TWENDE TUKAJIONEE: Rais wa Kenya, Mwai Kibaki (wapili kutoka kulia) akiwa na
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kutoka
kushoto), Mkuu wa Magereza nchini,
Kamishna Jenerali John Minja (kulia) pamoja na maofisa mbalimbali kutoka nchini
na Kenya, wakiingia ndani ya kiwanda hicho.
SALAM YA KENYA NA TANZANIA: Rais wa Kenya, Mwai Kibaki (kushoto) akimsalimia Mkuu wa Jeshi la Magareza nchini, Kamishna Jenerali John Minja kabla ya kuingia ndani ya Kiwanda cha Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam. Wa pili kutoka kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, anayefuata ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.
KITI CHA WAPENDANAO: Rais Mwai Kibaki (wa kwanza kutoka kulia aliyevaa tai) akiwafurahia Askari Magereza na ofisa kutoka nchini Kenya wakiwa wamekaa kwenye kiti cha wapendanao kilichotengenezwa na wafungwa kiwandani humo.
PAMOJA: Rais Mwai Kibaki akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali nchini pamoja na maofisa kutoka nchini Kenya.
HAKIKA NIMEJIONEA MWENYEWE: Rais Mwai Kibaki (wa
pili kushoto) akiwa na maofisa mbalimbali wakiondoka Kiwanda cha Magereza
Ukonga baada ya kumaliza kuangalia vifaa mbalimbali vinavyotengenezwa na
kiwanda hicho.
PICHA ZOTE NA
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
EmoticonEmoticon