REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

FAHAMU SABABU YA WAKAZI KUTOA SINGLE MBILI KWA WAKATI MMOJA

12:53:00 AM Add Comment



Na Baba Juti

RAPPER Wakazi amedai kuwa, siku hizi huwa anatoa Single Mbili kwa wakati mmoja, hasa katika Kuwalenga mashabiki zake wa aina mbali mbali

Kupitia Ukurasa wake wa Facebook, Wakazi aliandika Kuwa, hivi sasa anatoa Nyimbo Mbili kwa wakati mmoja, na Mikwaju hiyo, Moja Inakuwa katika Lugha ya Kiswahili, na Nyingine ikiwa katika Lugha ya Kiingereza

Aidha darasa amedai kuwa, katika mashabiki zake Wote, Wapo ambao wanapenda akirap Kwa Lugha ya Kiingereza, na Wengine Hupenda akiwa anarap katika Lugha ya Kiswahili


TUNAMNUKUU
“Siku hizi huwa natoa single Mbili kwa wakati mmoja ili kulenga fans tofauti wa Muziki wangu. Wapo wanaopenda nikirap kwa English na wapo wanaopenda nikirap kwa kiswahili. Je nyie mnaonaje niendelee na mfumo huo huo au tuchanganye ki Bilingual-flow?! What Yall think ...”

Instagram; @babajuti

WAKAZI:BARAKAH DA PRINCE ATASIKIKA KATIKA ALBAM YANGU

12:42:00 AM Add Comment



Na Baba Juti.
MKALI kutoka Jijini Mwanza, ambaye anakuja kwa Kasi ya Ajabu katika Muziki wa Kizazi Kipya (Bongo Flava), BARAKAH DA PRINCE, anazidi kung’ara katika “Kolabo”.

Barakah ambaye Hivi sasa anafanya Poa na Mkwaju wa NIVUMILIE aliomshirikisha RUBBY, atasikika katika albam ya Rapper WAKAZI, ambayo itashuka Sokoni Mara Baada tu ya Kukamilika.

Kupitia Ukurasa Wake wa FACEBOOK, wakazi alipost Picha yake akiwa na Barakah Da Prince, Studio, huku akitoa taarifa kuwa, Msanii huyo ni moja kati ya  Wasanii watakaokuwepo katika Albam Yake.

Tofauti na Hilo, WAKAZI amekazia kuwa, Vitu alivyovifanya Barakah katika Kolabo yao, ni vya ajabu sana, hivyo hatuna budi kuskilizia.

Ninamnukuu WAKAZI:
“Barakah Da Prince ni Moja Ya Wasanii ambao watakuwepo kwenye album yangu... Kafanya vitu amazing sana, I can't wait for you to hear the song. Can you guess who else is in it so far??!”

TUNASUBIRI !!!!!!

Instagram @babajuti

RICK ROSS AMEMALIZA KIFUNGO CHA NYUMBANI

12:30:00 AM Add Comment



Na Baba Juti
BAADA ya Kupigwa Kifungo Cha Nyumbani, hatimaye Big Bous wa MMG-Rick Ross a.k.a ROZAY, hivi sasa yuko Huru Kupiga Misele Mitaani kama kawaida

Rozay alipewa Kifungo Hicho Kufuatia Madai ya Kumpiga na Kumteka Mfanyakazi na Muangalizi wa Bustani yake katika Jumba Lake, huku Kitako cha bastola Kikidaiwa Kuhusika.

Kwa Mujibu wa hakimu ambaye alikuwa akisikiliza Kesi Hiyo, Rozay Hivi sasa Yuko Huru Kutoka Ndani ya Nyumba yake, na hata kufanya Shughuli zake Mbali mbali ikiwemo Muziki na  mengineyo

Instagram: @babajuti

LIL WAYNE ANARUDI TENA

12:27:00 AM Add Comment

Na Baba Juti
MWAKA 2009, Rapper Dwayne Carter Jr.- Lil Wayne, aliachia Mixtape Kali ambayo ilitambulika kwa jina la NO CEILINGS, na kila mtu aliichangamkia balaa.

Baada ya Ukimya Kidogo wa hapa na pale, Hurrraaaaaay, hatimaye Weezy ametangaza Ujio wa Mixtape Mpya ambayo ameipa Muendelezo , yaani NO CEILINGS 2, na inatarajiwa kudrop Sokoni Mnamo November 26, ikiwa Ni siku maalum ya THANKS GIVING
Weezy F baby alitoa Taarifa Hiyo kupitia Account yake ya Twitter, ambapo aliandika “Let's do it...Thxgiving...lets eat!”

Awali, Tunech alionekana akirap katika Mkwaju wa Drake BACK TO BACK, kisha akaonekana akirapm katika Mkwaju Wa Dreezy na Future JUMPMAN, hali iliyozua Maswali Kibao kwa Mashabiki Wake.

So, Ladiezzzz….and Gentooozzzz.. Get Ready For This

MNADA BANNER