REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

BAADA YA KUSHINDWA KUPUMUA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI, BMX AKANUSHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA

1:23:00 AM

SIKU ya Jumatatu ziliibuka Taarifa za Uhakika Kuwa, DMX alikimbizwa Hospitali baada ya Kuzidiwa na tatizo la Kifua Kubana (Asthma)

Kwa Mujibu wa Mtu aliyekuwa naye, Inasemekana kuwa, Tukio hilo lilimtokea Rapper DMX Nje ya Chumba cha Hotel ya RAMADA YONKERS iliyoko New York Marekani, ambapo alianza kukosa Pumzi na hata kupoteza Fahamu

Kutokana na Hali hiyo, DMX alidondoka Chini, hali iliyowafanya wamkimbize Hospitali ili kuoka Maisha yake, ambapo Gari la Msaada lilifika na kumchukua.

MADAI YALIYOTOKA.
BAADA ya Taarifa Hizo kuwafikia Walimwengu, DMX alianza kutajwa kuwa, alikutana na hali hiyo kutokana na kutumia na hata kuzidiwa na Dawa za Kulevya

Kwa Mujibu wa Shahidi ambaye alikuwa akitoa Ushuhuda kwa askari Polisi aliyekuwepo eneo la Tukio, inasemekana kuwa, DMX alionekana akijindunga Sindano ambayo ilikuwa na Dawa Za Kulevya.

MAJIBU YA DMX.
MARA Baada ya Kurudi katika Hali yake ya Kawaida, DMX anadai kuwa, hakuwa ametumia Dawa za Kulevya kama ambavyo shahidi amezungumza, bali ana Tatizo la Asthma kama ambavyo imeshawahi kufahamika

Tofauti na hilo, Familia ya DMX inasema kuwa, Mkali huyo baada ya kugundua kuwa anaanza kukosa Pumzi, basi aliomba Kifaa cha Kusaidia kupumua.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI
DMX hatofunguliwa Mashtaka ya Matumizi ya dawa za Kulevya au umiliki Dawa za Kulevya maana vipimo vinadhihirisha kuwa hakutumia vitu Hivyo bali ni Asthma tu

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER