REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KUHUSU CIARA KUMSHTAKI FUTURE KWA KUMDHARIRISHA.

1:19:00 AM
Zahir, Ciara na Future

Na Baba Juti
CIARA amechukua Jukumu la Kumshtaki Mzazi Mwenzake Rapper Future, ambaye walikuwa katika Mahusiano kipindi cha Nyuma na Mwisho wake kupigana Chini

STORY ILIVYOKUWA.
SIKU chache zilizokata , Future alitweet katika account yake ya Twitter  kuwa Ciara amekuwa akimbania kuonana na Mtoto wao Zahir, kitu ambacho anadai kinamuuma, na anahitaji kuonana na Wanasheria ili apate msaada.

Lakini katika Malalamiko hayo, Future alitumia maneno makali kama vile "kahaba", jambo ambalo lilimfanya Kila Mtu aanze kumpondea Ciara kwa hali hiyo.

HIVI SASA !!
BAADA ya kukutana na Kauli hiyo Mbaya, na hata kuitwa jina Baya, Ciara, amechukua Uamuzi wa kufunga Masghtaka Dhidi ya Future, kwa madai kuwa, amedharirishwa, na hayuko tayari kulivumilia hilo Suala.

Tofauti na Hilo, Katika madai yake, Ciara anaomba kulipwa USD Million 15 kwa madai kuwa amedhalilishwa na ameathirika Kisaikolojia.

CHA AJABU SASA!
Kutokana na malalamiko ya Future, na Hatua Ya Ciara Kuingia Mahakamani Kufungua Mashtaka, Still mashabiki wa Future wanazidi kumuandama na kumjia Juu Ciara kuwa hakustahili kufanya hivyo, bali anafanya maamuzi hayo sababu hana Mkwanja, na hata kimuziki hafanyi poa,

Tofauti na hayo, picha na Video Clip za Utani zimeanza kuhit Mitandao ya Kijamii, kumtania na hata Kumcheka Ciara kwa uamuzi aliouchukua dhidi ya Baba wa Mtoto wake, Future.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER