REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

NI HESHIMA KUBWA KWA OXS…NDIYE ANAYESHIKILIA NAMBA MOJA KUNAKO JIJI LA MWANZA..

2:47:00 AM Add Comment


MIKWAJU MIWILI inayomhusisha  Msanii ABDALLAH “OXS” OKELEKY, imeweza kumuweka katika heshima yake baada ya kupewa RANK No. 1 Katika Jiji la Mwanza. (KWA MUJIBU WA REVERBANATION)

Tofauti na Hilo, Ngoma Hizo ambazo Ni HOPE na CHUKIA zinazopatikana kunako Mtandao wa REVERBNATION, Pia zimeweza kuwa katika nafasi ya 26 Kitaifa.

“Ninafarijika kupata heshima Hiyo, na nnadhani inadhihirisha namna ambavyo Ninajituma, na ninatakiwa Kudeal na Muziki wangu. Big up to Ma Fanz”


Aidha Track ya HOPE ambayop Hivi sasa Inaonekana Kupendwa zaidi, Inapatikana katika Websites za HULKSHARE, REVERBNATION na AUDIOMACK


NGOMA YA P.DIDY YATAJWA KUWA UCHAFU WA KUTUPWA..SASA NANI KASEMA?

2:25:00 AM Add Comment

WALA HATUTAKI KUINGIA KATIKA UBISHI WOWOTE WALA UGOMVI NA MTU YEYOTE, LAKINI MCHAKATO MZIMA UKO HIVI……

TTM kimenyaka Mtonyo ambao tunaamini ni Uchokonozi Fulani hivi ambao haujaanza Muda Mrefu kihivyo, ila Una Kamuda kidoooogo.
RAPA JACKSON CURTIS maarufu Kama 50 CENTS, amesema Kuwa Track ya BIG HOMMIE ambayo inamilikiwa na Rappa P.DIDDY ni Uchafu Mtupu na Hakuna alichokifanya…

Akizungumza kuhusu hilo, FIF ambae anafahamiika kwa kutafuta Upenyo wa kutoka Kupitia Mabifu kadhaa, amesema kuwa Ngoma Hiyo ambayo Didy ameshirikiana na Jay Z, Ni Ngoma ambayo haina hadhi ya Kuitwa hit song, maana hakuna kilichofanyika humo Ndani zaidi ya UPUUZI tu.

Katika Maelezo Mengine, FIF ambaye hivi karibuni ametajwa na jarida la FORBES kuwa mmoja kati ya Wasanii wa Hip Hop wenye Mkwanja Mrefu, amesema kuwa Kiukweli atazidi kukazia kabisa kuwa Didy Sio Msanii na haiwezi kazi ya sanaa, badala yake anatakiwa kubaki akisimamia Miradi Mingine.

Aidha katika Hali Nyingine 50 amesema kuwa hatokuja Kupenda wala kukukbali ngoma Ya Rappa Huyo P.Diddy

ALIYEKUWA MKE WA NAS…..HAJISUMBUI HATA KUSKIIZA NYIMBO ZAKE.

2:21:00 AM Add Comment

STORI zilikuwa Ni story baada NAS kuzua Mjadala kwa Kutumia Picha Gauni La Ndoa (Shela) la X-WifeWake, Kelis, Katika Album Cover Yake.

Baada ya Kuunyaka Mchakato huo, TTM tulizama kazini kama ilivyo desturi yetu, na Kukutana na Mtonyo ambao Ni vema zaidi ukaufahamu.

KATIKA moja ya Interview kunako jarida la New York Times, Kelis ambaye alikuwa Mke Wa Nas, amezungumza kuwa kwanza sio gauni halisi la Ndioa, bali ni sehemu tu ya gauni hilo, ambalo anaamini alilisahau wakati anatemana na Kuondoka kwa Jamaa Huyo.

Aidha akijibu swali kama alipewa Taarifa na Nas kuhusu Kutumika kwa Picha Hiyo kwny Albam Cover yake, Kelis alidai kuwa, Nas alimpa Taarifa Siku mbili kabla, kuwa atatumia Kitu Hicho, hivyo kwake haikuwa shida hata Kidogo.

Pia Kelis alimiminika kuwa Hata kama sababu ya Nas Kuweka gauni hilo Ingekuwa Mbaya ama Njema, yeye hajalishi Chochote kwa sababu tayari hayuko hata katika maisha yake na Fikra Zake.


Katika Kumalizia, KELIS ameamua Kdhihirisha kuwa hana chochote kwa NAS kwa sababu hata Nyimbo zake hasumbuki hata kidogo kuzisikiliza.

MNADA BANNER