BEIJING
Wakati Dunia nzima ikiadhimisha Sikukuu ya Krismas,Polisi ya China imewaokoa watoto 89 na kuwatia mbaroni
watuhumiwa 355 tokea wiki iliopita kufuatia msako wa taifa zima dhidi wa
wasafirishaji watoto kwa njia ya magendo.
Chen Shiqu mkuu wa kitengo cha kupambana na usafirishaji wa
watoto kinyume na sheria katika Wizara ya Usalama wa Wananchi amekaririwa
akisema kwamba polisi imefanya operesheni ya pamoja katika majimbo tisa hasa
yale ya kusini kuanzia Disemba 18 kupambana na makundi yenye kujishughulisha na
usafirishaji huo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali Xinhua maafisa
wa serikali za mitaa wanawahudumia watoto hao kwa hivi sasa wakati polisi
ikifanya juhudi za kuwatambuwa wazazi wao. Chen amesema chembe hai za urithi
zitachukuliwa kutoka kwa watoto hao ili kuwatambuwa wazazi wao kupitia data za
DNA za taifa zilizowekwa kwa ajili ya kupambana na usafirishaji wa watoto ulio
kinyume na sheria.
Mtoto mchanga wa kiume hununuliwa kwa takriban yuan sarafu
za Kichina 30,000 sawa na dola 4,800 katika maeneo ya kimaskini na huuzwa kwa
yuan 11,000 katika majimbo yenye utajiri kama vile Fujian na jimbo jirani na
hilo la Guangdong.
Kwa mujibu wa Chen msako wa polisi wa taifa zima umeyavunja
magenge 11,000 yenye kujihusisha na usafirishaji watoto kinyume na sheria
katika mfulululizo wa kampeni tokea mwezi wa April mwaka 2009.
CHANZO : DEUTSCHE WELLE
EmoticonEmoticon