REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MNAZAA WA NINI?: MARIO WINAS ALIYESUMBUA NA "I DONT WANNA KNOW" ASWEKWA RUMANDE KWA KUSHINDWA KUMHUDUMIA MTOTO WAKE WA MIAKA 12

2:56:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu sijui kama mtakuwa mnakumbuka huyu jamaa aliyeukimbiza ulimwengu katika Hisia za Burudani kupitia Track yake inayoitwa I DONT WANNA KNOW akiwa amemshirikisha Rapper P.DIDDY.

Jina lake anaitwa MARIO WINAS, na alikuwa ni moja kati ya wasanii ambao walikuwa wanapatikana katika Record Label ya BAD BOYS ambayo iko chini ya SEAN COMBS maarufu kama DIDDY, mpaka hivi sasa

Sasa Taarifa ambazo tuko nazo mpaka hivi sasa, ni kwamba mkali huyu ambaye hivi sasa ni kama imekuwa ngumu kwake "kufurukuta" katika Game la Muziki, amekutana na RUNGU LA SHERIA baada ya kushindwa kumuhudumia mtoto wake wa Kiume mwenye miaka 12.

Maafisa wa Polisi kutoka Jimbo la BERGEN huko huko Nchini Marekani, walimvaa bwana Mario Siku ya JUMATANO huko Nyumbani kwake FORT LEE na kumkamata kwa kosa la kushindwa kumhudumia mtoto huyo toka kipindi cha nyuma na mpaka kufikia kudaiwa kiasi cha USD 171,000 kitu ambacho ni kinyume na makubaliano ya hapo awali

Ukiachilia mbali suala hilo, Mario Winas aliwahi kukutana na Rungu la kukwepa Kulipa Kodi kuanzia mwaka 2008 mpaka 2012.

Hata hivyo, Mkali huyo wa R&B  mwenye miaka 43, huenda akachezea miaka 6 Jela kama hatosuluhisha mapema jambo hilo

SAY WHAT? : LIL WAYNE ANATARAJIA KUPATA MTOTO WA SITA?

2:16:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
WAUNGWANA kuna habari ambayo binafsi imenibidi niwaze na kukubaliana na akili yangu kuwa sasa ni muda wa kuishusha Kwenu Kabisa, na hii ni kuhusiana na Lil Wayne

Jicho la "Waungwana" hatimaye limebaini kabisa kuwa Rapper Lil Wayne anatarajia kupata Mtoto wa Sita Sasa, kama mwenyezi mungu atajalia kila Kitu.

"Chai" hiyo kuhusu ujauzito mwingine kutoka Kwa Mpenzi wa Hivi sasa wa Lil Wayne, anayeitwa DHEA, ilimwagika katika Birthday Partyu ya Lil wayne ambayo ilikuwa ni Ndogo tu na iliwahusisha washkaji kadhaa akiwemo mpenzi wake huyo wa Hivi sasa

Katika Pekenyua ptkenyua, Dhea alionekana akishoot Video kwa Njia ya Simu, akiwa amevalia Kigauni Cheupe ambacho kilionesha kabisa kuwa Dhea ni mjamzito

Iwapo atapatikana mtoto huyu, Basi atakuwa ni Mtoto wa 6 kutoka kwa Wanawake 6 Tofauti.

FRIDAY BAM !!! : DIAMOND PLATNUMZ FT MORGAN HERITAGE- HALLELUJA

1:54:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
WATU wa Mungu Diamond Platnumz kaachia Video Mpya ambayo hatuna Budi kushare na Wewe. Track Inaitwa HALELLUYA na ameshirikiana na Morgan Heritage Kutoka Jamaica

Itizame kupitia FRIDAY BAM!! ya Baba Juti Blog

MNADA BANNER