REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

BOSI WA TANESCO ATIMULIWA MBALI !!!!!

8:30:00 AM Add Comment
Mhandisi Wiliam Geofrey Mhando, Mkurugenzi Mtendaji Wa Shirika La Nishati ya Umeme Nchini TANESCO, aliyetimuliwa Kazi


Nembo Ya TANESCO



MPITA NJIA : MH. MAGUFULI, TAFADHARI TUSAIDIE KATIKA HILI...TUNATESEKA !!!!

8:12:00 AM Add Comment
 Haya Ni Maeneo Ya Manzese ambako Ujenzi wa Bara bara ya Mabasi yaendayo kwa Kasi unafanyika Hivi sasa. Lakini Licha ya Ujenzi huo, Kuna kero kama ambavyo unajionea Mwenyewe, hali ambayo ni hatari kabisa kabisa kabisa zaidi ya kabisa, kwa Maisha ya Kila Mtanzania ama Mkazi wa Dar es salaam anayefika Eneo Hilo. Hiovi Ndivyo "MPITA NJIA" nilivyojionea, na nnaomba na wewe Ujionee Pia....hapo ni Foleni ya kwenda Posta, gari zinapita hadi kwenye Ujenzi.


 Foleni Kutoka City Center (Posta/ Kariakoo) inakuwa ndio mahala pake kuanzia saa Nane Mchana.


 Abiria hawana Sehemu maalumu ya Kusubiri Magari, namaanisha KITUO CHA DALA DALA. Hadi Leo, nimeshuhudia Watu wakiwa Wamesimama Hivi Kimakundi makundi kuanzia Magomeni KAGERA.


 Magari Yenyewe hayasimami Abiria Tukapanda. Tunasubiri mpaka Basi...yaani ni Tafrani Tupu, tunaweza tukaibiwa Simu Zetu na Bidhaa zetu hasa Mida ya Jioni kabisa


 Vumbi  ndio Mahala Pake. Mafua na Magonjwa Mengine ya Kuambukiza kwa Njia ya Hewa hususan Vumbi yanaambukizwa Kirahisi tu....


Haifahamiki Wapi Kwa Watembea kwa Miguu, Watumia Piki Piki na Baiskeli, Magari Makubwa na Madogo Madogo, na Bajaji. Yaani Tafrani Tupu hasa ikiwemo HATARI YA AJALI za Makusudio kabisa. 


Hakuna Kituo Maalum Cha Boda Boda, Hali inayohatarisha Maisha Ya Watoto na Wakazi wa Dar 


WAPIGA DEBE ndo wasumbufu kupita Maelezo...asipolipwa Hela yake, Gari haliondoki, Hali inayosababisha Foleni kupita Kiasi, Wizi hauishi, magari Tugombanie....ili Mradi Tafrani TUPU


 Wapiga Debe wenyewe wamekaa KI-WIZI WIZI.Sasa Kama Huyo(Mwenye Tisheti Nyekundu iliyochanika), anaita abiria?...au anatafuta Kitu kilichokaa Vibaya ili apite nacho?


Magari Yenyewe Tunagombania na Kujazwa kama Matikiti Maji 


Wanafunzi ndio Kwanza Masikini ya Mungu hawajui wakimbilie wapi 
Haya....Licha ya Vumbi, Uchafu, Mirundikano ya Watu, Mikono Michafu, Biashara ya MACHUNGWA ndio Kwanza inachukua Nafasi. Hii si Hatari kwa Afya Yetu Jamani? (Kwanza Hata Maji ya Kuoshea hayop Machungwa yako Wapi?)

HATUA MEDIA Inazidi Kupiga HATUA

9:17:00 AM Add Comment


Hizi Ni Sample Za Front Cover katika Gazeti litakalokujia Hivi Karibuni, litakalotambulika kwa Jina la HATUA "Ukweli Ni Jukumu Letu".

Gazeti hili litazalishwa na Kampuni ya Hatua (HATUA MEDIA COMPANY Ltd- HAMECO).
Jiandaeni kwa Utamu na Burudani Maridhawa

HONGERA ANORD KAYANDA WA CLODS FM

8:46:00 AM Add Comment
 Hivi Ndivyo Anord Kayanda na Mke wake Anitha Ruhinda Kayanda Walivyokula Kiapo Katika Kanisa la MT JOSEPH

 Dah.....tushakula Kiapo tayari

 Kit cha Keki hichoooooo

 Duuuuuh...Cheki Mng'ao huo

 Champagne Zilikuwepo kama unavyoona

 Wacha weee....wapambe walichangamka Balaa

Mzee Wa Amplifier MILLARD AYO aling'aa Hivi na Mrembo Huyo.

(Picha kwa Hisani ya BAAB KUBWA)

HAYA NDIYO YANAYOWAKUTA WAMAREKANI HIVI SASA...INASIKITISHA

8:16:00 AM Add Comment








Kimbunga Aina Ya Sandy kinachoamabatana na Mvua kali Katika Miji kadhaa ya Nchi ya Marekani, kimeendelea kufanya Yake huku kikiweka utata mkubwa katika Kampeni za Uchaguzi wa Urais Nchini Humo

HIVI NDIVYO P. DIDDY ALIVYPOATA AJALI SIKU YA JANA....

6:15:00 AM Add Comment
 Msanii wa Kundi La Dirty Money na Boss Wa BAD BOY ENTERTAINMENT nchini Marekani, Sean Combs P.Didy akiugulia Maumivu baada ya Kupona katika Ajali iliyotkea Jana Mchana

 Askari Polisi wakiwa Kwenye eneo la Tukio ambako Didy alipata Ajali

 Utaratibu wa Kuliondoa Gari katika Eneo la Tukio Ukifanyika.

 P. Didy akionekana Kutembea kwa Kuchechemea.

 Akipata Huduma ya Kwanza Mara baada ya Ajali

 Gari La P. Diddy lililopata ajali likiwa Nyang'a nyang'a kama unavyoliona

 Diddy akijikagu kama namajeraha katika Mkono wake

 P. Diddy akiwa na Askari Polisi mara baada ya Kufikishiwa Taarifa

 Polisi wakichukua Melezo ya Ajali hiyo

 Utaratibu wa Kulichukua gari hilo kutoka katika eneo la Tukio ukiendelea

Didy akiwa Amepata Ahueni baada ya Ajali hiyo

LIBYA HAKUKALIKI

4:48:00 AM Add Comment

BAN WALID, Libya
Serikali ya Libya imetangaza kuwa makundi ya wapiganaji wanaoiunga mkono serikali yameudhibiti mji wa magharibi wa Bani Walid uliokuwa ngome ya wafuasi wa Kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi. 

Wapiganaji wanauinga mkono serikali wengi wao wakitoka mji wa Misrata wamekuwa wakikabilina na wafuasi wa Gaddafi kwa siku kadhaa, mapigano ambayo yamewalazimisha maelfu ya watu kukimbia mji huo mwezi huu. 

Serikali ya Libya imesema mapigano yamesitishwa na kwamba vikosi jeshi la nchi hiyo vitadhamini usalama wa mji huo na kusimamia operesheni ya kutoa misaada. Omar Baoughdad kamanda wa wanamgambo wa Misrata amesema, vikosi vyake vitaendelea kubakia Bani Walid kwa lengo ya kuyafukuza magenge ya wafuasi wa Gaddafi.

Mji huo uliopo umbali wa kilomita 140 kusini mashariki mwa mji mkuu Tripoli ulikuwa ngome ya mwisho ya dikteta Muammar Gaddafi aliyepinduliwa na kuuawa nchini Libya mwaka uliopita.


SUDAN : UN TAFADHARI......

4:43:00 AM Add Comment

KHARTOUM, SUDAN.
Sudan imelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kulaani hatua ya Israel ya kukiuka ardhi yake na kushambulia kiwanda cha silaha mjini Khartoum.

Waziri wa Habari wa Sudan Ahmed Bilal Osman jana alisema kuwa, ndege nne za kivita za Israel zilishambulia kiwanda cha Yarmouk Jumanne usiku na kwamba watu wawili waliuawa.

Daffa-Alla Elhag Ali Osman Mwakilishi wa Sudan katika Umoja wa Mataifa amesema shambulizi hilo ni ukiukwaji wa wazi wa makubaliano ya umoja huo ya  kuimarisha amani na usalama duniani na ametaka hatua hiyo ilaaniwe kimataifa.


CONFIRMED: H.BABA AMFANYIA KWELI FLORA MVUNGI

3:59:00 AM Add Comment
 H.Baba akimvalisha Pete ya Uchumba Mpenzi wake wa Muda Mrefu Flora Mvungi
 
 H.Baba akipeana Mkono wa Pongezi sambamba na Kusalimiana na Ndugu na Jamaa waliohudhuria katika Tukio hilo Muhimu na la Kipekee
 
 Flora Mvungi kabla ya Kuvalishwa Pete ya Uchumba na H. Baba
 
 Ndugu Jamaa na Marafiki waliohudhuria katika Tukio hilo muhimu
 
Mkono wa Pongezi na Salam ukiendelea

(Picha zote kwa Hisani ya Mpekuzi)


HAYA HAYA...KWANI ILIKUWAJE?



ULE uchumba uliodumu kwa muda mrefu kati ya mastaa filamu na muziki wa Bongo Fleva nchini, Hamis Baba ‘H. Baba’ na Flora Mvungi umefikia pazuri baada ya H – Baba kumtolea mahari na kumvalisha pete ya uchumba.
Tukio hilo lililokuwa na mvuto wa aina yake lilichukua nafasi siku chache zilizopita, katika Ukumbi wa The Atriums Hotel, Sinza – Afrika Sana, Dar na kuhudhuriwa na ndugu wa pande zote mbili.

 SASA H.BABA SI NDO HUYU ANAFUNGUKA SASA?

“Namshukuru sana Mungu kwa kuniwezesha kufanikisha tukio hili, japokuwa gharama ilikuwa kubwa lakini niliweza kujitutumua mwenyewe bila kuomba mchango kwa mtu yoyote.....Alisema H baba  na kuongeza kuwa....

“Jambo kubwa ninalotamani litokee na ninaamini litafanikiwa ni kufunga ndoa na Flora wangu. Ninampenda sana na nina uhakika na uchaguzi wangu.”H-BABA


 NA MASTAA WALIOHUDHURIA JE?

Baadhi ya mastaa waliohudhuria ni pamoja na Baby Madaha, Kulwa Kikumba ‘Dude’,  Hisani Muya ‘Tino’, Jacqueline Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Husna Idi ‘Sajenti’ na Wilson Makubi aliye Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF).

MNADA BANNER