REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WATU WA MUNGU !!! NAY WA MITEGO ANATAKA KUUWASHA MOTO MWINGINE WIKI IJAYO?

2:11:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
#WatuWaMungu NAY TRUE BOY ambaye hivi Majuzi tu kauwasha Moto kwa Kuachia Track yake mpya ya MOTO, inavyoonekana yuko tayari kuuwasha Moto Mwingine Tena

Kupitia Instagram account Yake, Nay alitoa Kionjo ambacho kilikutana na Comments Kibao ambacho kiliashiria kabisa anytime hasa Wiki Ijayo, anaweza akashusha Mkwaju Mpya, endapo baadhi ya Watu watakubali ifanyike Hivyo

Nay ambaye hivi sasa anamiliki studio yake ya FREE NATION, aliandika Hivi
" Wananchi Ongeeni na Hawa Wahenga ISIHACK na BILLAL SAADAT kama Vipi Mi Niwarushe Watu Next Week"


HUWEZI AMINI !!! : UNAMKUMBUKA YULE ANNA WA KWENYE FILAMU YA PREDATOR?.. HUWEZI AMINI ANAVYOFANANA SASA HIVI AISEE

1:46:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Wengi sana Enzi zetu tulifuatilia ile Filamu ya ARNOLD SCHWARZENEGGER inayoitwa PREDATOR...au mmeshasahau?

Sasa katika Filamu hiyo, Kuna Avctress ambaye aliwateka wengi hisia kwa kuwa karibu na lile Predator... yeye anaitwa ANNA

Hivi Umeshamuona anavyofanana sasa hivi< licha ya umri kwenda, lakini bado ni Mrembo Haswa !!!



REDSAN: MAPROMOTER WENGI HAWAWEZI KUNILIPA, NDIO MAANA SINA SHOW NYINGI NCHINI KENYA

1:35:00 AM Add Comment

KENYA   
#WatuWaMungu Msanii SWABRI MOHAMED maarufu kama REDSAN ameamua kuuvunja ukimya kuhusu hatua ya Waandaaji wa Matamasha Nchini Kenya kutokumhusisha ama kutokumpa chance katika Matamasha yao

Redsan ambaye amekuwa katika Soko la Muziki wa Kizazi Kipya Afrika Mashariki kwa Takriban Miaka 15, amedai kuwa ni kweli kuna baadhi ya Wasanii wenzake Nchini Kenya ambao hufanya Shows mara kwa mara Ndani ya Kenya, lakini yeye imekuwa ni Ngumu kwa sababu ya gharama ambazo anatakiwa Kulipwa.

Hitmaker huyo wa BADDER THAN MOST ameongeza kuwa, waandaaji wengi wamekuwa wakishindwa kumpata kwa sababu ya Masharti magumu hasa katika Malipo kutokana na mkataba wake na RECORD LABEL yake ya Kimataifa ya SONY GLOBAL

Record Label yake hiyo imekuwa ikitoza Gharama Nyingi sana kwa wanaohitaji Show na yeye, na hiyo ni kutokana  na namna ambavyo wanawekeza katika Muziki wake

TUNAMNUKUU   
"Unajua, Vitu vingi sana vimebadilika tangu miaka kdhaa iliyopita. Moja ni kwamba nimesaini mkataba na SONY GLOBAL ambao wananimanage kwa hivi sasa. Ukinipigia kwa ajili ya show hivi sasa, makubaliano ya mkwanja na Management yangu yako juu kwa sababu wamewekeza sana katika muziki wangu na mie mwenyewe na  Mapromota wengi wa Kenya hawajawahi kukutana na mahitaji haya. Mapromota wanaweza kuwekeza sana kwa wasanii wa nje hata kama wasanii wazawa wahapa tunazalisha muziki wa Ubora ule ule. Ni kwa sababu hii kuwa napata show chache hapa nyumbani, lakini nje ninapata Nyingi sana sababu wanaweza kukidhi hali yangu kimasoko."




AIBU ETI EEH !!!? : MARIAH CAREY AKUTANA NA JANGA HILI WAKATI AKIFANYA SHOPPING

1:12:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Mariah Carey ni Moja kati ya Wasanii wa Kike wakongwe ambao mpaka hivi sasa wanasadikika kumiliki Mkwanja Mzuri tu, ingawa hakuwa na namna ya kuepukana na Aibu hii !!!

MARIAH alijikuta akikutana na aibu baada ya Credit Card yake kukutwa haina kitu wakati akifanya Malipo ya Shopping aliyoifanya.

Mkali huyo wa Mkito wa "WE BELONG TOGETHER" alikuwa akijiachia vya kutosha kwa moja kati ya Designers wa Mavazi ya gharama haswa, na maduka Mengine, lakini kwa bahati mbaya alipokuja kufanya malipo kupitia CREDIT CARD yake, "muamala" ulizingua na hakukuwa na mkwanja wa Kutosha

Baada ya kubaini kuwa tayari Kimeshanuka, Msaidizi wake ambaye alikuwa ameambatana naye anayefahamika kwa jina la STELLA BULOCHNIKOV aijitahidi kutatua jambo hilo ili kufuta aibu hiyo, lakini baadaye ilibainika kuwa zoezi lingechukua Muda Mrefu kidogo na wangejichoresha haswaaa

Chanzo ambacho kilikuwepo eneo la Tukio, kinafafanua kuwa, wakati hali hiyo inatokea, Mariah aliamini kuwa kuna tatizo la kitknolojia labda ambalo limesumbua, hivyo akaamua kwenda eneo lingine kwa ajili ya manunuzi.

lakini baada ya kufika Duka lingine, alikutana na janga hilo hilo, na ndipo ilipokuja kubainika kuwa hakukuwa na mkwanja katika Crediot Card yake, hali iliyomuacha Mariah Carey katika hanya hanya za kutosha asiamini kinachotokea..

Hata Hivyo, mmoja kati ya wahusika wa Duka lingine anadai kuwa, Mariah alijihisi kuaibika kupita maelezo huku akikutanan na Jamba jamba za kutoka Nje ya Duka maana kulikuwa na wapiga Picjha kibao waliokuwa wakimsubiri kwa hamu na kutaka kujua nini kimemtokea mpaka akakutana na Aibu hiyo

BASI SAWA !!!! : HATIMAYE CELINE DION AMEPIGA PICHA AKIWA "MTUPU" KWA AJILI YA JARIDA LA VOGUE

12:57:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
#WatuWaMungu Licha ya kuwa na Miaka 49 kwa Hivi sasa, Hatimaye Mwanamama Celine Dion amekubali kuzivua Ngupo zake zote na kubaki Mtupu kwa ajili ya Picha za Jarida la Vogue.

Hit Maker huyo wa My Heart Will Go On, amekuwa ni Mwanamke ambaye kuupata Utupu wake kipindi cha Nyuma, ni jambo gumu sana lakini Safari Hii ameamua kuzichojoa kwa ajili ya Jarida hilo maarufu sana Ulimwenguni Kote

Katika Picha ambayo ilipostiwa Rasmi siku ya jana katika account ya Instagram inayomilikiwa na Jarida hilo, Celine alionekana akiwa ameketi katika Kiti kwenye Chumba kidpogo, huku Magoti yake na Mikono yake ikiwa imeficha "sehemu Maalum" ambazo zinapatikana katika Mwili wake

Hata Hivyo, wengi hawakutarajia kitu kama hiki ingawa kuna baadhi wanasema hakina madhara kibiashara, licha kuna wengine wanakandia kitendo hicho ukizngatia ni mwanamuziki ambaye amekuwa akiheshimika sana miaka na miaka

MNADA BANNER