REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

SANAIPEI : SITUMII TENA POMBE KALI AINA YA TEQUILA TAFDHARI !! INATOSHA"

8:18:00 AM Add Comment
 
Na Joe Mwangi-KENYA 
SIJUI kama wengine huwa wanachukua uamuzi kama ambao ameuchukua huyu bibie ambaye ana ukongwe wake kutoka Nchini Kenya, SANAIPEI TANDE (Zamani alikuwa anajiita Sana)

Kama hukuwa unajua kuhusu hili, Jana SANAIPE alitimiza Umri wa miaka 33, tukimaanisha kuwa ilikuwa ni maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa, na hakuwa nyuma kushare ujumbe mzuri kwa waungwana ambao wanamzunguka na hasa mashabiki wake

Kupitia Instagram account yake, Sanaipei aliomshukuru mwenyezi mungu kwa kufikia hatua Nzuri ya kutimiza miaka hiyo 33 akiwa hai, huku akiahidi kuachana na matumizi ya vitu ambavyo kwa asilimia kubwa vinaweza kumrudisha nyuma

Bibi huyu ambaye aliuvuna umaarufu mkubwa kupitia Kolabo yake na JUA CALI-"Kwa Heri", ametangaza rasmi kuwa hivi sasa hatumii tena pombe kali (Tequila)

Tunamnukuu
 "Ninamshukuru Mungu kwa Miaka yangu 33 Leo. Amekuwa na atazidi kuwa MWAMBA wangu!. sasa, hakuna tena Tequila tafadhari. Nimemaliza"
 

KI-BEN TEN CHA BLAC CHYNA KIMESEMA KUWA HUWA HAWAVAI KONDOM WAKATI WA TENDO LA NDOA..NI MWENDO WA KAVU KAVU !!!

7:47:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi  
WATU WA MUNGU nina imani tunafahamu kuwa Ex-wa Rapper Tyga, Blac Chynna hivi sasa ana mahusiano Mapya na "ki-ben Ten" chake ikiwa ni baada ya kukumbana na kashfa ya kuvuja kwa Video yake ya Ngono hivi karibuni.


Sasa kama ulikuwa hujafahamu Vizuri, Boyfriend wake huyo anaitwa YBN ALMIGHTY JAY na ana umri wa Miaka 18 ilihali Blac Chyna ana miaka 29 na kwa hali ambavyo inaonesha, bwana mdogo anamiliki mpunga mzuri tu kama sio kutuoneshea kupitia social networks tu.


WIKI hii Bwana Mdogo huyu kaibua siri nyingine kuwa yeye na Blac Chyna Hawatumii Kondom piindi wanapokuwa wanafanya tendo la Ndoa, yaani maana yake ni kwamba huwa wanaenda "Kavu Kavu"

Tunamnukuu
" Huwa ninaenda kavu kavu. Huwa sivai mipira mie rafiki yangu. Nani afanye huo upuuzi?. Nisengefanya mapenzi na mwanamke kama ningekuwa naogopa yeye kupata Mimba"

KILICHOSIKIKA LEO KATIKA INTERVIEW YA MO MUSIC KUHUSU NAMNA AMBAVYO WASANII CHIPUKIZI KUTOKA MWANZA WANAVYORUDISHA TAARIFA TOFAUTI KUTOKA KWAO WANAPOKUTANA NAO, MUZIKI WAKE, MANAGEMENT YAKE MPYA, KUUMIZWA NA MCHUMBA WAKE

7:12:00 AM Add Comment

Na Rich Sam-Mwanza  
Msanii MO MUSIC ambaye hivi sasa anakiri kuwa na Bajaji katika Mikoa karibu yote ya Tanzania (yaani Nyimbo yake ya Bajaji iko Kila mkoa wa Tanzania) Siku ya Leo alipita Unyamwezini katika Studio za JEMBE FM 93.7 MHz-Mwanza, na kukutana na Interview katika kipindi "korofi" cha HIT ZONE

Katika Interview akiwa na Baba Juti pamoja na Natty E, Mo Music alizungumza Mengi hasa akitutambulisha kwenye Management yake Mpya ikiwa ni baada ya ile ya awali kumalizika katika Hali ya Mtafaruku kidogo.


Mo Music awali ameweka wazi kuwa Mwaka huu wa 2018, anatarajia kuachia Audio na Video takribani 8, hivyo mashabiki wake wanatakiwa kukaa tayari kwa ajili ya "mikwaju" heavy itakayofuatia.

Upande Mwingine, Mo Music ameweka wazi kuhusu namna ambavyop wasanii wenzake kutoka jijini Mwanza hasa namna ambavyo huwa wanafikisha taarifa tofauti na kile ambacho wanakikuta kwa wenzao walioko Dar Es Salaamu, kitu ambacho kinaonekana kuwakatisha tamaa kuwasaidia pindi wanapowahitaji

INTERVIEW FULL IKO HAPA

MAKUBWA !!!!!!!! : MSANII BOBBY VALENTINO KATIKA TUHUMA ZA UBAKAJI

7:36:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
WATU WA MUNGU mambo yanazidi kuwa makubwa sana ndani ya Mwaka huu wa 2018 ukizingatia bado ni Mapemaaaaaaaaa...kabisa aisee!

Baada ya kumaliza ile kashfa ya kumkimbia Kahaba ambaye alimtumia katika Starehe zake bila kumlipa, na siri ikafichuka kuwa kumbe yule ni Dume aliybadili jinsia na kuwa mwanamke, yameibuka mengineyo watu wa mungu dhidi ya Msanii Boby Valentino.

Bobby Valentino ambaye hivi sasa hana chochote katika soko la Muziki wa kizazi kipya Duniani, anatuhumiwa kumbaka mwanamke (jina limehifadhiwa) usiku wa Jumapili na tayari yuko Chini ya Upelelezi wa Jeshi La Polisi Nchini Humo

Taarifa za kipolisi kutoka katika jimbo la COBB COUNTY, Huko Georgia Marekani, mwanamke huyo kafungua mashtaka dhidi ya Hitmaker huyo wa SLOW DOWN hasa kwa kitendo hicho cha ubakaji ambacho ni kinyume cha sheria na haki za binadamu

Pia ripoti inafafanua kuwa, tukio hilo lilifanyika Nyumbani kwa msanii huyo, na taarifa zaidi zitatolewa mara baada ya uchunguzi kamili kukamilika

Hata Hivyo, Msemaji wa Bobby Valentino amejitokeza na kudai kuwa, kitendo anachokifanya mwanamke huyo, ni kutumia njia za uwongo ili kujipatia fedha, kitu ambacho Boby Valentino hakubaliani nacho na ni taarifa za Uwongo

TULICHOKISIKIA KATIKA INTERVIEW YA RASCO SEMBO KUPITIA JEMBE FM 93.7, KUHUSU DEEY CLASSIC, NGOMA YAKE NA MR BLUE KUTOKUPIGA HATUA, NA MENGINEYO

7:00:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
LEO Kupitia Interview na Kipindi cha HIT ZONE kinachomilikiwa na 93.7 Jembe Fm-Mwanza, Msanii Rasco Sembo amezungumza Mengi sana kuhusu Muziki wake hasa ikiwemo kuitambulisha Track yake Mpya inayoitwa "Changa Karata"

Akijibu maswali katika Kipindi hicho, Rasco sembo amezungumza namna ambavyo ukaribu wake ulivyo na Producer Deey Classic, ambaye wengi tunafahamu kuwa ni Meneja wake na amekuwa akimsukuma katika soko la Muziki kwa Njia tofauti

Ukiachilia mbali hayo, Pia Rasco amezungumzia namna ambavyo wadau mbali mbali hasa Wasanii Wenzake wanatakiwa kuelewa kuhusu comments zao dhidi ya kutokufanya Vizuri kwa Track ambayo amefanya na Mr Blue pamoja na Mo Music

Full Interview Hii Hapa

MCHUMBA WA BOSS ANADAIWA PESA HII...NAYE NI TONI BRAXTON

2:38:00 AM Add Comment
 
Na Baba Juti   
HIVI, Kwa Wewe Binti ambaye ni Mrembo, unatokea kupendwa na Mwanaume ambaye ana mihela kibwena, halafu anakuchumbia na kuonesha hadharani kuwa kwako amekufa ameoza, utafurahia au hautofurahia kuwa naye?

Kama kama hautofurahia mahusiano hayo, basi inabidi ujifunze maana linaweza tokea la kutokea kama ambavyo limetokea kwa Toni Braxton ambaye ni Mchumba wa Birdman ambaye ni boss wa CASH MONEY RECORDS LABEL

Kama utakuwa hujafahamu, Mamlaka ya Kodi Nchini Marekani, imetangaza Rasmi kuwa inamdai Toni Braxton Mkwanja wa Kodi ambao alikwepa kuulipa, ambao ni USD 780,808.29 sawa na Tsh 178,024,290.12 kuanzia mwaka 2015 mpaka hivi sasa

Kwa Mujibu wa Taarifa kamili kutoka katika Kitengo husika, Toni anadaiwa Kodi hiyo kutoka maeneo mawili na yo ni 
State of Californa
2015: $113,500.93
2016: $116,870.07
Federal
2015: $310,223.28
2016: $240,214.01
Sasa, hatujafahamu atalipa vipi mkwanja huo, wacha tusubiri

MJANE WA MOWZEY RADIO : NIMEKWAZIKA KABISA !!!!

3:33:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi- UGANDA  
HAKUNA kitu kinauma kama pale ambapo mtu anaamua kutumia kipindi kigumu ulichopo kwa ajili ya kutengeneza pesa ama kutengeneza jina lake, ama kutafuta Sifa  hasa kwa watu mbali mbali

Na kinachokera zaidi, ni pale ambapo anatumia maneno makali na ushahidi usio na tija ili aendelee kuwaaminisha watu na aendelee kukukandamiza ili aingize mpunga zaidi kwake

Moja kati Ya Blog Nchini Uganda (jina tunalihifadhi) imejikuta akimuudhi na kumkwaza LILIAN MBABAZI mzazi mwenzake na Marehemu Radio kwa kumuandama na kitu ambacho hakina ukweli hasa katika kipindi hiki ambacho bado anaugulia maumivu ya Msiba wa Mzazi mwenzake.

Blogger anayetumia jina la Scoop alipost Picha inayomuonesha Lilian Mbabazi akipiga Kinywaji na Marafiki zake, na kisha kukoment kuwa imekuwa ni mapema sana kwa Bibie huyu kula bata mapema

Tunamnukuu
"Lilian Mbabazi, Mjane wa Mowzey Radio akiwa Out anapiga kinywaji na KARITAS KIRISIMBI na Marafiki wengine. Sio mapema kwake kutoka out na kula Bata, au ni muda wa kusonga mbele?"

Lilian aliscreen Shot Comment hiyo kisha akaandika
"Ka Jambo Scoop, kuchukua picha za Tangu Mwaka 2016 na kuzipost Sasa Hivi... MUSWADDE NYO"


#DakaHiiFasta : BEHIND OF AVRIL KUVAA MIWANI YA MACHO....

2:35:00 AM Add Comment

Na Joe Mwangi  
UKIMUONA Avril kama uko Very serious , ukasikia sauti yake inakuita, halafu unapomaliza kuitika, anaomba angalau "akuchumu", basi kama utakataa, we nii mgumu kuliko wanaume wote Duniani

Urembo tunaouona kwa Binti Huyu mwenye taji  lake la kuitwa "Mrembo na Msexy" kutoka kwangu, kuna muda huwa unachagizwa na Mavazi yake, Umbile Lake, nywele zake, tabasamu lake, lakini Pia MIWANI zake

Sasa kama ulikuwa hujafahamu, Avril mwenyewe anazungumzia kile ambacho kipo Nyuma ya Miwani ambayo huwa anavaa sometimes, ili kuweka sawa kwa wale ambao pengine wanatafsiri kuwa huwa ni swagg tu na anaongeza urembo.

Kupitia Instagram account Yake, Avril Mwenyewe kaweka wazi kuwa, Kitendo chake cha kuvaa miwani ya macho, kisitafsiriwe kama ni Urembo, ila huwa anatatizo la macho (Myopic) na amekuwa akifanya hivyo mara kadhaa maana hiyo ndioyo tiba ya mwisho kwake

Ukiachilia mbali hilo, Avril akaongeza kuwa , amekuwa na tatizo hilo tangu alipogundulika akiwa mtoto mdogo

KULIKONI TENA !!!! :HAKUNA JAMBO LA KHERI KATIKA URAFIKI WA CHRIS BROWN NA BOW WOW...

1:50:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
KWA mujibu wa kile kinachoonekana na kusikika katika Video Mpya ya BOW WOW inayofahamika kwa jina la DRUNK OFF CIROC, na kile kinachojibiwa na Chris Brown, ni dhahiri kabisa kuna namana gani vipi kati ya wawili hao

Siku ya Jana, Bow Weezy aliachia Video yake Mpya ambayo tumeitaja hapo mwanzo huku ndani yake akisikika kulalamika namna ambavyo ukaribu wake wa Swahiba wake Chris BNrown umekuwa Mbali sana tofauti na Kipindi cha Nyuma ambapo wawili hao walikuwa wakionekana Ku-Hang out Pamoja

Katika moja kati ya Lines ambazo zinapatikana katika Track hiyo ya Drunk Off Ciroc, inaashiria kabisa kuwa BOW WOW, hafurahishwi na anahisi vibaya sana kuona kama Chris Brown hamjali tena, hayuko karibu naye, na wala hamjulii hali , kitu ambacho anajiuliza maswali mengi mpaka sasa

Mashairi hayo yako hivi
"Niliacha kufanya Show ili Nikuone Chriss
Siku ya Kwanza, mie na wewe tumepitia Mengi
Hata iwe vipi, siku zote utakuwa mdogo wangu
Na inaniuma sana tunapokuwa katika uma na bado hatusemeshani
Huu ni Uchizi
Tumekua watu wazima, hebu tuachane na haya masuala"

Baada ya kukutana na Kitu Hicho Chris Brown aliamua kujibu kile alichokiona, kwa kupost kipande cha mashairi hayo huku akiandika

"Nimechanganyikiwa... Uko sawa Bro?" 

MUNGUA OKOA JAHAZI !!!!! : WABUNGE NCHINI KENYA WALALAMIKA KUTUMIWA PICHA ZA UTUPU

3:26:00 AM Add Comment

Na Joe Mwangi  
INAWEZEKANA kabisa baadaye mambo ya Mitandao na hata matumizi yake Nchini Kenya, yaakanza kubanwa vilivyo kama ambavyo inafanyika Nchini Tanzania, na hii itakuwa Very Soon

Hii inatokana na hatua ambayo imeonekana kuwa "Chungu Kumeza" na haitoweza kuvumilika baada ya binti mmoja Nchini humo kufanya jambo "korofi " kidogo kwa Waheshimiwa Wabunge, bila kujali kuwa wao ndio wanaotunga Sheria

Wakiwa Bungeni, Baadhi ya Wabunge wa Kiume wameamua kutoa Malalamiko yao ya kutumiwa picha za Utupu kabisa kutoka kwa binti ambaye hajafahamika, kitu ambacho kimeonekana kuwasumbua na kuwakwaza kwa asilimia kubwa.

Mmoja wa wabunge alisimama na kutoa lawama zake kuwa inaonekana binti huyo anazo namba za wabunge wote wa kiume, na huamua kutuma Picha za Utupu ili kuwatega na hata kuwarubuni kitu ambacho hakistahimiliki kwa upande wao

Aidha mbunge mwingine alisimama na kusema kuwa, kwa mara ya kwanza alipotumiwa picha hizo na kuzifungua, ilimuwia vigumu sana kuendelea kuzitazama, na akasema pia kama akimpatia Mheshimiwa Spika azione, hawezi kuzitizama kwa macho hivi hivi, lazima awe amevaa kifaa maalumu ili kuona kama atapunguza makali


Ukiachilia mbali Mbunge huyo, mwingine alisimama na kudai kuwa, picha hizo zinazotumwa na binti huyo zilipoingia katika simu yake, zilileta mgogoro mkubwa sana katika Familia yake

Wabunge hao wameomba kuwa, iwapo utaletwa muswada bungeni kuhusu Sheria ya Makosa ya kimitandao basi ni vema wakashirikiana kuuweka sawa na kutilia mkazo zaidi katika makosa kama hayo ili kuepusha mengi sana

MWANAMKE ALIYEPIGWA NA MSANII TREY SONGS AKIRI KUWA, WATU WALIKUWA WAMESIMAMA WAKATI ANAPEWA KIFINYO NA HAWAKUTOA MSAADA WOWOTE

2:08:00 AM Add Comment

Na Rich Sam  
HATIMAYE Mwanamke ambaye alifungua Mashtaka dhidi ya Msanii Trey Songs kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi hadharani kisa  kaongea na mwanaume mwingine , ameamua kuweka wazi na kuanika namna ambavyo amejeruhiwa na Msanii huyo

Awali tulitoa Taarifa kuwa Trey Songs alifunguliwa mashtaka na Bibie ANDREA BUERA kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi katika upande wa Parking walipokuwa wakitoka kula bata, huku tatizo kubwa likiwa ni bibie huyo kuongea na mwanaume, yaani kwa tafsiri ya Fasta ni kwamba, kulikuwa na Ishu ya WIVU

Akiwa na mwanasheria wake, Andrea aliweka wazi maeneo ambayo amejeruhiwa FEBRUARY 18 wakati wanatoka kunako After Party ya NBA ALL STARS WEEKEND na kudai kuwa ameamua kujitokeza mbele ya umma kuweka wazi kilichotokea ili uwe mfano bora hata kwa binti yake ambaye ana umri wa miaka 7

Katika Maelezo yake huku akitokwa na machozi, Andrea ambaye alikuwa ameambatana na Mwanasheria wake LISA BLOOM alizungumza haya, tunamnukuu

" Nilikuwa nimehudhuria After Party hiyo na ndipo Trey alianza kunifokea, kunikaba na kunipiga mitama na kunipiga ngumi na hata kunipiga mpaka nikaanguka Chini."

Kitu kilichoonesha kumuuma zaidi, ni namna ambavyo watu walishindwa kutoa msaada kwake wakati zoezi zima la kipigo kutoka kwa HIT MAKER huyo wa BOTTOMS UP linaendelea, tunamnukuu tena

"Watu walikuwa wamesimama tu na wanatazama namna ambavyo ninapewa kipigo. Nilipoona hali imekuwa mbaya, nilichukua simu nimpigie mtu wa usafiri aje kunichukua, lakini alichukua simu yangu na kuipiga chini, halafu akachukua na simu yangu nyingine akafanya hivyo hivyo. Nililia sana katika Mshtuko mkubwa na nilitaka kwenda nyumbani

Nilijitahidi sana kwenda hosiptali kwa sababu aliniumiza sana, na hata nilipoamka usiku wa manane, bado nilikuwa nasumbuliwa na kumbu kumbu za ajabu na tukio lile"



MAKUBWA !!!: MTUHUMIWA WA KOSA LA UDHALILISHAJI KWA MWANAMKE KWA KUMSHIKA SEHEMU ZAKE NYETI AACHIWA HURU...KISA?

1:36:00 AM Add Comment

Na Joe Mwangi-KENYA
IMAGINE wewe ni Binti na umefanyiwa jambo la "Udhalilishaji" na mtu tena mbele ya kadamnasi, halafu hukumu inayotoka ni kwamba jamaa alokufanyia hivyo hana hatia....utajiskiaje?

Kutoka Nchini Kenya, Ndugu yetu anayetambulika kwa jina la ALEXANDER MBONDO, alifunguliwa mashtaka na binti mmoja (jina limefichwa) ya kudhalilishwa hadharani mnamo Mwezi April na September 2016 katika Jengo la FONTANELLA huko Mombasa tena kwa makusudi kabisa

Kwa mujibu wa Mlalamikaji, inasemekana kuwa, Bwana Alexander alimkamata Sehemu Za "Makalio na Matiti" mbele ya umati wa watu katika mazingira tofauti, kwanza ilikuwa ni Ndani ya Basi na mara ya Pili ilikuwa ni katika Duka ambalo linapatikana katika maeneo hayo, na jamaa alikamatwa baada ya binti huyo kupiga kelele

Akijibu tuhuma hizo, Alexander ambaye ni mtuhumiwa, alikana kumshika mwanamke huyo katika sehemu zake Hizo nyeti, ila akaiambia mahakama kuwa uzuri wa mwanamke huyo umekuwa ukimchanganya mpaka kufikia hatua ya kuanza kumtongoza ili awe Mke wake, lakini bibie alikuwa akigoma kwa asilimia kubwa

Tunamnukuu:
"Ninampenda Mwanamke huyu mpaka nahisi kufa, na siwezi kujizuia kumpenda kwa sababu ya Urembo alio nao. Niko Tayari kumuoa muda wowote endapo atakubali ombi langu la muda Mrefu"

Kauli hiyo ya Mbondo iliiacha mahakama Katika Butwaa, ukizingatia alishakaa mahakamani tangu mwaka 2016 kwa kukosa dhamana ya Shilingi za kenya 20,000

Katika Kujazia zaidi, Mtuhumiwa aliiomba Mahakama na kudai kuwa itakuwa haijamtendea haki kumhukumu kifungo chochote kwa kumtongoza mwanamke anayempenda, maana alichokionesha ni Hisia

Tunamnukuu
"Ninaiomba Mahakama iniachie Huru , ili niweze kutimiza azma yangu ya kumuoa mwanamke ambaye ni Pendo la Maisha yangu"

Baada ya kusikiliza kesi hiyo, Hakimu aliyekabidhiwa kesi hiyo, HENRY NYANKWEBA alidai kuwa, upande wa mlalamikaji haukutoa Ushahidi wa kutosha kuhusu kudhalilishwa kwa mwanamke huyo, hivyo akaamua kumuachia Huru Bwana Alexander Mbondo


AJALI KAZINI,AU?: JAMAA AMNG'ATA ASKARI POLISI NA KUMUAMBUKIZA UKIMWI

3:03:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
KUNA wakati unaweza ukatamani ujute kufanya kazi fulani hata kama ilikuwa ndiyo ndoto yako, hasa kutokana na hili ambalo limetokea na linakatisha tamaa kwa asililimia kubwa

Kutoka Eneo la KERICHO Nchini Kenya, Katika Mahakama ya Kericho, mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la MUTAI, mwenye miaka 30 anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa kumng'ata Askari Polisi katika Kidole Gumba na kumuambukiza VIRUSI vya UKIMWI

Kwa Mujibu wa mashtaka yalisyosomwa katika mahakama hiyo Mutai alifanya Tukio hilo alip[okuwa amekamatwa na Askari Polisi huyo mnamo February 27 Mwaka 2018 katika Eneo la kibiashara la KEBENETI majira ya Usiku

Taarifa zinaongeza kuwa Katika hali ya kujitetea kutoka katika Maumivu ya kukamatwa na Askari huyo, aliamua kuzamisha meno yake katika Dore Gumba la Polisi , hali iliyompa majeraha sanjari na kuambukizwa Virusi vya UKIMWI

Hata Hivyo, Mtuhumiwa alikana mashtaka hayo, Na askari Polisi yuko anaendelea na matumizi ya Dawa za kupunguza Makali ya Virusi hilo, na Kesi imepangwa kusikilizwa Tena MARCH 15,2018



HONGERA SANA !!!: NICK CANNON KAPOKEA PONGEZI NYINGI KWA HILI

2:38:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
NICK CANNON ameanza kuonesha namna gani anamthamini mwanamke na hasa Uzuri wake kupitia Projects mbali mbali ambazo huwa anazifanya na Very Soon tutarajie Album yake Mpya

Rapper huyu ambaye pia ni Mchekeshaji ambaye ni Mzazi mwenzake na Mariah Carey huku ndoa yao ikishindwa kudumu, ameandaa album Maalum aliyoipa jina la MODEL MUSIC ambayo itasheheni nyimbo kibao za kuhamasisha wanawake wajikubali hasa kimuonekano kuanzia nje Mpaka Ndani

Awali Nick Cannon ambaye mpaka hivi sasa anausherekea Mwezi wa Wanawake, alkuwa na mpango wa kuandaa kazi ambayo itamuhamasisha Binti yake huko mbeleni hasa kuhusu muonekano wake na uzuri ambao yuko nao

Lakini ukiachilia mbali Idea hiyo ambayo inaonekana kufanikiwa, Katika Video yake ya MOTIVATION, aliona ni Bora awashirikishe wanawake ambao ni Wazee akiwemo Bibi Yake mwenye alipokuwa amefikisha Miaka 99, ili kujenga tafsiri ya kile ambacho kinaitwa Uzuri na Urembo

Wengi wamepongeza sana Idea Hiyo ya Nick Cannon ahasa kuwatumia Wanawake Wazee tupu badala ya kuweka Mademu wakali wenye Figure Kali na kadhalika

JACQUELINE WOLPER: "NILIANZA MASUALA YA FASHION KABLA HATA SIJAINGIA BONGO MOVIE"

2:14:00 AM Add Comment

Na Baba Juti  
WENGI tumeanza kumfahamu Jacqueline Wolper kupitia kiwanda cha Filamu hapa Nchini Tanzania, maarufu kama Bongo Movie, lakini yeye mwenyewe anathibitisha kuwa kuna jambo lingine ambalo amekuwa akilifanya hata kabla hajaingia Katika ulimwengu wa Filamu hapa Nchini tanzania

Akizungumza weekend hii katika Ukumbi wa King Solomon alipokuwa ameenda kwa ajili ya Shughuli ya Usiku wa The Vikings, Wolper alisema kuwa haonekani sana katika Bongo Movie kutokana na shughuli zake za Ujasiliamali ambazo ndo hizo tunazoita Fashion

Wolper ambaye hivi sasa anaitwa WOLPER STYLISH, amedai kuwa alianza kuonesha dalili za kuwa mtu wa Fashion wakati yupo Shule na aliwahi kubuni vazi lake mwenye ambalo lilikuwa na Material ya Mifuko Ya Rambo

Na alipofika uraiani, akagundua kuwa watu wanapenda kile anachokifanya katika Mavazi, akaona ni Bora aendelee tu

MSIKILIZE HAPA

SIRI IMEFICHUKA !!! : KUFULIA KWA KRI HILSON, BEYONCE NA CIARA WANAHUSIKA

1:48:00 AM Add Comment

Na HEZRON MUNISI
#WatuWaMungu Siri taratibu zinaanza kufichuka hasa kuhusu kile ambacho kilimfanya Keri Hilson apotee kwenye muziki na vitu vyake kutokusonga vizuri

Kipindi cha awali kidogo tulikupa taarifa kuwa Keri Hilson aliamua kuweka wazi kuhusu yeye kukutana na anguko kubwa sana lenye kishindo kizito kimuziki, huku akifafanua kuwa Kuvunjika kwa mahusiano yake yaliyodumu kwa miaka 11 lakini pia kukutana na vidole vingi vya watu na hata kupewa pressure kubwa na watu wanaomzunguka vilikuwa ni chachu kubwa ya kuanguka kwake

Lakini bwana, kumbe kuna jambo lingine ambalo kama tulikuwa hatulifahamu, basi na tulifahamu lkeo kupitia hapa hapa Ndugu zangu.

Bifu zito lililokuwepo baina ya Keri Hilson na Mwanamama Beyonce pamoja na CIARA, ndivyo pia vilichangia bibie huyu kuamua kukaa kimya maana lilimuathiri kwa namna kubwa sana

Ishu Iko Vipi sasa wakubwa wa kazi, Kunako Kipindi cha Mwaka 2007 mpaka 2011, Keri Hilson alikuwa anatarajiwa huku akitengenezewa mazingira ya kuwa Msanii Bora na Malkia wa muziki wa RnB kutokana na uwezo ambao aliouonesha katika Vitu mbali mbali

1. KUWA BACKGROUND ARTIST WA WASANII MBALI MBALI
Uwezo mkubwa wa kuimba wa Keri Hilson, ulimfanya akawa Background wa wasanii wengi sana akiwemo CIARA, KELLY ROWLAND, USHER, LUDACRIS, BRITNEY SPEARS, TONI BRAXTON na wengineo Wengi sana. hii ilimtengenezea mazingira makubwa ya kuitwa Malkia Mtarajiwa wa RnB

2. KUANDIKA NYIMBO KADHAA ZILIZOHIT
Keri Hilson aliandika mikwaju kadha wa kadha ya wasanii ambayo ilihit kwa asilimia kubwa. Mfano RUN AWAY LOVE ya LUDACRIS Feat. MARY J BLIDGE, TAKE ME AS I AM ya MARY J BLIDGE, LIKE A BOY ya CIARA, ICE BOX ya OMARION, GIMME MORE ya BRITNEY SPEARS, WAIT A MINUTE ya PUSSY CAT DOLLS na nyinginezo kibao

3. KUANDAA SOUND TOFAUTI
Keri Hilson akifanya kazi na Timberland, walifanikiwa kutengeneza sound mpya kabisa na ya kipekee ya muziki wa RnB huku bibie huyo akiwa ni mmoja wa wasanii ambao waliandaa melody nyingi tamu na nzuri zaidi. Uzuri huo ulimfanya apewe kolabo nyingi sana na hata kutengeneza jina kubwa

Lakini sasa, Kuna kitu kilikuja kutokea ambapo inasemekana Tabia ya Keri Hilson ilianza kubadilika huku akionesha dhaihiri kuwachukia baadhi ya Wasanii na hata kuleta Pozi za hapa na pale.

Katika hilo, Keri alianza kutajwa kuwana Beef na Wasanii BEYONCE, RIHANNA na CIARA. Katika hilo, Keri aliwadiss Ciara na Beyonce katika Track ya TURN ME ON Remix, huku Beyonce naye akirusha Dongo zito kwa Keri Hilson kupitia TRACK ya DIVA....

Baada ya hilo kufahamika, madongo yalianza kurushwa huku na kule, na mpaka hivi sasa, weekend hii, Keri Hilson aligusia hilo hilo pia kuwa katika sehemu ya kuwa na Msongo wa Mawazo

NI KWELI EX-MCHUMBA WA RICK ROSS AMEFULIA MPAKA KUSHINDWA KURUDISHIA "KUCHA" BANDIA?

1:45:00 AM Add Comment

Na Rich Sam
Wazee Wa Kazi tunafahamu Fika kabisa kuwa Hivi sasa Rapper Rick Ross anaendelea Vizuri na hali yake ikiwa ni baada ya kuugua weekend iliyopita na kupelekwa hospitali, lakini hilo bado haliwapi wengine ukimya wa kufunga midomo yao na hata kutengeneza Info kupitia Big Boss huyu wa MMG.

LIRA GALORE, Ex Mchumba wa Rapper Rick Ross, naye ameamua kuanzisha la kwake kunako mitandao ya kijamii na kutoa taarifa kuwa bado anayo ile pete ya Uchumba aliyovalishwa na Rick Ross

Ingawa kuna mastaa wengi ambao wakiwavalisha Pete za Uchumba wanawake wanaowapenda, na ghafla wakaachana, basi piga ua, kama pete ni ya gharama, lazima kesi itafunguliwa tu ili madini hayo yarudishwe haraka iwezekanavyo

Uchokozi wa kujua kuwa Pete bado yuko nayo, ulianza pale ambapo Bibie huyu alianza kuandamwa kuwa tangu ameachana na Rozay, hivi sasa amefulia kiasi cha kushindwa kubandika kucha nyingine ya bandia ambayo ilionekana imeng'oka katika kidole chake kimoja cha mkononi


Kama ilivyo wataalamu wa Kuzoom, walipoona kabisakuwa Bibie huyo kama kidole chake kimoja kilichoshika POWER BANK hakina kucha, ndipo walipoamua kuzoom kile kidole na kugundua kuwa ni "Kucha-less" na hata ile Power Bank ni ya bei rahisi sana.

Katika kukazia zaidi, walidai kuwa kufulia kwake kunatokana na yeye kuachana na Rozay ambaye inaonekana alikuwa anamuweka Mjini

ILI kujibu tuhuma hizo, Ex Mchumba wa Rozay, Lira, aliamua kusema kuwa , wakati anapiga picha hiyo alikuwa afrika Kusini mbugani, na ndipo kucha hiyo iliyotoka, hivyo hawezi kushindwa kununua Kucha ya USD 7 ili arudishie katika kidole chake.

Na katika kuongezea, Bibie huyo alidai kuwa asitafsiriwe kama aliyefulia, maana hata Pete ya Rozay aliyovalishwa mwaka 2015 inayoigharimu USD 350,000 bado anayo , hivyo anaweza akaiuza na akapata mpunga

MEGHAN TRAINOR: HATA UWE NA MPENZI WA MAISHA YAKO, STRESS ZIKO PALE PALE KAMA ILIVYOKUWA KWANGU"

1:17:00 AM Add Comment

Na Rich Sam   
MEGHAN TRAINOR aliwahi kuwa sehemu ya Tabu kubwa katika ulimwengu wa Muziki wa Pop ulimwenguni baada ya kuwaimbisha watu karibia Lyrics zake zote za Mkwaju wa NO

Ukiachilia mbali kufanya Vizuri katika upande huo, pia alifanikiwa kugusa vipengele kadha wa kadha kwenye tuzo kubwa tu Duniani kama vile GRAMMY, BILLBOARDS AWARDS, na nyinginezo, huku akiibuka na kadhaa ambazo zilimpa jina kwa asilimia kubwa

Lakini kama ulikuwa hufahamu, licha ya kuwa na Furaha katika sekta hiyo na sekta ya mahusiano ya kimapenzi mpaka kufikia kuvalishwa pete ya uchumba na kuandaa mipango kadha wa kadha ya ndoa, Megan Trainor hatokuja kusahau kipindi kigumu alichopita hasa cha msongo wa mawazo, hali ambayo yeye binafsi anadai hajui ilikotokea

Katika hali isiyo ya kawaida, Hitmaker huyo wa NO anadai kuwa, alishindwa kujua mambo hayo yametokea wapi maana alikuwa ana maisha mazuri tu, na wala hakuwahi kujua kama itafikia muda atakuwa anakata tamaa katika baadi ya vitu hasa ambavyo vina faida kubwa katika maisha yake

Baada ya kugundua hilo, Meghan Trainor anadai kuwa ilikuwa ikimpa wakati mgumu sana hali hiyo, hivyo akaamua kuingia katika eneo husika kwa ajili ya tuba na hata kuwa na madaktari maalum wa kumuangalia

   TUNAMNUKUU    
"Yah, nilishuka sana Chini na ndio nikaamua kwenda kwa watatua matatizo ya akili maana ukikaa kimya, ndivyo mawazo yako yanazidi kuwa mepesi zaidi. Hata kama ukiwa na mpenzi wa maisha yako ambaye anazunguka na wewe kila siku na anafanya kila kitu kwa ajili yako, bado utakuwa karibu na mawazo yako na wala huwezi kumuambia giza linalotanda katika Fikra zako"

MKATO WA SIKU: H CHRISS x COYO- HATUJIELEWI (VIDEO)

12:44:00 AM Add Comment

Na Baba Juti   
LEO ni Jumatano, na kama ilivyo siku zote, tunachukua "Chance" ya kupitia na kushare na nyie Mikwaju Mikali ambayo wasanii mbali mbali wa Mwanza wanakuwa wanaiachia ili kutoa support na kuelekeza kile wanachokifanya, kwa wale ambao ni wadau wa Muziki

Jumatano ya Leo "tunakunjua" Video ya H-CRISS WA KITAA inayoitwa "HATUJIELEWI na katika Upande wa pili , anasikika Rapper mwenzake COYO ambaye alipewa ubavu wa "Collaboration" katika Track Hiyo

AUDIO Imepikwa OVER THE CLASSIC mkono ukiwa ni wa Engineer DAY DREAMS (Himself) lakini Video imenyongwa na Director VIPPER

Mpaka tunaiweka hapa, Video hiii ambayo imekuwa Uploaded katika Youtube Channel ya HCriss, mnamo Januari 21 mwaka 2018, ina VIEWERS 3744 tu.

Itazame hapa na utoa Comment yako :

DAYS OF THE YEAR: 07TH MARCH-BE HEARD DAY

12:28:00 AM Add Comment

DAYS OF THE YEAR
Small businesses have many challenges to be successful. It can be an exciting experience to start a business and do something that you love. The reality comes in getting your message out and bring the paying customers in. Getting marketing advice can be an expensive proposition and every penny counts to a small business. Be Heard Day is the day to make things a little easier!
History of Be Heard Day
The task of getting the message of a small business through all the noise of bigger companies and their marketing machines could be described as herculean. Local and small businesses are sometimes not even noticed by those who live near them because of this. Marketing and Business Strategist Shannon Cherry saw this problem and decided to do something about it. She created Be Heard Day in 2004 and since then has been making a difference to many small business owners.
Her goal for Be Heard Day reportedly is to make it a “give away day”, a day where she and other business and marketing professionals offer their services and knowledge for free. How amazing this that? Being able to get advice from these professionals could mean the difference between complete failure or shinning success for some small businesses!

How to Celebrate Be Heard Day
There are some great ways to celebrate Be Heard Day and it doesn’t matter if you own a business or not! If you are a business owner, the best way for you to celebrate is to grab your favorite search engine and get to Ms. Cherry’s site for this year and sign up! The ability to receive thousands of dollars’ worth of advice is too good to pass up!
Another way to celebrate is to make time to sit down and objectively look over the marketing plan you are currently working with. See if you are being creative enough to cut through all the other marketing going on in your area. Should you try to use different types of marketing? These questions and more that she offers can lead to greater success!
Don’t own a business? Don’t worry! You can celebrate Be Heard Day and have fun at the same time! Grab the family and get out on the town! Find those small businesses in your community that you haven’t had time to stop into yet. Have a fun day of shopping and helping to support your community. Learning where these great businesses are is only part of the fun. There is nothing better than a great day of shopping, and seeing friends along the way. Ok, maybe there is… you could make new friends as you check out the shops!
Consumer or Owner, Be Heard Day is a great time to make connections. Thanks to Shannon Cherry, there are many options for advice that previously may not have been available to those who are following their dream running a small business. Be a part of the day and post on social media using #BeHeardDay to show how you are taking part!

BOBBY BROWN" NATAMANI NICK GORDON ANGEFUNGWA MAHALI AMBAKO KUNA MTU ANAMLAWITI

2:31:00 AM Add Comment

Na Hezron Munisi  
WatuWaMungu Bado Bobby Brown ana hasira na NICK GORDON, kijana aliyesababisha mauaji ya binti yake BOBI KRISTINA, ambaye alizaa na Marehemu Whitney Huston.

Kama utakuwa unakumbuka Vizuri, Mwaka 2016, Nick Gordon ambaye pia ni mtoto wa Kuasili wa Whitney Huston, aliamuliwa na mahakama kulipa USD Milioni 36 kwa familia ya Bobi Kristina baada ya kubainika kuwa ana hatia juu ya hilo, lakini bado Biby Brown ni kama hajaridhikia.

Hali hii inatokana na kauli yake ya kusema kuwa anaona kabisa kuwa bado mahakama haijatenda haki juu ya Marehemu mwanaye sababu bado Nick Gordon anazidi kuzurura mitaani tena akiwa huru kabisa, kitu ambacho kinamuuma kwa asilimia kubwa sana

Kilichokuja kudhihirisha zaidi kuwa Bado Boby Brown ana hasira juu ya Kijana huyo, ni kauli yake nyingine ya kudai kuwa Kijana huyu alitakiwa awe jela sasa hivi analawitiwa na wafungwa wake..lakini bado yuko huru.

Namnukuu
"Ni Kwa Sababu yuko Huru mtaani na anazunguka tu. Haki?. Kama angekuwa amefungiwa sehemu ambako mtu yeyote angekuwa anamlawiti. Hivyo ndivyo ninavyohisi. Alinilawiti kwa kunichukulia mtoto wangu"

HATIMAYE ASHANTI KATHIBITISHA KUWA NELLY ALIMSALITI

1:58:00 AM Add Comment


Na Rich Sam  
WATU Wa Mungu ni nani ambaye anabisha kuwa "Mapenzi" yanauma kuliko kawaida na hata inaweza ikasababisha madhara makubwa sana

Na Tunaimani kabisa, ukishaingia katika mahaba na mtu fulani hata kwa miaka kadhaa, halafu ikatokea mkakatisha safari yenu ya mahusiano, lazima kuna mmoja ataumia kidogo, na kuna mmoja ataumia sana

Hii ndiyo inayooonekana hivi sasa kutoka kwa mamito Ashanti ambaye kipindi cha nyuima alikuwa katika "Mahaba Mazito" na Rapper NELLY ambaye ni Hit Maker wa Track ya Dillema. Wengi tunajua kuwa Kila mtu ana maisha yake ya kawaida na mahusiano pia, ila kipindi cha nyuma walikuwa ni kama Kumbi kumbi

Si Ashanti wala si Nelly ambaye amewahi kuzungumzia kile ambacho kimewahi kutokea baina yao na hata kuvunja mahusiano yao, lakini Leo Tumefanikiwa kumnyaka mmoja wao ambaye ni Ashanti akikiri moja ya chanzo cha kuvunjika kwa mahusiano yao.

 Akiwa jukwaanini wakati anapiga Perfomance yake, Ashanti aluthibitishia umma kuwa amewahi kusalitiwa (Huku akimlenga Nelly ambaye sasa hivi ana mahusiano mapya) hivyo anayafahamu maumivu ya kusalitiwa na kuumizwa kimahusiano.

Ili kuthibitisha kuwa alikuwa anamlenga Nelly, shabiki mmoja alipiga kelele na kusema "F***CK NELLY" na kisha ASHANTI pale pale akajibu "WORD" yaani "Hilo Nalo Neno"

MNADA BANNER