REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WEEKEND YAKO YA LEO IFANYE HIVI:

5:51:00 PM Add Comment

Kuna Muda huwa Tunapata wakati mgumu sana Zinapoingia Siku za WEEKEND.

Kuna Muda Pia Stress huwa Nyingi Kila Inapotimia Siku ya Kwanza Ya Weekend

Na kuna baadhi ya watu huwa Tunaamini kuwa Weekend Bora ni Lazima uwe na Pesa Nyingi ama Ulewe kupita maelezo,ama Uspend Pesa Nyingi sana.

Lakini kuna jambo la Msingi ambalo natamani tulifahamu kwa hali na mali.

Tunatamani sana Uifanye Hivi Weekend Hii ambayo inaanza Leo.
·        Weka Mipango yako Vizuri
·        Jitahid Kukutana na Marafiki zako/ Wafanyakazi Wenzako
·        Jitahid kuzingatia mazingira ya Nyumbani..(fanya marekebisho ya Nyumba, mpangilio wa Ndani,nk)
·        Epuka Kulewa/Ulevi kupita Kiasi.
·        Jitahidi Kutoka Nje ya Nyumbani (kukutana namarafiki maeneo ya Uwazi)
·        Jitahidi kufanya Kitu Kipya Siku za Weekend
·        Epuka Stress/Mawazo Mengi Siku zaWeekend.

·        Jitahidi kujumuika katika Michezo/Shughuli za Michezo

WEUSI: NI PROJECT AFTER PROJECT.

6:45:00 AM Add Comment

DA ES SALAAM, Tanzania.
Moja kati ya Vibao ambavyo vinakubalika sana kutoka Kunako Kundi Hili la Weusi ni pamoja na NJE YA BOX, BEI YA MKAA na Vinginevyo ambavyo vimewafanya wakuchukua Tuzo ya KTMA-2014 katika Kipengere cha Kundi Bora.

Wakishusha One Of The Interview Kunako Kituo Kimoja chha Radio, Joh Makini ambaye ni Moja kati ya Membaz wa Familia ya Weusi amesema kuwa, kwa upande wao wanazingatia sana kufanya kazi kwa ushirikiano Mzuri na kwa Mpangilio Mzuri.

Pia Joh ameongeza kuwa, ubora wa Kazi zao, na kujiamini, ni kitu ambacho hakiwaogopeshi kuachia Projects zao ambazo huzitoa kwa Utaratibu maalum.

Pia Joh ameongeza kuwa, Weusi kama Weusi hawaaoni Kitu cha Kuwazuia kufanya Projects zao pamoja na kusukuma kundi ama familia yao kwa Pamoja, sanjari na kuingiza solo Projects.


Joh ambaye amewahi kuzigusa hisia za Mashabiki wengi wa Muziki wa Hip Hop Nchini kupitia Mikwaju kama Vile BAI BAI, SHOW ZA JOH, na nyinginezo kibao, amesma kuwa sasa hivi yeye na Nick wanatengeneza Project ya JOH MAKINI Vs NICKI WA PILI ambayo ni kazi isiyohuska na Kundi lao, na Inafanywa na Producers Tofauti

INASEMEKANA: DRAKE NA RIHANNA INAWEZEKANA WAMEACHANA

6:37:00 AM Add Comment

NEW YORK, Marekani
Kipindi Cha Nyuma Kulikuwa na Info za uhakika kuwa Drake –Dreezy na Robbin Fenty- Rihanna hivi sasa ni wapenzi.

Lakini KITENGO AMINIFU CHA CHIMBUA CHIMBUA kimeshusha Ripoti kuwa Kuna Taarifa zinazosambaa kuwa Rihanna na Mpenzi wake huyo Drake wamemwagana huku sababu ikisadikika kuwa ni MAHABA NIKANYAGE ya Drake kupita maelezo kwa Bibie Rihanna.

Aidha Kitengo hiki kimedai kuwa, kwa mujibu wa Info kutoka US WEEKLY, kuna chanzo kilicho karibu na wawili hao, ambacho kimemenika kuwa Drake anampenda kupindukia Rihanna, hali ambayo humfanya aonekane na Wivu hasa dhidi ya Mwenzi wake Huyo.

Aidha Chanzo hicho bado kimedai kuwa, Dreezy na Riri wamekuwa wakigombana mara Kwa mara, na Siku za hivi karibuni waligombana kwa mara nyingine.


Hata Hivyo wadakuzi wa mambo wanadai kuwa, Rihanna alionekana akiwa Peke yake katika GALA AFTER PARTY tofauti na Awali.

• SAKATA LA JAY Z KUPIGWA NA SOLANGE: KWA MARA YA KWANZA, HATIMAYE BEYONCE NA JAY Z WAMETOA TAMKO.. ALIYEVUJISHA VIDEO ATIMULIWA KAZI.

3:01:00 AM Add Comment

NEW YORK, Marekani
Baada ya Mengi kurindima huku kila mtu akiwa na sababu zake kuhusu ugomvi uliotokea baina ya Solange na jayz Katika Lift ya STANDARD HOTEL , na Video kuvuja, hatimaye Watatu hao, yaani Jay Z, Beyonce na Solange wametoa tamko kuhusu Kilichotokea baina yao.

Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewajana katika Mtandao wa AP (ASSOCIATE PRESS), Watatu hao wamedai kuwa hivi sasa wameshamaliza tofauti zao, na Kila kitu kinaenda sawa katika familia yao.

Taarifa hiyo inaeleza Kuwa, ni kweli tatizo limetokea, lakini wao pia ni familia kama Zilivyo nyingine, lazima Zitakumbana na matatizo hasa ya Misuguano.

Aidha Taarifa hiyo bado imesisitiza Kuwa, Kuachiwa kwa Video Footage katika Mitandao Mbali mbali ya Kijamii, kulileta Wakati Mgumu Kidogo hasa katika familia Nzima, lakini kwa sababu wanahitaji kuwa Bora, hawakuwa na Budi kumaliza Tofauti zao


Pia Jay Z na Solange walikubali kuwa Wote walisababisha linalotokea kuhusu familia yao, na wameamua kuwajibika hata kama Video hiyo imesababisha Madhara Gani kwa Jamii. Hivyo Wameombana Radhi, na Kila Kitu Kmeenda sawa, hasa kama ilivyokuwa Awali 

MNADA BANNER