info zinamiminika Kuwa, RACHEL ROY, ambaye ni EX-WIFE wa rafiki wa Jay Z hasa katika Biashara, alisadikika kutaka kuhudhuria Party ya Rihanna (RIHANNA AFTER PARTY), ambayo Pia JAY Z alitaka Kwenda Bila Beyonce, jambo ambalo SOLANGE hakukubaliana nalo, na Baada ya Muda kadhaa ukatokea Ugomvi huo ambao Hivi sasa Ni Story tu.


Kwa Maana Hiyo, Endapo Jay Z na Beyonce wangehudhuria , basi wangekutana na Kimwana Huyo ambaye alihisiwa kutaka kubiringika na Jay Z, na Ndipo la kuibuka lingeibuka.

KUMBU KUMBU YA MWAKA MMOJA TANGIA ALBERT MANGWEA ATUTOKE

5:01:00 AM Add Comment

DAR ES SALAAM, Tanzania
LEO ni Siku ambayo wadau na wapenzi wa Muziki wa Kizazi kipya Nchini, wanakumbuka Kifo cha rapa na Mkali wa Freestyle, Marehem ALBERT MANGWEA- COW WEEZY, tangia ametuachia Simanzi nzito hapo Mwaka jana Tarehe kama Ya Leo, nazungumzia May 28,2013.

Hivyo TTM imezinyaka Info kuwa MASTAA mbalimbali nchini wakiwemo wanamuzik,i wanatarajiwa kushiriki kwenye tukio maalum la kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ , litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nyumbani Park (Samaki samaki Spot) , Kihonda Morogoro mjini.

Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo, Kareeem Omary ‘KO’ alisema maandalizi ya tukio hilo litakalokuwa la kila mwaka, limepwa jina la ‘Love Concert – Kumbukumbu ya kifo cha Albert Mangwe’.

Aidha Kareem, aliwaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuunga mkono kwenye tukio hilo kwani litakuwa la kipekee na la aina yake ambalo pia litatoa fursa kwa wakazi hao pia mikoa jirani na watu kutoka nje ya Tanzania ambao watahudhuria.

Pia  amewataja wasanii watakaotoa burundani, ni pamoja na kutoka kwa kundi la Wanachemba ambalo pia aliwahi kuwa nalo marehemu Ngwair, JSqueezer, P Funky Majani na Mswaki. Kwa upande wa wasanii kutoka Morogoro ni pamoja na Afande Sele, Team Racers, Mc Koba Chris wa Marya, Belle 9, Samir, Zombie, President Mirrow, Jordan wa Dejavu na wengine wengi.

Kabla ya matukio ya shoo ukumbini, itatanguliwa na ibada mbili maalum ikiwemo ya Kanisani na ile ya nyumbani.

MNADA BANNER