REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

PROJECT STUDIO: KUTANA NA HARSHBASE RECORDS WAKIZUNGUMZIA STUDIO YAO NA NAMNA WANAVYOFANYA KAZI (AUDIO)

8:05:00 AM Add Comment

Na Baba Juti (@babajuti)
HARAKATI za Kufahamu Recording Studios ambazo zinapatikana Mitaa Mbali Mbali ya Jiji la Mwanza ndo Imeshaanza.

Dhumuni Kubwa ni Kuzipa nafasi Studio Hizi za Muziki kusikika, na hata kutambulika namna ambavyo wanafanya kazi.


Hii Pia ni kutoa Fursa kwa wao kuzungumzia Ugumu ama Changamoto wanayokutana nayo, bila kusahau undani wa Kile kinachofanyika katika Studio Hizo.

WIKI, Nimeweza Kutembelea Studio za Harsbase (Harshbase Records) zinazopatikana katika Mtaa wa BUZURUGA MITI MIREFU, Jijini Mwanza.

Wasikilize hapa


INAWEZEKANA ROCK TOWN IKARUDI KWA KISHINDO BAADA YA MABORESHO HAYA?

7:24:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
INAWEZEKANA Ujio wa ROCK TOWN RECORDS ukawa na Utofauti baada ya Kukaa Kimya kwa Muda Kadhaa, ikiwemo kutokuachia Kazi Yoyote Mpaka hivi sasa

Chanzo Cha Studio Hiyo Kukaa Kimya, ni pamoja na Kufanya Ukarabati na maboresho kwa ajili ya Wateja watakoifika hapo kwa ajili ya Kufanya kazi.

Tofauti na maboresho, Rock Town Records Chini Ya Mkurugenzi Wake, Mkubwa Hermidou, Imekuja na Project ya T-Shirt ambayo ina Logo Mpya kabisa na za kibunifu- ROCK TOWN RECORDS.



Katika Logo hiyo, Kuna Jiwe Maarufu linatambulisha Jiji la Mwanz\a (Bismark Rock) hali inayoifanya kuwa Tofauti na Studio Nyingi za Mwanza

LAKE ZONE FRUITS: OBBY HUYU HAPA TENA !!

7:04:00 AM Add Comment

Na BABA JUTI
Mdogo Wangu Huyu Hapa Tena, Anaitwa Obby, anakuja na Brand Track Baada ya Mkwaju wa TENA, kufanya Vema kunako Kanda ya Ziwa.

Mabile Kwa Mabwale, Get Ready, nab ado unaweza kuupata Mkwaju wake katika Website ambayo itakuwa Uploaded.
Pia Tembelea Blog Hii kuupata Mzigo Huu

#Support

HII NDIYO ZAWADI AMBAYO H BABA KAMNUNULIA MWANAE TANZANITE KATIKA BIRTHDAY YAKE

6:53:00 AM Add Comment

MSANII wa “Bongo-Bolingo Flava”, H BABA, amedai kuwa amempa Zawadi ya Kiwanja, Mwanae wa Kwanza, TANZANITE  ikiwa ni ndani ya Siku yake Maalum ya Kuzaliwa, yaani Birthday.


Kupitia Ukurasa wake wa Face Book, H baba anadai kuwa, Dhumuni la Kufanya hivyo, ni kumpongeza Mama Yake (Mke wa H baba-Flora Mvungi) kwa Kumvumilia.


Hiki Ndicho alichoandika:


“MWANANGU @tanzanitehbaba NIMEMPA ZAWADI YA #KIWANJA #MAENEO YA MBEZI BEACH CHENYE UKUBWA WA #52 KWA 44 ZAWADI HII NI YA #birthday YAKE YAKUZALIWA KWAKE NAMSHUKURU MAMA TANZANITEONE KWAKUNIVUMILIA KUPATA MSHANGAO WA KIWANJA CHA MWANAE #HAKUTEGEMEA #KIUKWELI MBEZI BEACH UWANJA SIO MCHEZO KWAWANAOJUA THAMANI YA ARDHI #WANAELEWA NINI NAMAANISHA #SIWEZI KUMPA MWANANGU ZAWADI YA GARI KWASABABU #BADO MDOGO PIA KIWANJA KILA ANAVYOKUWA NAKIWANJA KINAPANDA #THAMANI ILA GARI #LINASHUKA THAMANI #NAMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWAKUFANIKISHA HILI KUBWA KWA MWANANGU @tanzanitehbaba haya haya walee wa mbezi beach #JIRANI YENU MPYAA”

NOT THIS TIME AGAIN… CHRIS BROWN ANAFUNGULIWA KESI TENA YA KUMPIGA MWANAMKE?

6:34:00 AM Add Comment

LETS hope kwamba Kila Kitu kitaenda Fizuri kwa Baba Royalty Himsefu, Chris Brown

Mwanamke mmoja amemtaja Breezy katika mashtaka yake, kwa Kuhusika Kumpiga na kuharibu Simu yake, baada ya Kusukumwa kutoka kunako Bas Tour la Mkali huyo wa LOYAL

Kwa Mujibu wa maelezo ya Bibie huyo, anadai kuwa Tukio hilo lilitokea SEPTEMBA 14, ambapo Bus Hilo la Chris Bizzo lilipaki Nje ya Strip Club ama Club ya Akina dada wacheza Utupu, kipindi ambacho FETTY WAP, Breezy na French Montana walikuwa wakifanya Video.

Mwanamama Huyo anaendelea Kudai kuwa, Alijikuta akisukumwa kutoka Ndani ya Bus hilo, na Kuanguka Nje kisha Simu yake Kuharibiwa, lakini ni baada ya Kuambiwa Kuwa haruhusiwi kuingia Ndani ya Basi hilo na Vitu kama Kamera, ama Kitu chochote Cha Kurecord, sheria ambayo iliwekwa na Chris na Watu wake


Jeshi la polis nchini marekani, wanafanya uchunguzi Juu ya Tukio hilo, nab ado wanahitaji kufanya mahojiano na Baba Royalty pamoja na watu wake

RICK ROSS AMESHINDWA KUFUA DAFU MBELE YA LMFAO

6:30:00 AM Add Comment

THE BIG BOSS Kutoka Ufalme wa MMG-Rick Ross, Mwaka huu unaweza kumalizika kwa Kupigwa Chini katika Kila madai anayofungua, huku yale anayofunguliwa dhidi yake, yakimkomba Mkwanja Mrefu.

Kama Utakuwa unafahamu tangia Kitambo, Rozay alifungua Mashtaka dhidi Ya Kundi la Pop Nchini Marekani, LMFAO, kwa Madai kuwa wanatumia Maneno yake, ambayo ni EVERY DAY I’M SHUFFLIN, hivyo anawataka kuacha kutumia Swagg hiyo, maana inatokana na maneno yake ya EVERY DAY I’M HUSTLING kunako Mkwaju wa HUSTLING

Kesi Hiyo ilifunguliwa Mwaka 2013, ambapo Rozay alikuwa anadai kuwa, Yeye Peke yake ndo ana haki ya Kutmia kauli Hiyo, na kitendo cha Kundi Hilo la LMFAO kufikia hatua ya kuprint mpaka T-Shirt ya Slogan Hiyo, ni Ukiukwaji wa hakimiliki Yake.

Lakini Hakimu ambaye alikuwa anaendesha Kesi hiyo, alimkata maini kabisa Rick Ross kwa kusema kuwa, hakuna haki Miliki ya Neno Hustin ambalo Rozay analalamikia, hivyo Kesi hiyo haina Mashiko.

Katika Kufafanua zaidi, hakimu Huyo, Kathleen Williams, amesema kuwa, Wimbo wa HUSTLIN alioutoa Mwaka 2006, utabaki na Hakimiliki ya Wimbo kama Wimbo, na Sio Neno ama Kauli Mbiu.


Katika Kutoa Mifano, Judge William alinukuu Misemo kama Vile “Holla Back”, “We Get It Poppin” na Mengineyo, kama vitu ambavyo havina Copyright lakini Vinatumika na Kila Mtu

DULLY SYKES HATAKI U-TEAM KATIKA INSTAGRAM

2:54:00 AM Add Comment

Mtandao wa Instagram ni mtandao wa kijamii ambao umetokea kuwa na mashabiki wengi sana Tanzania hivyo wengi wanaamkia huko asubuhi mchana na mpaka usiku na kumekua na team zinatengenezwa kwa wale wenye mapenzi na watu flani.

Dully Sykes ametangaza rasmi hataki kutengenezewa team ya aina yoyote, anakubali mashabiki wenye upendo nae ila hataki mtu atengeneze team manake zinamtengenezea uadui na watu wengine pale team inapotumika vibaya.

TUNAMNUKUU
"Sitaki kuwa huko sababu nitatengeneza maadui, hawa wanaonisuppot kila siku nitabaki nao tu ila kama wataongezeka waongezeka kwa nguvu za Mungu na sio ushabiki wa kitimu."
"Timu za Instagram zimeharibu hali ya hewa sasa hivi, zamani sisi kulikua kuna makundi yanashindana kwenye bongofleva lakini sio kushindana kwa ugomvi, ni kazi inapigwa alafu baadae tunatembeleana, na kulikua kuna Camp ikiwemo Misifas Camp ya kwangu, pamoja na kushindana kote lakini tulikua tunakaa tunakula na kunywa pamoja”

Dully Sykes ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania ambao kwenye page zao za Instagram hawamfollow mtu yeyote, mwingine kwenye hiyo list ni Ali Kiba ambapo wote wanasababu zao kwanini imekua hivyo.

ET H.BABA, HAYA NI MALAPA YA AINA GANI?

6:16:00 AM Add Comment

HII nimekutana nayo katika Post yake ya Asubuhi, Kiasi kwamba natamani kufahamu aina ya Malapa ambayo H. BABA amevaa

INASEMekana muuaji wa mama wa kanye ni cousin wa kanye

3:20:00 AM Add Comment

BAADA ya kumfanyia Upasuaji, Siku iliyofuata, mama Wa Kanye West Alifariki, huku Daktari akibaki katika Wakati Mgumu hasa na Kupokea lawama za Kusababisha mauaji ya Bibi Huyo DONDA WEST

Hivi sasa Daktari Huyo, anamlaumu Binamu wa kanye West kwa Kusababisha mauaji hasa kwa Kumpatia Dawa ziszostahili


JB: MAREHEMU KUAMBIANA ALIKUWA CHADEMA..SITAKI UTOTO NIKITANGAZA KAZI ZANGU…

2:37:00 AM Add Comment

INAWEZEKANA Mashabiki wakawa wanakosea sana hasa pale wanapoamua kutengeneza kitu ambacho kiujumla hakitakiwi kuwapo katika mchakato mzima wa kuhusisha Burudani, na shughuli Nyinginezo.

Mkali kutoka Bongo Muvi, amejikuta “akijaa Povu” baada ya Mashabiki kadhaa kumfika pabaya na kudiriki kuhusisha Kazi zake na Suala la Siasa.

Mashabiki wa Soko la Filamu Nchini Tanzania, wamejikuta wakishindwa kwenda sawa na Jacob Steven, ikiwa ni baada ya Big Bos Huyo wa JERUSALEM FILM kupost Muvi Mpya ambayo Marehemu Adam Kuambiana ameshiriki, na Filamu hiyo inaitwa MAHABUSU.

Sasa, kilichotokea ni Watu Kuanza kumuambia kuwa, akauze Kazi Hiyo kwa Wana-ccm, ukizingatia kuwa Jb Yuko CCM.

Baada ya Kukerwa sana na hayo, JB aliwaka na kudai kuwa, Marehemu Kuambiana alikuwa Mwanachama wa CHADEMA Kuliko Wengi wao.

Pia ili kukazia Zaidi, JB amesema hataki UTOTO akitangaza Kazi zake, na kama haupendi , Piga Kimya

JB aliandika Hivi

NARUDIA TENA SIASA SIO VITA...MAREHEMU ADAM ALIKUWA CHADEMA KULIKO WENGI WENU..MPAKA ALIKUWA CAMPAIGN MANAGER WA MKEWE JANET KULE KAWE KWENYE UDIWANI...MBONA TULIKUWA TUNASHIRIKIANA???WASANI MBONA WENGINE WAKO UKAWA LAKINI BADO NI MARAFIKI...NINA NDUGU AMBAO WAKO UKAWA NA NYINYI PIA MNA NDUGU WAKO CCM MNAGOMBANA NAO????HAMSHIRIKIANI NAO????AU MME ONA SINEMA ZETU TU...VITU VYOTE MNAVYO NUNUA MADUKANI VIMETENGENEZWA NA UKAWA???ACHENI SIASA ZA KIJINGA..SITAKI UTOTO NIKITANGAZA KAZI ZANGU...KAMA HUPENDI PIGA KIMYA...

TIZAMA PICHA ZA MTOTO WA WILL SMITH, JADEN SMITH, AKIWA KATIKA MAHABA MAZITO NA KISHTOBE CHAKE

1:53:00 AM Add Comment








MUONEKANO MPYA WA KARRUECHE TRAIN, BAADA YA KUPIGANA CHINI NA BREEZY

1:31:00 AM Add Comment
 AWALI tulizoe Kumuona Karrueche Tran, ambaye ni Ex-Girlfriend wa Chris Brown akiwa na Muonekano wa Nyewle Nyeusi.

Lakini Ikiwa Imepita Muda Kadhaa baada ya kupigana Chini na Weezy, hatimaye amebadilisha Muonekano wake hasa wa Nywele


LIL WAYNE MAJANGA?. ANATAKIWA KULIPA DOLA MILLIONI MBILI.

1:17:00 AM Add Comment

blacktouchez.com
BAADA ya kudaiwa kuwa amepigana chini na Mpenzi wake Christina Millian, Leo Hii tunashusha Info Mpya ya Lil Wauyne Kuhusu kudaiwa “Mpunga” Mrefu ikiwa ni baada ya kuwepo kwa Kesi Dhidi yake, kuhusu Private Jet (Ndege Binafs)

Mnamo Mwezi August, kampuni ya Ndege Binafsi Nchini Marekani, SIGNATURE GROUP, walifungua Kesi dhidi ya Lil Wayne ikiwa ni kulipwa Mkwanja Wao ambao walikuwa wanamdai Mkali huyo aliyejiengua CASH MONEY RECORDS.

Kampuni Hiyo Ilimkodisha Lil Wayne Private Jet Hiyo kwa ajilio ya Matumizi yake, huku akitakiwa kulipa Mkwanja waliokubaliana, na Mwisho wa Siku mpaka July 2014 Wakati Kesi inafikishwa Mahakamani, Weezy alikuwa anadaiwa USD Mill 1.

Lil Wayne hakulipa Chochote, na Kadri Muda Ulivyozidi Kwenda, Ndivyo alivyokuwa akizidi kuongeza Deni Mpaka kufikia USD Milioni 1.8 (hiyo Ilikuwa ni kufikia August ya Mwaka Huu)

USD 200,000, ambazo zinakamilisha Idadi ya USD Million 2, ni ya kumlipa Mwanasheria.

Ingawa Weezy analalamika kuwa Hakukuwa na Mkataba wala makubaliano wakati wa Kukodishiana Ndege Hiyo, Bado hakimu kayatupilia Mbali Madai yake, Hivyo Piga , ua, Lazima Weezy “Atapike “ Mkwanja Huo bila Ubishi


LIST YA WATAKAOCHUANA KATIKA TUZO ZA BET HIP HOP AWARDS 2015 HII HAPA

12:16:00 AM Add Comment

HATIMAYE BET HIP HOP AWARDS 2015 imeweza kumimina List ya maninja ama Wasanii kutoka Nchini marekani, pamoja na wadau mbali mbali wa Muziki wa Hip Hop, watakaowania Tuzo hizo, ikiwa ni katika Vipengele Tofauti.

Safari Hii itakuwa ni Msimu wa 10 Kwa BET Awards, tangia wameanzuisha Utoaji wa Tuzo hizo, na Mwaka huu, atakayehost Mchakato Mzima, ni The Dog Father-Snoop Dogg.

“Best & Hot Female Rapper” Kutoka YMCMB-Nicki Minaj, ameonekana Kuwa Tishio zaidi hasa kwa Kutokea Takribani Mara Tisa Katika Category Mbali mbali ambazo zimepangwa.

Drake, Big Sean, Kendrick Lamar, Kanye West, na Wengineo, wameonekana kuingia katika Mchuano Mkali hasa Ukizingatia kila Mtu ana Uzito wa Kutosha Katika Mainstream.


Pia Djs, Na Website ambazo zimeweza kusupport Muziki wa Hip Hop, nazo zimewekwa kunako Mchakato Huo.
List Hiyo ni kama Ifuatavyo:

BEST HIP HOP VIDEO
  • Big Sean featuring 
  • Chris Brown & Ty Dolla $Ign - "Play No Games"
  • Big Sean featuring Drake & Kanye West - "Blessings"
  • Fetty Wap - "Trap Queen"
  • Kendrick Lamar - "Alright"
  • Nicki Minaj featuring Beyoncé - "Feeling Myself"


BEST COLLABO, DUO OR GROUP
  • Big Sean featuring Drake & Kanye West - "Blessings"
  • Big Sean featuring E-40 - "Idfwu"
  • Fetty Wap featuring Monty - "My Way"
  • Nicki Minaj featuring Beyoncé - "Feeling Myself"
  • Nicki Minaj featuring Drake & Lil Wayne - "Truffle Butter" 

BEST LIVE PERFORMER
  • Drake
  • J. Cole
  • Kanye West
  • Kendrick Lamar
  • Nicki Minaj


LYRICIST OF THE YEAR
  • Big Sean
  • Drake
  • J. Cole
  • Kendrick Lamar
  • Nicki Minaj


VIDEO DIRECTOR OF THE YEAR
  • Alan Ferguson
  • Benny Boom
  • Chris Robinson/Lil Chris
  • Colin Tilley
  • Director X


DJ OF THE YEAR
  • DJ Drama
  • DJ Envy
  • DJ Esco
  • DJ Khaled
  • DJ Mustard


PRODUCER OF THE YEAR
  • DJ Mustard
  • J. Cole
  • Kanye West
  • Mike Will Made-It
  • Pharrell Williams
  • Timbaland


MVP OF THE YEAR
  • Big Sean
  • Drake
  • Future
  • J. Cole
  • Kendrick Lamar
  • Nicki Minaj


TRACK OF THE YEAR
  • "Alright" - Produced By Pharrell Williams & Sounwave (Kendrick Lamar)
  • "Blessings" - Produced By Boi-1da & Vinylz (Big Sean FEATURING Drake & Kanye West)
  • "Commas" - Produced By Dj Spinz & Southside (Future)
  • "Idfwu" - Produced By Dj Dahi, Dj Mustard, Kanye West & Key Wane (Big Sean FEATURING E-40)
  • "Trap Queen" - Produced By Tony Fadd (Fetty Wap)


ALBUM OF THE YEAR
  • Big Sean - Dark Sky Paradise
  • Drake - If You're Reading This It's Too Late
  • J. Cole - 2014 Forest Hills Drive
  • Kendrick Lamar - To Pimp A Butterfly
  • Nicki Minaj - The Pinkprint
  • Wale - The Album About Nothing


WHO BLEW UP AWARD
  • Bobby Shmurda
  • Dej Loaf
  • Fetty Wap
  • Rae Sremmurd
  • Tink 

HUSTLER OF THE YEAR
  • Dr. Dre
  • Drake
  • J. Cole
  • Jay Z
  • Nicki Minaj


MADE-YOU-LOOK AWARD (BEST HIP HOP STYLE)
  • A$Ap Rocky
  • Dej Loaf
  • Drake
  • Kanye West
  • Nicki Minaj


BEST HIP HOP ONLINE SITE
  • Allhiphop.Com
  • Complex.Com
  • Hotnewhiphop.Com
  • Rapradar.Com
  • Worldstarhiphop.Com


BEST CLUB BANGER
  • Big Sean featuring E-40 - "Idfwu" (Produced By Dj Dahi, Dj Mustard, Kanye West & Key Wane)
  • Dej Loaf - "Try Me" (Produced By Dds)
  • Fetty Wap - "Trap Queen" (Produced By Tony Fadd)
  • Future - "Commas" (Produced By Dj Spinz & Southside)
  • Rich Homie Quan - "Flex" (Ooh, Ooh, Ooh) (Produced By Dj Spinz & Nitti Beatz)



BEST MIXTAPE
  • Future - 56 Nights
  • Future - Beast Mode
  • Future - Monster
  • Lil Wayne - Sorry 4 The Wait 2
  • Travis Scott - Days Before Rodeo
  •  

SWEET 16: BEST FEATURED VERSE
  • Drake - "Blessings" (Big Sean Featuring Drake & Kanye West)
  • Drake - "My Way Remix" (Fetty Wap Featuring Drake)
  • E-40 - "Idfwu" (Big Sean Featuring E-40)
  • Kendrick Lamar - "Classic Man Remix" (Jidenna featuring Kendrick Lamar)
  • Lil Wayne - "Truffle Butter" (Nicki Minaj featuring Drake & Lil Wayne)


IMPACT TRACK
  • Big Sean featuring Kanye West & John Legend - "One Man Can Change The World"
  • Common & John Legend - "Glory" (From The Motion Picture "Selma")
  • J. Cole - "Apparently"
  • J. Cole - "Be Free"
  • Kendrick Lamar - "Alright"


PEOPLE'S CHAMP AWARD
  • Big Sean featuring Drake & Kanye West - "Blessings"
  • Fetty Wap - "Trap Queen"
  • Future - "Commas"
  • Kendrick Lamar - "I''
  • Rae Sremmurd - "No Type"
  • Rich Homie Quan - "Flex (Ooh, Ooh, Ooh)"

KIMENUKA TWITTER: NI AUNT EZEKIEL TENA !!!

2:52:00 AM Add Comment

SIKU Ya Jana taarifa ziliznza kuzagaa kuwa, Aunt Ezekiel, Msanii wa Bongo Muvi, ambaye alikuwa akimsupport Mgombea Urais Kupitia CHADEMA-UKAWA, amepiga Chini UKAWA, na Kuhamia CCM.

Kwa Mujibu wa Taarifa ambazo tunazinukuu kutoka kwa Steve Nyerere, ni kwamba Hata Vicent Kigosi- Ray, pia amejiunga na Wana CCM.

Sasa, mapema Leo katika account yake ya Twitter, Aunt Ezekiel ameandika kama ifuatavyo huku Baadhi ya Tweet zikimlenga JACQUELINE WOLPER.







LUSHOTO KUTOKUPIGA KURA

2:26:00 AM Add Comment




TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema wananchi wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga, hawatapiga kura ya kuchagua mbunge katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.

Hatua hiyo, inatokana na kufariki dunia kwa aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Mohamed Mtoi (39). Mtoi, alifariki dunia Jumamosi iliyopita baada ya gari lake alilokuwa akisafiria kuacha njia na kupinduka kisha kudumbukia kwenye korongo wilayani Lushoto.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema sheria inaruhusu kama mgombea atafariki dunia wakati huu wa uchaguzi uahirishwe. “Wananchi wa Lushoto hawatapiga kura ya mbunge Oktoba 25, tumeahirisha hadi hapo baadaye tutakapowatangazia na chama husika kitapokuwa kimepata mgombea,” alisema Jaji Lubuva.

Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Zubery Mwombeji, Mtoi alipata ajali katika eneo la Magamba Coast, Kata ya Magamba wilayani Lushoto.

Alisema gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Miraj Nuru (43), likitokea Tarafa ya Mlola kwenda Mkuzi baada ya kumaliza shughuli za kampeni.

MNADA BANNER