MWANAFUNZI wa
kidato cha tatu katika shule ya
Sekondari ya Tongoni nje kidogo ya jiji la
Tanga, (jina tunalihifadhi)
amekutwa amekufa ndani ya nyumba ya kulala wageni alikopelekwa kutolewa mimba
bila mafanikio.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Constantine Massawe mwanafunzi huyo
alikutwa amekufa juzi katika nyumba ya kulala wageni iliyopo barabara ya 21
jijini Tanga.
Mmoja wa wahudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni ambaye
aliomba jina lake lihifadhiwe alisema kwamba mwanafunzi huyo aliingia saa 4.00
asubuhi siku ya tukio akiwa ameambatana na kijana mmoja wakakodi chumba.
“Baadaye alikuja mwanaume mmoja wa makamo ambaye alituuliza
kama wameingia mwanafunzi huyo na mwenzake, tulipomwonyesha chumba walichoingia naye akakodi chumba cha jirani
ndipo tukaona wote wakijifungia kwenye chumba kimoja,” alisema mhudumu.
Mhudumu huyo alisema baada ya muda wa saa moja, mvulana na
mzee huyo wakaaga kwamba wanatoka huku wakisema kwamba msichana amebaki chumbani
akiwa amepumzika. Akithibitisha habari hizi, Kamanda Massawe alisema taarifa ya
tukio hilo ilitolewa na mhudumu wa nyumba hiyo ya kulala wageni katika Kituo
cha Polisi cha Chumbageni Jijini Tanga.
“Tatizo ni kwamba nyumba hii ya wageni wahudumu wake hawakuwapa
wageni hao daftari ili waorodheshe majina yao hivyo inakuwa vigumu kuwafahamu,” alisema Kamanda Massawe na
kufafanua kuwa alifariki akitolewa mimba ya mwezi mmoja.
Kamanda Massawe alisema mpaka sasa hakuna mtu aliyekamatwa
na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na kifo
hicho.
Na: Raisa Said, Tanga
EmoticonEmoticon