Na Hamza Mashole
wa Songea
Kampuni ya GAME
FRONTIERS OF TANZANIA kwa kushirikiana askari wanyamapori wa Selou na Askari wa
vijiji vinavyozunguka pori la Akiba la Selou wamefanikiwa kukamata meno ya
tembo 15 yenye thamani ya milion miambili, Risasi 9, Bunduki moja aina ya
RIFFLE 458 na Gobole moja ambavyo hutumika kuulia wanyama .
Doria hiyo imechukua takribani siku tatu katika pori la
Akiba la Selou ikiwa ni sehemu ya kuwatafuta majangili wanaofanya mauaji ya
wanyamapori katika pori hilo,
Akizungumza na mwandishi wetu Bw. Mohamed Mpapa ambaye ni
mwakilishi wa kampuni hiyo ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA, Amesema kuwa hiyo ni
kujituma kutokana na motisha ya fedha anayoitoa mwezeshaji wa kampuni ya GAME
FRONTIERS OF TANZANIA ndio chachu ya mafanikio ya kukamata meno,bunduki na
risasi.
Akiendelea
kuzungumzia tukio hilo Bw. Mohamed Mpapa amesmea baada ya majangili kuwaona
Game Frontiers Tanzania wakiwa katika doria ndani ya pori hilo huku wakiwa
wamekamilika kimapigano majangili hao waliweza kukimbia na kuacha nyara hizo
baada ya kuona nguvu yao ni ndogo katika kupambana na kundi la doria.
Ameongezea kwa kusema Kampuni yake imefurahishwa na
mafanikio na ushirikiano uliopo kati yao, Serikali na wanavijiji kukabiliana na
ujangili unaoendelea kuwamaliza tembo katika Pori la Akiba la Selou pia ametoa
wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kuwafichua majangili.
Nae Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba
la Selou Bw. Bernald Lijaji amesema Pembe zilizokamatwa ni 15 pamoja na Bunduki
aina ya RIFLE 458,Gobole moja na Risasi 9 aina ya 458 vimekamatwa katika Doria
iliyofadhiriwa na Mwekezaji wa Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA
EmoticonEmoticon