Askari wa upelelezi akifanya vipimo eneo la tukio, mahali ambapo inasadikika Mvamizi alijichoma moto
NA New Vision, KAMPALA & Frank Joachim
Baba mzazi wa mtu aliyejulikana kama Robert Karamagi ambaye
alifariki kutokana na majeraha ya kuungua kwa moto kwa kile kinachoaminika
kuchomwa kwa makusudi ndani ya nyumba ya mwanamuziki Jose Chameleone wa Uganda
ameibuka na kusema mtoto wake hakujilipua mwenyewe kama inavyodaiwa.
Karamagi aliyekuwa na umri wa miaka 27 alifariki katika
hospitali ya Mulago saa chache baada ya kufikishwa hapo na kulazwa.
Matukio yaliyosababisha Karamagi aliyevamia nyumba ya msanii
huyo kukumbwa na mkasa huo bado ni kitendawili huko mke wa Chameleone Bi.
Daniella akisisitiza kuwa Karamagi alijitia moto mwenyewe alipotaka kujaribi
kumchoma bibie huyo.
Lakini baba wa mtu huyo Meja Benedict Kyamanywa amepingana
na ripoti kuwa mwanawe alijichoma moto mwenyewe.
Amesisitiza kuwa mwanaye alifungwa kwa kamba na kuchomwa
moto ndani ya makazi ya mwanamuziki huyo.
Ameongoza kuwa kabla mwanaye huyo hajakata roho alimuambia
kuwa alifungwa kamba na kuchomwa na mafuta ya ndege.
Hata hivyo katika hatua nyingine Meja Kyamanywa ambaye ni
daktari msaidizi wa Kakiri Barracks amesema kuwa mtoto wa alikuwa na matatizo
ya akili, na kuwa kijiji kizima kilikuwa kinajua akiwemo Chameleone mwenyewe.
EmoticonEmoticon