Afisa wa polisi ameuawa kwa kupigwa risasi na bunduki yake
kuibwa, katika shambulizi mjini Mandera karibu na mpaka wa Kenya na Somalia.
Kwa Mujibu wa Taarifa zilizothibitika kutoka Nchini Kenya,
imesemekana kuwa Afisa huyo wa Polisi alikuwa katika doria pamoja na wenzake wakati waliposhambuliwa saa tatu
usiku wa alhamisi, huku mwenzake huyo
akipona kuuawa na pia hakujeruhiwa.
Maafisa wa polisi wanasema ujumbe uliopatikana kutoka kwa
wanachama wa kundi hilo unaonyesha kuwa kundi hilo liko tayari kutoa shilingi
890 000 kwa kila mwanamgambo anayemuua afisa mmoja wa usalama wa Kenya.
Zaidi ya maafisa 20 wa usalama katika eneo la Kaskazini
Mashariki wameuawa katika mashambulizi yanayoaminika kutekelezwa na wanamgambo
wa Al Shabaab.
EmoticonEmoticon